Lowassa kavunja record, tumpe kura ya ndiyo

Lowassa kavunja record, tumpe kura ya ndiyo

Sifa moja kubwa zaidi ya Lowassa ni fisadi papa.

Sababu kuu ya matatizo ya Tanzania ni kuwa na viongozi aina ya Lowassa.

Kama tunataka matatizo ya Tanzania yaendelee kuwepo basi hatuna budi tumpe kura za ndiyo Lowassa ili awe Rais wa Tanzania.

Ni vizuri tumpe kura ya ndiyo Lowassa ili avunje record ya kuwa Rais wa Tanzania ambaye ni fisadi papa!

The choice is yours!

Hilo nalo neno, umenena. Mafisadi wa Escrow account, nyumba za serikali kuuziwa vimada; wizara ya ujenzi chini ya Dr.Makufuli imefisidi bilion 230; EPA, ufisadi ujenzi wa barabara zinazogeuka mahandaki na matuta ndani ya miezi 6 tu.

HILO NALO NENO!
 
Siyo siri. El amefanikiwa kubomowa na kuudhoofisha upinzani. Bado upinzani haujastuka tu.wamelewa pesa. Wasioamini tubiri oct 25.
 
Kama unaakili timamu trh 25 waza mambo machache kuhusu utawala wa ccm kuhusu dawa kukosekana hospitln kupatikana madukani, waza kuhusu elimi ya mcng, sec na vyuo ilivyo ya upendeleo, waza kuhusu shilingi yetu kwa miaka kumi hii, waza kuhusu tgt escrow, waza kuhusu epa waza kuhusu bei ya cement bati misumari na bei ya sembe kwa sasa na sukari utapa kwann mabadiliko ni lazima mwaka huu

Kuna jamaa mmoja akasema hivi mtu yeyote narudia tena yeyote nasema mtu yeyote ambae anawaza kuipigia kura ccm mwaka huu mtu yeyote msaada wa kwanza kumpa ni kumpima akili yake, kumba nimesema mtu yeyote.
 
Tatizo la maji, afya, elimu na maisha bora kwa kila mtanzania. Yatawezekana tukimchagua LOWASA
Nampa kura kubadili mfumo
 
Hahahahahah

Alikuwa mtendaji Mkuu wa Serikali kwa miaka miwili aliuondoa umasikini wa nani?

Mimi nnaona alituzidishia tu umasikini, akashtukiwa.

Magufuli. Amekuwa waziri kwa miaka 20 Ameondoa umaskini? Sasa ivi anajidai anawapenda watanzania wakati aliwambia wa kazi wa kigamboni, wasio kuwa na shlg 200 ya kupanda kivuko wapige mbizi?

Ninyi mshabikieni lakini sisi hatuta mchagua. Hatutaki kupiga mbizi ya maisha. Sumu haijaribiwi kwa kuionja.
 
Hahahahahah

Alikuwa mtendaji Mkuu wa Serikali kwa miaka miwili aliuondoa umasikini wa nani?

Mimi nnaona alituzidishia tu umasikini, akashtukiwa.

kumbe miaka 2 tu! siyo miaka zaidi ya 50.
ccm out!
 
Niliichukia CCM long time kutokana na kutokuwa na utendaji wa kutuvusha na uadilifu. Lakini wakati nikijaribu kutathmini watia nia wote CCM niliona ni Lowassa pekee alikuwa na merites za kuwasumbua ukawa katika uchaguzi huu kutokana na utendaji wake. The man always walk the talk, and not merely talking the walk.

Kimsingi nilivutiwa sana na utendaji wa Lowassa kwa kipindi kifupi alichofanya katika awamu ya nne kama waziri mkuu. Hata hivyo, baada ya kutia nia kupitia chama chake cha awali cha kijani, nisingeweza kumpa kura kutokana na kupoteza imani na chama hicho kitambo. Kwa bahati nzuri amanipa fursa, kwa kukikimbia chama chenye kelele nyingi bila vitendo na kuja huku aliko ambapo nasi tupo. Ni wakati wa kutimiza ndoto yangu, ya kumchagua kwa kuwa ninaamini atatuvusha. Amekuja tulipo kwa dhati kabisa, alipo nipo, alipo tupo.

"Nitaendesha serikali kwa speed ya ajabu", hii ni kauli yake ambayo sina mashaka nayo kabisa. Inanipa matumaini ya Tanzania mpya isiyo na uzembe na taarifa za mkaguzi mkuu zilizojaa wizi wa rasilimali zetu. Na hii ni tahadhari kwa wale wanaofanya kazi kwa mazoea, kwa uzembe bila malengo, siku zao zinahesabika. Lowassa ni mtendaji, na si mtu wa maneno.

Ukombozi mpya ni sasa. Jibu tayari tunalo, jibu ni Lowassa. Na kama huamini juu ya ubora wa kiongozi huyu, muda utakujibu, na utakuja kunishuhudia haya niyasemayo kama ndoto yangu hii itatimia.
 
Sifa moja kubwa zaidi ya Lowassa ni fisadi papa.

Sababu kuu ya matatizo ya Tanzania ni kuwa na viongozi aina ya Lowassa.

Kama tunataka matatizo ya Tanzania yaendelee kuwepo basi hatuna budi tumpe kura za ndiyo Lowassa ili awe Rais wa Tanzania.

Ni vizuri tumpe kura ya ndiyo Lowassa ili avunje record ya kuwa Rais wa Tanzania ambaye ni fisadi papa!

The choice is yours!
So ni bora tuwape ccm?
 
hahahahahah

alikuwa mtendaji mkuu wa serikali kwa miaka miwili aliuondoa umasikini wa nani?

Mimi nnaona alituzidishia tu umasikini, akashtukiwa.
acha wivu bibi hapa hatusemani vibarazani bali tina jenga hoja mujarab...
 
Lowassa ndio RAIS wetu... Mungu mpe KILA BARAKA, KILA NGUVU...

Ma CCM yatakufa kabla ya October 25... Sbb Mungu kaamua tutoke UTUMWANI... KWA IBILISI CCM...!!!

Lowassa, hadi nashindwa kuandika maneno gani ya KUKUPA UTAKATIFU...!!!

Chagua, Lowassa, Ukawa.
 
Back
Top Bottom