Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,095
- 43,305
Siupendi sana huu mchezo; kwani unaweza kukuaminisha kabisa kuwa utashinda. Unaona kabisa kwa macho yako kuwa karata nyekundu imefunikwa upande wa kushoto na unaona mtu mwingine anaapa kabisa iko pale na anaweka hela zake pale na wewe kwa kuamini "ulichokiona" na "ushawishi" wa mtu mwingine unaamua kuweka fedha zako pale. Unaulizwa una uhakika na wewe unaapa kabisa. Kweli ikifunuliwa unakiona kipo pale na wewe na yule mwingine wote mnalipwa! Unafurahia moyoni, unachekelea kwa sababu macho yako hayajakudanganya.
Raundi nyingine inafuatia; safari hii wewe peke yako una uhakika umeona karata iile na yule mwingine yeye anaweka pale ambapo una uhakika siko. Lakini kwa vile unaona kuwa una uhakika unaongeza na dau lake kusubiria mavuno. Karata zikifunuliwa unakuta umeliwa jumla!! Unataharuki na kuapa kuwa uliona kabisa. Unaamua kuondoka kwa kujikunyata. Umeweka fedha za ada ya watoto na pango la nyumba!
Baadaye unaambiwa kuwa wote wale walikuwa timu moja- yule mchezeshaji na yule shabiki aliyekuwa anakushawishi wewe - unaamua kurudi kwa hasira ili uwafungie kazi. Unakuta wameanua jamvi na wameondoka mahali. Unafikiria utamwambia nini mama wawili ukirudi nyumbani.
Ndivyo ambavyo tunaweza kuelezea jitihada kubwa ya kutikisa NEC na kumtikisa Kikwete. Kwa miaka karibu miwili kulikuwa na tishio la kutaka kutenganisha nafasi za Uenyekiti na ile ya Urais na hata siku chache zilizopita kulikuwa na madai ya kura za vijana ambao wanataka mabadiliko. Mwisho wa siku ni watu 2 tu walithubutu kumpigia kura za "Hapana" Mwenyekiti. Watu 2!
Kwa sababu hawakutegemea CCM kuwapiku kwa kubadilisha mtindo wa kupiga kura ambapo ingekuwa rahisi sana kuweza kujua kura za hapana zimetoka wapi. Hata uhesabuji kura - vyanzo vya ndani vinadokeza na hili litafumuka baadaye - ulifanywa ili kuhakikisha kujua ni kundi gani lilimpigia Rais kura za hapana.
Ni wazi mwisho wa kundi la Lowassa utaanzia leo; hasa tukisubiri uundwaji wa sekretariati mpya ya CCM ambayo itakipeleka chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa 2015. Mtu kaliwa. Lakini atarudi tena na fedha nyingine kujaribu kucheza mchezo ambao uko dhidi yake?