Lowassa kawashinda CCM nzima na serikali yao

Lowassa kawashinda CCM nzima na serikali yao

Itabidi iwasubiri Mbowe na Kubenea pale watakapoamua kuupeleka ule ushahidi dhidi ya Lowasa. Polisi haiwezi kuwavamia au kuwakamata mbowe na Kubemea ili iwalazimishe watoe ushahidi walionao. Kutumia nguvu kupata ushahidi sio utawala bora.
mwakyembe...waziri wa sheria aliyetuambia lowasa ameiba anavyo vyombo vyote vya dola kwa nini anamwogopa lowasa?
 
Wwe nenda kwenye hoja. Kama ninyi ni serikali makini, mnajua Lowasa ni fisadi kwa nini hammfikishi mahakamani?

Vinginevyo unazidi kuonesha namna gani mnaweweseka na Lowasa hata kama hayuko ccm. Kuendelea kumuwewesekea mnathibitisha ni jinsi gani alivyojinamizi kwenu!.

La sivyo, mnajua ni mharifu, na ninyi mnaserikali, mpelekeni mahakamani akahukumiwe kama waharifu wengine.

Kuna mambo vijana wa kitanzania mnapaswa kuyafahamu,kwanza mfahamu kuwa dunia ina impunity ya hali ya juu. S tu Lowassa hafikishwi mahakamani kwa makosa yaliyodhahiri bali pia viongozi wengi wakuu duniani hawafikishwi mahakamani. Kuna sababu nyingi zikiwemo nguvu za magenge wanayoyatumikia. Kutofikishwa kwao hakumaanishi hawakutenda kinyume, hasha. Bali kunaonesha tatizo la mfumo wa utoaji haki duniani ulivyo. Mtu anayejishughulisha kufahamu magenge ya kihalifu duniani na mawakala wao atalifahamu hili.Wanaoshabikia wahalifu kama ilivyo Colombia na Mexico nao wapo radhi kuwatetea wahalifu hao kwani kwao kushabikia wahalifu ni starehe kama wengine wanavyoshabikia mpira.
 
Kinachonichekesha ni kwamba vilaza wa CCM wakiulizwa kwanini hawampeleki Lowasa Mahakamani wanakuwa kama mtu aliyefumaniwa na mke wa mtu. Wanabaki kuinamia chini tu. Ama kwa hakika ukiwa CCM ni lazima uwe na akili za kushikiwa.
 
Ndugu zangu tazameni hapa:-

Lowassa ni fisadi. Aliiba fedha kwa mfumo Richmond, serikali ilijua na iliogopa kumchukulia hatua. Amejiunga na upinzani hadi kugombea uraisi, serikali ya CCM inamwangalia na kuishia kuongelea uvunguni kwamba ni fisadi. Hakuna ajasiri wa kumfikisha mahakamani. Halafu bado serikali hii inajibainisha kwamba inatumikia wananchi kwa misingi ya haki na uzalendo.

Serikali imetumia majeshi yake yote kulinda maslahi ya CCM. Lakini haina uwezo wa kulinda maslahi ya taifa kwa kumfikisha Lowasa fisadi mbele ya sheria. Hapa ni dhahiri lowasa amewashinda Ccm na serikali yote ama serikali haina uwezo wala ujanja wa kupambana na ufisadi. adui wa tano wa maendeleo akifuatia nyuma ya Ccm yenyewe.

Lowassa amesema hadharani kwamba mwenye Richmond ni Jakaya Mrisho Kikwete, la ajabu Ccm na serikali yake, haina uwezo wa kushughulikana hili suala. Imeendelea kumfunika huyo aliyetajwa na kuzidi kulalamika juu ya ufisadi wa Lowasa lakini hakuna siku kafikishwa mahakamani ili aadhibiwe na mali ya taifa irudishwe kwa maslahi ya umma. Hiyo ni serikali.

Kumetokea ufisadi mwingi wa kutisha sana kama Escrow, Lugumi, EPA, na mingine mingi ambavyo washiriki wake ni wanachama wa ccm ama watumishi wa serikali ya ccm. Ccm haina ubavu wa kuongelea hayo wala haina mpango wa kuwachukulia hatua. Badala yake imefunika bunge lisitangazwe watu wasijue hayo mambo na hata mara nyingnine wabunge wamezuiliwa kuyaongelea hayo mambo. Lakini Ccm na serikali yake imekazana kusema Lowasa fisadi bila kumchukulia hatua. Serikali inalalamika badala ya kuchukua hatua. Ccm na serikali yake haina ubavu wa kumchukulia hatua Lowassa.

Leo wabunge wa ajabu kabisa wa CCM wanasema Uuzwaji wa nyumba usiongelewe kwa sababu na Lowassa alinunua. As if kununua nyumba za serikali ni kosa kuliko kuuza. Halafu lisisemwe kwa vile Lowassa alinunua nyumba. Lowassa kiboko ya Ccm na serikali yake kiasi kwamba hawana uwezo wa kugusa lolote alifanyalo wanaishia kulalamika.

Watanzania tunapata picha gani kuhusu CCM na serikali yake inayojiweka madarakani kwa hila huku haina uwezo wa kuongoza nchi?

Ama katika michango yetu, naomba tuongee kwa mifano halisi pale ambapo panathibitisha CCM kushindwa kuongoza nchi yetu kwa maslah ya taifa.

1. Ni kweil Lowassa ana nguvu kulilko CCM, Serikali yote na sheria zote kwamba hawana uweo wa kumfikisha mahakamani kwa ufisadi? Au wanaogopa vivuli vyao wenyewe? Kama siyo uoga, anayejibu aeleze ni kwa nini serikali na ccm yake wanamtaja fisadi wakati huo huo hawana uwezo wa kumfikisha kwenye sheria kama waharifu wengine.

2. CCM kupata kigugumizi kuzungumzia ufisadi na kuwachukulia hatua mafisadi waliodhahiri na kubaki kusema Lowasa lowasa. Wathibitishe kwamba Lowasa ni fisadi wa richmond, Escrow, Epa, Kagoda, Kiwira, Lugumi, Nida, N.K. Na kwa nini hafikishwi mahakamani?

Wenye uelewe waongee constructively huku mkisite relevant examples na nini kifanyike.

LOWASA AMEASHINDWA, CCM NA SERIKALI YAKE HAWATAKI KUONGELEA UFISADI MWINGINE LOWASSA NA BADO HAWANA UBAVU WA KUMSHITAKI.

HII NI SERIKALI AMA MAANDALIZI YA MAZISHI YA TAIFA LA TANZANIA?
Siasa za maneno matupu zilishaisha, huu ni mda wa siasa vitendo kwa wananchi.
Hizi tamthilia za JK, JPM, Lowasa n.k haziwezi kuisha.
Tumia uo ubunifu wa kuandika kujiingizia kipato ndugu, hii nchi ni zaidi ya uijuavyo.
 
mwakyembe...waziri wa sheria aliyetuambia lowasa ameiba anavyo vyombo vyote vya dola kwa nini anamwogopa lowasa?
Yeye alimwambia apime kisha achukuwe hatua. Baada ya kusikia mbowe na kubenea wanao ushahidi mh Kikwete alimwambia Lowasa anateuwa waziri mkuu mwingine. Ndipo Lowasa akatangazia umma hicho mnachoita kujiuzuru.
Mwakyembe aliangalia swala la uwajibikaji katuka utendaji wa serikali wakati wa kushughulikia uhaba wa umeme na taarifa yake mliisoma.
Mbowe na Kubenea na wanachadema wote mlisema Lowasa ni mlarushwa mkubwa na ubadhilifu. Tuhuma hizi ni jinai ya kupelekwa Takukuru au polisi. Mbowe na Kubenea hawakufanya hivyo. Sasa mnataka Lowasa apelekwe mahakamani wakati hamtaki Mbowe na Kubenea kutoa ushahidi.
 
Wewe una akili sana unatakiwa kuwashauri CDM waachane na makapi ya Ccm ama siyo tutawaona na wao vilaza zaidi ya Lumumba. Haiji akilini mtu kwenda kwa kumchukua kilaza mmoja kutoka ktk kundi la vilaza na ukamweka mgombea urais. Ndiyo maana tulikosa mabadiliko tuliyoyataka maana watanzania si vilaza waliamua kubaki na vilaza waliobaki ccm maana ccm walijitetea kwa kutumia ari moja vilaza tumewapeleka upinzani. Unakumbuka nini mkapa aliwaita UKAWA?
Sasa sisi MALOFA Ilani yetu ya Uchaguzi inamuunga Mkono Warioba Inataka katiba Mpya Nyie hamjaliweka ili Muendeleze UDIKITETA wenu vzuri Eheeee yana Mwisho haya
 
Sasa sisi MALOFA Ilani yetu ya Uchaguzi inamuunga Mkono Warioba Inataka katiba Mpya Nyie hamjaliweka ili Muendeleze UDIKITETA wenu vzuri Eheeee yana Mwisho haya
Kaka mbona hujaelewa hoja yangu? Shule ulielewana na mwalimu kweli? wakati magufuli anaanza kazi si mlisema kua anaitumia ilani yenu ya Uchaguzi pia mbona sasa mnamkataa ama anatumia yenu wananchi wakimsifu inapotokea kuna mapungufu anatumia Ilani ya CCM umesema mwenyewe na kujiita ni lofa na hapo ndo ulofa wako unajionyesha, mimi sijakuita lofa though.
 
Hivi kama Lowasa, Kingunge, Sumae ni vilaza, basi ccm imebaki na mizoga inayonuka kwa sababu hao ndio walikuwa Cream ya awali hadi mkawapa uwaziri mkuu na uongozi wakitaifa.

Ongelea hoja ya ufisadi kwa sababu tukianza kuangalia ukilaza, utabakia uchi mjomba. Kwa nini hamuwapeleki mahakamani kwa ufisadi? Au ni kwa sababu ya ukilaza wenu kama Agness Marwa hivyo hamna uwezo hata wa kuwagusa kwa sababu nyinyi ndio vilaza wafu?
Siwezi kuongelea ufisadi maana kuzungumzia ufisadi kwa hoja na mwanachadema ni sawa na kwenda milembe kuzungumza na wale wagonjwa maana hii hoja kwa CDM imeshakwisha, aliondoka nayo Slaa na Zitto.
 
Siwezi kuongelea ufisadi maana kuzungumzia ufisadi kwa hoja na mwanachadema ni sawa na kwenda milembe kuzungumza na wale wagonjwa maana hii hoja kwa CDM imeshakwisha, aliondoka nayo Slaa na Zitto.

Wewe peleka hao mafisadi mahakamani. unaloloma nini? Nani anahitaji kusikia mawazo yako ya kiwenda wazimu hapa? Utajisafisha tu kwa kuwachukulia hatua. Kinyume cha pale ni sawa na kujipaka kinyesi halafu unalaumu nzi wanakufuata!. Kwanza nani anaongelea habari ya chama hapa? Tunaongelea serikali inayoshindwa kuwachuklia hatua majizi na kubaki kulalamika. Wewe mbwiga nini usiyeelewa hoja?
 
Hapo ndiyo uwezo wako wa kufikiri umefika kikomo. Matusi mara nyingi hutumiwa na watu wanaoutoa hoja.
 
Kuna wengine wanadokeza kwamba lowassa ana uwezo wa kusambaratisha ccm kwa masaa pungufu ya 24 , akitaka , wanasema mpaka sasa ccm iko kwenye kiganja chake tena cha mkono wa kushoto !
Hahahaaaaaaaaaaaaa.Yani hizi akili za wafuasi wa Lowassa zinahitaji maombi.
 
Lowassa hahusiki na ufisadi wa richmond ndo maana ana relax tu.Serikali imeshatuma watu wake wa vitengo vyote vya usalama kuchunguza richmond wamekutana na mambo ya kuogofya maana wahusika wakuu ni vigogo wa juu serikalini na hawagusiki kamwe.
 
Kaka mbona hujaelewa hoja yangu? Shule ulielewana na mwalimu kweli? wakati magufuli anaanza kazi si mlisema kua anaitumia ilani yenu ya Uchaguzi pia mbona sasa mnamkataa ama anatumia yenu wananchi wakimsifu inapotokea kuna mapungufu anatumia Ilani ya CCM umesema mwenyewe na kujiita ni lofa na hapo ndo ulofa wako unajionyesha, mimi sijakuita lofa though.
Tatizo lake hanaitumia huku anakurupuka Ndio Maana Anafell Muda utaongea
 
Wwe nenda kwenye hoja. Kama ninyi ni serikali makini, mnajua Lowasa ni fisadi kwa nini hammfikishi mahakamani?

Vinginevyo unazidi kuonesha namna gani mnaweweseka na Lowasa hata kama hayuko ccm. Kuendelea kumuwewesekea mnathibitisha ni jinsi gani alivyojinamizi kwenu!.

La sivyo, mnajua ni mharifu, na ninyi mnaserikali, mpelekeni mahakamani akahukumiwe kama waharifu wengine.
Hivi ufisadi wa Lowasa nani aliuibua na kuuhubiri majukwaani?
 
Hivi ufisadi wa Lowasa nani aliuibua na kuuhubiri majukwaani?

Unakaa nchi gani ndugu yangu wakati kila mahala watu wakisema fisadi maana yake ni Lowasa. Hadi bungeni, kina ndungai na wabunge wa ccm hadi wanasema Muhongo siyo fisadi bali lowasa. Nchi hii fisadi ni Lowasa tu.

Sasa tunataka haki itendeke. Serikali ya Magufuli imejibainisha kupambana na mafisadi, na kwa mujibu wa ccm na serikali yake, fisadi hapa Taznania ni Lowasa na kinachosemwa ni kwa nini alipewa kugombea uraisi. Hawa ni wawaklishi wa watu watunga sheria za nchi hii, hawajui hatua gani wahalifu wanapashwa kuchukuliwa.

Tunawakumbusha, vita ya ufisadi ambayo kwa lugha ny;ingine ni vita na Lowasa, haitaisha kwa kuzomea na kumsema kwa nini aligombea uraisi kitu ambacho nakiona ni muweweseko wa nguvu aliyonayo Lowasa hadi sasa kinachowanyima usingizi ccm. Vita hiyo pia isingekuwa imeisha kwa kumfungia ccm kwamab asiondoke ili wasimzomeee, hii labda ya kuwafungia ccm mafisadi ni hukumu ya ufisadi kwa mujibu wa katiba ya ccm.

Tunachosema hapa, vita dhidi ya ufisadi wa Lowasa, iishe kwa mjibu wa katiba ya nchi. Serikali impeleke mahakamani ili ahukumiwe kulingana na ufisadi wake. Na hapo mafisadi watakuwa wamekiwsha Tanzania. Na fedha atakazothibitika amefasidi, zirudi zikajenge madaraja ya wananchi na kuimarisha huduma za afya mahospitalini.

Ninawapa tahadhari ccm wasifikirie hatujui mkakati walioupanga wa kumzomea Lowasa hadi bunggeni kwamba ni fisadi wakati hawamchukulii hatua. Na kwa amani ya nchi tunataka wampeleke mahakamani au la wakome kuzomea kama mitoto isiyokuwa na malezi iliyokulia getoni.

Wasidhani watu hawajui ushenzi wanaoufanya. Wewe subiri.
 
Wwe nenda kwenye hoja. Kama ninyi ni serikali makini, mnajua Lowasa ni fisadi kwa nini hammfikishi mahakamani?

Vinginevyo unazidi kuonesha namna gani mnaweweseka na Lowasa hata kama hayuko ccm. Kuendelea kumuwewesekea mnathibitisha ni jinsi gani alivyojinamizi kwenu!.

La sivyo, mnajua ni mharifu, na ninyi mnaserikali, mpelekeni mahakamani akahukumiwe kama waharifu wengine.
Hoja yako si uwezo wa "Loh Hasa" kuisambaratisha Ccm ndani ya masaa 24..?
Ndo nimekuuliza kama alikuwa na uwezo huo sasa hiv si angekuwa Ikulu na asingepata ile shida kudhalilika kipind cha kampeni kama kule Chato..? Au hata kuonyesha uwezo wake wa kushindwa kutunza kumbukumbu kama ilivyotokea Morogoro..?
Unaposema sisi mimi na nani..?
 
Unakaa nchi gani ndugu yangu wakati kila mahala watu wakisema fisadi maana yake ni Lowasa. Hadi bungeni, kina ndungai na wabunge wa ccm hadi wanasema Muhongo siyo fisadi bali lowasa. Nchi hii fisadi ni Lowasa tu.

Sasa tunataka haki itendeke. Serikali ya Magufuli imejibainisha kupambana na mafisadi, na kwa mujibu wa ccm na serikali yake, fisadi hapa Taznania ni Lowasa na kinachosemwa ni kwa nini alipewa kugombea uraisi. Hawa ni wawaklishi wa watu watunga sheria za nchi hii, hawajui hatua gani wahalifu wanapashwa kuchukuliwa.

Tunawakumbusha, vita ya ufisadi ambayo kwa lugha ny;ingine ni vita na Lowasa, haitaisha kwa kuzomea na kumsema kwa nini aligombea uraisi kitu ambacho nakiona ni muweweseko wa nguvu aliyonayo Lowasa hadi sasa kinachowanyima usingizi ccm. Vita hiyo pia isingekuwa imeisha kwa kumfungia ccm kwamab asiondoke ili wasimzomeee, hii labda ya kuwafungia ccm mafisadi ni hukumu ya ufisadi kwa mujibu wa katiba ya ccm.

Tunachosema hapa, vita dhidi ya ufisadi wa Lowasa, iishe kwa mjibu wa katiba ya nchi. Serikali impeleke mahakamani ili ahukumiwe kulingana na ufisadi wake. Na hapo mafisadi watakuwa wamekiwsha Tanzania. Na fedha atakazothibitika amefasidi, zirudi zikajenge madaraja ya wananchi na kuimarisha huduma za afya mahospitalini.

Ninawapa tahadhari ccm wasifikirie hatujui mkakati walioupanga wa kumzomea Lowasa hadi bunggeni kwamba ni fisadi wakati hawamchukulii hatua. Na kwa amani ya nchi tunataka wampeleke mahakamani au la wakome kuzomea kama mitoto isiyokuwa na malezi iliyokulia getoni.

Wasidhani watu hawajui ushenzi wanaoufanya. Wewe subiri.

Kama ungefahamu kuwa jinai huwa haiishi ungesubiri mpaka afe ndipo utoe 'hukumu' kuwa hajachukuliwa hatua. Labda kama una hamu na ashki ya kutaka aanze kuchukuliwa hatua muda huu ili wengine wapate kusema anaonewa kwa kuwa amaejiunga upinzani. Wenye akili hawatatoa nafasi hiyo!
 
Hakuna binadamu anayeweza kuitwa kiongozi ambaye ataogopa kuchukua hatua stahiki dhidi ya wanaotishia ufanisi wake, eti anaogopa kuambiwa kaonea!. Ridiculous!. Hufai hat kuwa mzazi wa mtoto wako kama akili yako inaishia hapa!.

Kama ungefahamu kuwa jinai huwa haiishi ungesubiri mpaka afe ndipo utoe 'hukumu' kuwa hajachukuliwa hatua. Labda kama una hamu na ashki ya kutaka aanze kuchukuliwa hatua muda huu ili wengine wapate kusema anaonewa kwa kuwa amaejiunga upinzani. Wenye akili hawatatoa nafasi hiyo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom