Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Takribani wiki moja imepita tangu kuhitimisha kilele cha maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 17, viongozi mbalimbali wa kisiasa na dini walialikwa kuzungumzia masuala ya nchi. Ikiwamo maadili ya uongozi, kuoinga rushwa na demokrasia. Lowassa aligoma kuhudhuria huku ikibainika sababu kubwa ni kukwepa maudhui ya mkutano ule ulioratibiwa na taasisi ya Mwl.Nyerere, sababu nyingine iliyobainishwa ni yeye mwenyewe alijipima na kuona hatoshi kujadili maudhui ya kongamano.
Jana tarehe 21.10.2016 kulikuwa na kongamano kuntu lililoandaliwa na tume ya haki za binadamu, viongozi kadhaa walihudhuria na kutoa michango yao kuhusu masuala ya haki za binadamu,sharia,amani na rushwa kama kawaida aliingia mitini. Walihudhuria mawaziri wakuu wastaafu kama Warioba,Sumaye na wengine akiwamo raisi mstaafu Mzee Mwinyi.
Niseme tu kwa mwanasiasa aliye na dhamira katika siasa za ushindani makongamano kama yale si mahala pa kukosa,pale ni sahihi kuliko kulipa wahuni kushiriki maandamano na ukuta. Ila lazima nikubali tu kwa kiongozi aliye tofauti na asiyeamini mijadala ya rushwa,amani na utawala bora hukwepa kwa sababu ya dhamira inayomsuta.
Hata hivyo namtakia mema katika mkutano wa Chadema ambapo yeye ndiye anatarajiwa kuwa mzungumzaji mkuu katika ajenda ya maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wa mashinani ndani ya Chadema, natumaini vijana wake wa ulipo tupo,TeamEL na 4U movement wamejipanga 'kutafuna' mnofu.
Weekend njema.