Lowassa kasusa tena kongamano la Tume ya Haki za Binadamu

Lowassa mbona hausauliki tu?Wewe mtu ukoje?Usiku tukilala tunakuota wewe,tukila tunakula wewe mbona unatitesa hivi.CCM OYEEE
 
Takribani wiki moja imepita tangu kuhitimisha kilele cha maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 17, viongozi mbalimbali wa kisiasa na dini walialikwa kuzungumzia masuala ya nchi. Ikiwamo maadili ya uongozi, kuoinga rushwa na demokrasia. Lowassa aligoma kuhudhuria huku ikibainika sababu kubwa ni kukwepa maudhui ya mkutano ule ulioratibiwa na taasisi ya Mwl.Nyerere, sababu nyingine iliyobainishwa ni yeye mwenyewe alijipima na kuona hatoshi kujadili maudhui ya kongamano.

Jana tarehe 21.10.2016 kulikuwa na kongamano kuntu lililoandaliwa na tume ya haki za binadamu, viongozi kadhaa walihudhuria na kutoa michango yao kuhusu masuala ya haki za binadamu,sharia,amani na rushwa kama kawaida aliingia mitini. Walihudhuria mawaziri wakuu wastaafu kama Warioba,Sumaye na wengine akiwamo raisi mstaafu Mzee Mwinyi.

Niseme tu kwa mwanasiasa aliye na dhamira katika siasa za ushindani makongamano kama yale si mahala pa kukosa,pale ni sahihi kuliko kulipa wahuni kushiriki maandamano na ukuta. Ila lazima nikubali tu kwa kiongozi aliye tofauti na asiyeamini mijadala ya rushwa,amani na utawala bora hukwepa kwa sababu ya dhamira inayomsuta.

Hata hivyo namtakia mema katika mkutano wa Chadema ambapo yeye ndiye anatarajiwa kuwa mzungumzaji mkuu katika ajenda ya maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wa mashinani ndani ya Chadema, natumaini vijana wake wa ulipo tupo,TeamEL na 4U movement wamejipanga 'kutafuna' mnofu.

Weekend njema.
Lowassa anaendelea kukukosha bila shaka
 
Amepiga sana ela za walipa kodi tutaendelea kuzungumzia kwa mambo ya kifisadi aliyo yafanya mbaka kwa wajukuu na vitukuu, tuta andika na vitabu yaliyotokea 2010 pale Chadema walipo mpokea Fisadi na kumpa nafasi agombee urais, ili wajukuu wetu walifahamu ili.
 
Kwani Dr Slaa aliposema mme amishia Choo ndani hamkumwelewa? Simlikua mna mtukana.Kazi mliyonayo ni kufukuza inzi mwaka 2020
 
Msiwashangae hao jamaa unajuwa EL aliwatenda mpaka wakalazimika kuiba kura kwa kutisha kuweka mambo sawa sasa mh wamepewa kazi ya kumpaka tope no matter what
Lowasa hata atajwe kila kukicha mpaka siku ya kufa kwake haiwezi ikafikia idadi ya jinsi alivyotamkwa mara nyingi zaidi na CHADEMAkwa ufisadi
 
Si mlishindwa kumfikisha kortini sasa kelelele za nini ?! Na hata leo hamuwezi kumpereka kwa kuhofia kufukua makaburi ya awamu ya 4
 
Watambue hawa walipo kwenye picha kama akili zako zinafanya kazi vizuri.
14671179_198403363926822_6619246951819591300_n.jpg
namuona rais wa mioyo ya watanzania
 
aliona hatoshi kama kile kijamaa kilichokimbia mkutano wa UN kikiogopa kiti moto cha Ban ki moon, tena kiti moto cha kiinglish juu ya chaguzi haramu za tanzania..
 
Takribani wiki moja imepita tangu kuhitimisha kilele cha maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 17, viongozi mbalimbali wa kisiasa na dini walialikwa kuzungumzia masuala ya nchi. Ikiwamo maadili ya uongozi, kuoinga rushwa na demokrasia. Lowassa aligoma kuhudhuria huku ikibainika sababu kubwa ni kukwepa maudhui ya mkutano ule ulioratibiwa na taasisi ya Mwl.Nyerere, sababu nyingine iliyobainishwa ni yeye mwenyewe alijipima na kuona hatoshi kujadili maudhui ya kongamano.

Jana tarehe 21.10.2016 kulikuwa na kongamano kuntu lililoandaliwa na tume ya haki za binadamu, viongozi kadhaa walihudhuria na kutoa michango yao kuhusu masuala ya haki za binadamu,sharia,amani na rushwa kama kawaida aliingia mitini. Walihudhuria mawaziri wakuu wastaafu kama Warioba,Sumaye na wengine akiwamo raisi mstaafu Mzee Mwinyi.

Niseme tu kwa mwanasiasa aliye na dhamira katika siasa za ushindani makongamano kama yale si mahala pa kukosa,pale ni sahihi kuliko kulipa wahuni kushiriki maandamano na ukuta. Ila lazima nikubali tu kwa kiongozi aliye tofauti na asiyeamini mijadala ya rushwa,amani na utawala bora hukwepa kwa sababu ya dhamira inayomsuta.

Hata hivyo namtakia mema katika mkutano wa Chadema ambapo yeye ndiye anatarajiwa kuwa mzungumzaji mkuu katika ajenda ya maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wa mashinani ndani ya Chadema, natumaini vijana wake wa ulipo tupo,TeamEL na 4U movement wamejipanga 'kutafuna' mnofu.

Weekend njema.
Mkuu,Kinana,Mkama na mzee makamba walihudhuria au?
 
Najaribu kufikiri kama EDWARD LOWASA angekuwa mlopokaji kama wao ingekuwaje
 
Back
Top Bottom