Lowassa kuchunguza Ufisadi Meremeta! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa kuchunguza Ufisadi Meremeta!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Matola, Sep 3, 2011.

 1. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Friday, 02 September 2011

  [​IMG]

  NI KAMPUNI YENYE UHUSIANO NA JWTZ, ZITTO AHOFU USIRI KUTAWALA

  UCHUNGUZI wa Bunge kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh205.9 bilioni unaodaiwa kufanywa kupitia Kampuni ya Meremeta iliyokuwa ikimilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), umeingia katika sura mpya baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhamishia jukumu hilo katika Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa.

  Awali, Spika alikuwa amepeleka suala hilo katika Kamati ya Nishati na Madini ili lifanyiwe kazi na Kamati Ndogo ambayo imepewa kibali cha kufanyia kazi sekta ya gesi hasa nafasi ya Kampuni ya Pan African Energy katika uzalishaji na usambazaji wa gesi nchini.

  Hata hivyo, taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel zinasema Spika Makinda alibatilisha uamuzi wake wa awali, hivyo kuamua kupeleka suala hilo katika Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
  "Ni kweli suala la Meremeta Spika amelihamishia Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, maana hiyo ndiyo inayohusika na masuala hayo, nadhani watakuwa wameshapewa taarifa," alisema na kuongeza:

  "Kamati hiyo ndiyo hasa inayohusika na suala hilo la Meremeta, hivyo baada ya uamuzi wa Spika niliijulisha Idara ya Shughuli za Bunge, pengine watakuwa wameshaitaarifu kamati hiyo, naomba unitafute kuanzia tarehe 9 (Septemba) nitakuwa nimefahamu ‘position' (nafasi) ya kila kamati iliyopangiwa kazi na Spika."

  Zitto ahofia

  Hata hivyo, mwasisi wa hoja hiyo ya kuchunguzwa kwa Meremeta, Zitto Kabwe alisema juzi kuwa ameshtushwa na uamuzi huo wa Spika na kwamba anahofia huenda taarifa hiyo isiwekwe wazi kwa umma.

  Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini (Chadema), ameonyesha hofu hiyo ya kuwapo kwa usiri pengine kutokana na kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwahi kusema bungeni kwamba ni bora asulubiwe kuliko kutoa siri za Meremeta hadharani, kwani kufanya hivyo ni kuanika hadharani siri za JWTZ na Usalama wa Taifa.

  Hoja inayotakiwa kufanyiwa kazi na Kamati hiyo inayoongozwa na Lowassa ni kuchunguza uhalali wa malipo ya dola milioni 132 (wastani wa Sh205.9 bilioni kwa viwango cha sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Sh1,560 dhidi ya Dola ya Marekani) ambazo zilitoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenda Ned Bank ya Afrika Kusini ikiwa ni malipo ya mkopo wa Dola 10 milioni, uliokuwa umechukuliwa na Kampuni ya Meremeta Ltd.

  Kumekuwa na mvutano baina ya wabunge tangu enzi za Bunge la Tisa na Serikali kuhusu kufanyika kwa uchunguzi ndani ya Meremeta kwa maelezo kwamba suala hilo linagusa masuala ya usalama wa nchi.

  Habari zilizopatikana zinasema hoja hiyo ndiyo iliyosababisha Spika Makinda kuhamishia uchunguzi wake kutoka Kamati ya Nishati na Madini kwenda Kamati inayohusika na masuala ya ulinzi na usalama wa nchi.

  Zitto akizungumzia uchunguzi huo, alikiri kupata barua kutoka kwa Spika Makinda kwamba suala hilo limehamishiwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama lakini akasema hofu yake ni iwapo taarifa ya matokeo ya uchunguzi huo "itawekwa wazi kwa Bunge na umma."

  Alisema awali alipongeza uamuzi wa Spika wa suala hilo kufanyiwa kazi na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kwa sababu alifahamu kwamba mambo yote yatakayobainika yangewekwa wazi, lakini akahofu kwamba uwazi huo hauwezi kuwepo katika Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

  "Nasema nimeshutushwa na uamuzi wa Spika kwa sababu awali, suala hili lilikuwa liundiwe Kamati Teule ya Bunge kama nilivyoomba, lakini kwa busara zake, Spika akaamua lipelekwe Kamati ya Nishati na Madini ambako mimi nilidhani alikuwa sahihi sana," alisema Zitto na kuongeza:

  "Lakini katika kamati hii ya masuala ya Ulinzi na Usalama, sidhani kama kutakuwa na uwazi, kwa nini… wewe unafahamu kwamba mambo ya ulinzi na usalama huwa wanasema taarifa zao ni za siri, sidhani hapo kama kutakuwa na uwazi wa kusema kile kilichotokea na fedha za walipa kodi kufujwa kiasi kile."

  Uzoefu wa utendaji wa Kamati za Bunge, unathibitisha kuwapo kwa usiri mkubwa ndani ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ukitiliwa nguvu na nyongeza ya saba katika kanuni za Bunge toleo la 2007 zinazoiweka kamati hiyo kuwa miongoni mwa kamati zinazotakiwa kufanya kazi zake kwa faragha.

  Zitto alisema kwa kuzingatia maslahi ya taifa ndani ya suala hilo la Meremeta, ikiwa Kamati iliyopewa jukumu hilo itaamua kuunda kamati ndogo, basi Lowassa anapaswa kuunda timu imara ambayo itafanya kazi yake kwa maslahi ya umma.

  "Mimi niko tayari kushirikiana na kamati ya Mheshimiwa Lowassa kwa kuwapa vielelezo vyote nilivyo navyo ambavyo vitawezesha kufanya kazi yao vizuri, nitafanya hivi kwa sababu fedha zilizopotea hapa ni nyingi mno, wakilegea hatutaweza ku -achieve (kufanikisha) kile ambacho tulikusudia," alisema Zitto.

  Kauli ya Lowassa

  Kwa upande wake, Lowassa akizungumza kwa simu alisema bado hajapata taarifa rasmi iwapo suala la uchunguzi wa Meremeta limewekwa chini ya kamati anayoiongoza."Kwa kweli sina taarifa hizo, ujue mimi niliondoka mapema pale Dodoma na hadi naondoka sikuwa nimepewa taarifa hizo, ngoja nitafuatilia kesho (jana) ili nifahamu usahihi wa taarifa hiyo," alisema Lowassa.

  Kwa sababu hiyo, hadi sasa haijafahamika iwapo Kamati hiyo ikishapewa taarifa hizo itaunda kamati ndogo kuchunguza suala hilo au italifanyia kazi ikiwa na wajumbe wake wote.

  Kanuni ya 114 fasili ya 18 ya Kanuni za Bunge toleo la 2007 inaruhusu Kamati za Kudumu za Bunge kuunda kamati ndogo, kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli zake kadri itakavyoona inafaa.

  "Kamati yoyote inaweza kuunda kamati ndogo kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zake, kadri itakavyoona inafaa na kila kamati ndogo itapangiwa kazi zake na kamati ya kudumu husika," inaeleza sehemu ya kanuni hizo.

  Chimbuko la Uchunguzi

  Zitto alianzisha hoja ya kuchunguzwa kwa Meremeta alipowasilisha barua kwa Katibu wa Bunge akitoa taarifa ya hoja ya kuunda Kamati Teule kwa ajili ya kuchunguza tuhuma za ufisadi kupitia Kampuni hiyo ya uchimbaji wa dhahabu.

  Barua hiyo ilitanguliwa na taarifa yake ya mdomo aliyoitoa bungeni Julai 13, 2011 kwa mujibu wa Kanuni ya Bunge Namba 117 (2)-(a) inayomruhusu kutoa taarifa ya kusudio lake la kuwasilisha hoja ya kutaka Bunge liunde Kamati Teule.

  Mbunge huyo alimwandikia Spika Makinda barua kutoa taarifa ya hoja husika Julai 15, mwaka huu akisema: "Kuna haja ya kujua uhalali wa ongezeko la Dola 122milioni zilizoongezeka katika malipo yaliyofanywa."

  Historia ya Meremeta

  Serikali imekuwa haiko tayari kuzungumzia Maremeta kwa maelezo kwamba ni suala ambalo lina maslahi ya usalama kwa taifa.

  Awali, ilisema Meremeta Ltd ni kampuni ya Kitanzania iliyokuwa ikimilikiwa na JWTZ kwa ajili ya mradi wake wa Nyumbu, Mkoa wa Pwani huku taarifa za usajili zilizotolewa na Msajili wa Makampuni wa Uingereza na Wales zikisema kuwa kampuni hiyo iliandikishwa nchini humo mwaka 1997 na baadaye ilifilisiwa hukohuko mwaka 2006.

  Taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ya Mei 31, 2005 inabainisha kwamba Meremeta Ltd, ni tawi la kampuni ya kigeni iliyosajiliwa Tanzania, Oktoba 3, 1997 na kwamba hisa 50 za kampuni hiyo zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Triennex (Pty) Ltd. ya Afrika Kusini, wakati hisa 50 zilizobaki zilikuwa zinamilikiwa na Serikali ya Tanzania.

  Utata kuhusu umiliki wa Meremeta Ltd unatokana na taarifa ya Brela ambayo pia inazitambua kampuni mbili za Kiingereza, London Law Services Ltd na London Law Secretarial Ltd kuwa wamiliki wa hisa moja kila moja ndani ya Meremeta.

  Licha ya Serikali kutokuwa mmiliki pekee wa kampuni hiyo, BoT inadaiwa kuwa ililipa madeni yote ya Meremeta badala ya kusaidiana na na washirika wake ambao kisheria wanaonekana kuwa walikuwa wakimiliki hisa katika kampuni hiyo.

  Serikali Tanzania ilikuwa ikimiliki asilimia 50 ya hisa na kwa mujibu wa taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), uhalali wa malipo hayo ulikuwa na walakini kwani kiutaratibu Nedbank Ltd ilitakiwa iachwe idai fedha zake kutoka kwa mfilisi wa kampuni hiyo sawa na wadeni wengine.
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Just when you thought it's stopped raining, a hurricane has gotten under way...!!!
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  & Wonders shall never end in Tanzania,........
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  ....... A large thunders are heard everywhere .... so it means rain has just stopped but its not yetover . We are in rain forest.... teh teh teh teh
   
 5. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Yeye mwenyewe FISADI.
   
 6. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  nitarudi.........
   
 7. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,968
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Fisadi anapewa tenda ya kuchunguza ufisadi! What a joke! Ama kweli bongo mambo tambalale.
   
 8. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Kama anataka urais 2015, atafanya kweli! akichemka hapa asahau ndo litakuwa kaburi lake la kisiasa. I am watching him, lakini pia yawezekana dili limesukwa juu kwa juu na watu watakuwa busy kutafuta namna ya kutudanyanya ili kutuwin badala ya kufanya uchunguzi.
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mambo ya bongo bana, hata ukiwa na gunia la popcorn for a weekend utalimaliza whilst episode after episodes will still be rolling on!!!!!!!!!
   
 10. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  ''si nilisoma kuwa yu mgonjwa huyo ndugu!''
   
 11. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mchawi kapewa mtoto kulea.
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  you can cheat all the people for some time or some people all the time but you can not cheat all the people all the time...................
   
 13. ubun2

  ubun2 Senior Member

  #13
  Sep 3, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Does this current regime have credibility at all?

  From the Wikileaks cables one thing has emerged as consistent, that is Pres. Kikwete's reluctance/unwillingness in prosecuting ANY corrupt sharks within the TZ gvt:former/current.
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Sep 3, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Pinda: "Ni bora nisulubiwe kuliko kutoa siri za Meremeta hadharani, kwani kufanya hivyo ni kuanika hadharani siri za JWTZ na Usalama wa Taifa." Nchi hii haina viongozi ndugu zanguni!
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Sijawaelewa vizuri hapo juu, mmesema eti Lowassa huyu huy apewa jukumu la KUCHUNGUZA kitu hapa chini ya jua na wengine tuendelee tu kuamini kwamba kuna zoezi fulani lenye kuaminika linaendel kutendeka mahali sio??? My foot!!!!!!!!!!!

  Kumbe ndio maana kilio cha WALAZWAHOI nchini kimeanza kuandama kisawasawa kiasi hiki hasa kwa wale magwiji wa ufisadi chini kwa kasi kiasi hiki?????????

   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />probably we should change from tanzania to neverland...
   
 17. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,071
  Likes Received: 1,108
  Trophy Points: 280
  Someone is putting some dogshit on my goggles again.
   
 18. Jefe

  Jefe Member

  #18
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fisadi kuchunguza ufisadi, dah! hii kali yaani.any way let's see kama hatutoishia kupigwa changa la macho.
   
 19. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tz kwa vioja!Ivi kutakuwa na uchunguzi apo kweli?by the way enzi za meremeta EL alikuwa na cheo gani
   
 20. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #20
  Sep 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,997
  Likes Received: 2,653
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Hata mimi nashangaa leo amepona kabisa na kupewa majukumu?au sredi ya jana ilikuwa ya kizushi?
   
Loading...