Ndugu zangu tazameni hapa:-
Lowassa ni fisadi. Aliiba fedha kwa mfumo Richmond, serikali ilijua na iliogopa kumchukulia hatua. Amejiunga na upinzani hadi kugombea uraisi, serikali ya CCM inamwangalia na kuishia kuongelea uvunguni kwamba ni fisadi. Hakuna ajasiri wa kumfikisha mahakamani. Halafu bado serikali hii inajibainisha kwamba inatumikia wananchi kwa misingi ya haki na uzalendo.
Serikali imetumia majeshi yake yote kulinda maslahi ya CCM. Lakini haina uwezo wa kulinda maslahi ya taifa kwa kumfikisha Lowasa fisadi mbele ya sheria. Hapa ni dhahiri lowasa amewashinda Ccm na serikali yote ama serikali haina uwezo wala ujanja wa kupambana na ufisadi. adui wa tano wa maendeleo akifuatia nyuma ya Ccm yenyewe.
Lowassa amesema hadharani kwamba mwenye Richmond ni Jakaya Mrisho Kikwete, la ajabu Ccm na serikali yake, haina uwezo wa kushughulikana hili suala. Imeendelea kumfunika huyo aliyetajwa na kuzidi kulalamika juu ya ufisadi wa Lowasa lakini hakuna siku kafikishwa mahakamani ili aadhibiwe na mali ya taifa irudishwe kwa maslahi ya umma. Hiyo ni serikali.
Kumetokea ufisadi mwingi wa kutisha sana kama Escrow, Lugumi, EPA, na mingine mingi ambavyo washiriki wake ni wanachama wa ccm ama watumishi wa serikali ya ccm. Ccm haina ubavu wa kuongelea hayo wala haina mpango wa kuwachukulia hatua. Badala yake imefunika bunge lisitangazwe watu wasijue hayo mambo na hata mara nyingnine wabunge wamezuiliwa kuyaongelea hayo mambo. Lakini Ccm na serikali yake imekazana kusema Lowasa fisadi bila kumchukulia hatua. Serikali inalalamika badala ya kuchukua hatua. Ccm na serikali yake haina ubavu wa kumchukulia hatua Lowassa.
Leo wabunge wa ajabu kabisa wa CCM wanasema Uuzwaji wa nyumba usiongelewe kwa sababu na Lowassa alinunua. As if kununua nyumba za serikali ni kosa kuliko kuuza. Halafu lisisemwe kwa vile Lowassa alinunua nyumba. Lowassa kiboko ya Ccm na serikali yake kiasi kwamba hawana uwezo wa kugusa lolote alifanyalo wanaishia kulalamika.
Watanzania tunapata picha gani kuhusu CCM na serikali yake inayojiweka madarakani kwa hila huku haina uwezo wa kuongoza nchi?
Ama katika michango yetu, naomba tuongee kwa mifano halisi pale ambapo panathibitisha CCM kushindwa kuongoza nchi yetu kwa maslah ya taifa.
1. Ni kweil Lowassa ana nguvu kulilko CCM, Serikali yote na sheria zote kwamba hawana uweo wa kumfikisha mahakamani kwa ufisadi? Au wanaogopa vivuli vyao wenyewe? Kama siyo uoga, anayejibu aeleze ni kwa nini serikali na ccm yake wanamtaja fisadi wakati huo huo hawana uwezo wa kumfikisha kwenye sheria kama waharifu wengine.
2. CCM kupata kigugumizi kuzungumzia ufisadi na kuwachukulia hatua mafisadi waliodhahiri na kubaki kusema Lowasa lowasa. Wathibitishe kwamba Lowasa ni fisadi wa richmond, Escrow, Epa, Kagoda, Kiwira, Lugumi, Nida, N.K. Na kwa nini hafikishwi mahakamani?
Wenye uelewe waongee constructively huku mkisite relevant examples na nini kifanyike.
LOWASA AMEASHINDWA, CCM NA SERIKALI YAKE HAWATAKI KUONGELEA UFISADI MWINGINE LOWASSA NA BADO HAWANA UBAVU WA KUMSHITAKI.
HII NI SERIKALI AMA MAANDALIZI YA MAZISHI YA TAIFA LA TANZANIA?