Mgagaa na Upwa
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 11,626
- 22,004
Unamaanisha nini? Kwamba Watanzania tukiamua kwa pamoja hatuwezi kuing'oa CCM madarakani?
Hapana ila nimeipenda tu hiyo
Unamaanisha nini? Kwamba Watanzania tukiamua kwa pamoja hatuwezi kuing'oa CCM madarakani?
Ni kweli kabisa, maisha ni magumu sana na mbaya zaidi yanazidi kuwa magumu..Kila kitu kiko juu, hakuna unafuu.
Ni wakati wetu sasa Watanzania kuitumia hii turufu kuchagua viongozi bora watakaotumia madaraka yao vyema.
#PamojaTutashinda
Ooh boy, come on
You were in same government.
You are also responsible
achana nayo fanya mambo mengne.
maisha magumu unakesha j.miii forum ??
maisha magumu soko la kina iphone. samsung na magar ya bei yamejazanaa foren??
mnataka maisha gan nyinyi ???
unadhan chadema itakuja kutatua matatizo yak ya familia.????
hahahah nifah beiby
Hahahaaaaa, mwanzo nilitaka nikujibu hovyo ila nimeona haina maana.
Kwani kutokushinda JF ndio maisha yatakua marahisi ilhali gharama za maisha zinapanda kila siku?
Jaribu kutumia akili basi kujenga hoja, sio unakuja na hoja nyepesi ambayo hata mtoto wa darasa la 3 atakushangaa.
Hayo ma iPhone n.k ni swali la kuuliza? Hujui kwamba tabaka kati ya matajiri na masikini linazidi kukua siku hadi siku?
Mwisho kabisa ndio nimekuona kilaza kabisa hata sikustahili kukujibu basi tu nimeamua kukupa darsa la bure.
Huwezi kuikwepa siasa katika maisha yako, leo hii kila kitu kiko juu kutokana na haohao wanasiasa wanaosaini mikataba mibovu huku wakiweka maslahi yao mbele zaidi ya taifa.
Leo hii umeme uko juu na kila kitu kimepanda....jaribu kujiongeza.
Hata kama ufanye kazi zaidi ya punda, mchana na usiku huku gharama za maisha ziko juu sahau kupata mafanikio kwa wakati.
Hivi wakati lowasa yupo PM kwenye senate walikua hawafuati ushauri wake?
Mkuu alikuwa anapata amri kutoka mamlaka ya juu nini cha kufanya.Ooh boy, come on
You were in same government.
You are also responsible
Ni kweli ameharibu uchumi anaepinga ni kula kulala.
Wenzake waadilifu hawatekelezi amri zisizoelewekaMkuu alikuwa anapata amri kutoka mamlaka ya juu nini cha kufanya.
Hawakufuata ushauri wake, ukitaka kuthibitishiwa hilo kuhusu RICHMOND baada ya kuona magumashi aliita kikao cha makatibu wajadili na kuvunja mkataba lakini likatoka AGIZO KUTOKA MAMLAKA YA JUU kuruhusu mchakato uendelee.
Mwaka 2008 umeme uniti 72 tulipata kwa tsh.10,000/- lakini mwaka 2015 umeme unit 64 unazipata kwa tsh.30,000/-.
Kwa nini gharama za uzalishaji bidhaa, huduma zisipande?
Sukari, Sabuni, Ndala, Biki, Daftari, Ream Paper, Mafuta ya kula, Ngano, Kiberiti, Pipi, Biskuti vyote vimepanda bei hata uongezewe mshahara hakuna unafuu.
Tumegundua gesi ilipaswa ipatikane kwa bei nafuu ili kusaidia kupunguza matumizi ya mkaa na kuni na upatikanaji wa umeme lakini ni kucheka cheka tu.
Kama mwadilifu yupi mkuu...si unaona bandari isiyo na tija inajengwa Bagamoyo wakati ya Dar ipo mita chache kutoka hapo...hiyo ni amri ya mkubwa kwa mwadilifu Mwakyembe kupitia baraza la mawaziri ambalo halikupinga. Lowassa nani apinge mamlaka ya juuWenzake waadilifu hawatekelezi amri zisizoeleweka
Suala la utendaji wa Lowassa halipimiki kwa muda ambao Kikwete amekuwa madarakani. Lowassa anahistoria ndefu saana. Anaweza kutuambia ana mali kiasi gani na amezipataje? Anaweza kutuambia ule msafara kwa kura za maoni mpaka kuchukua fomu ni nani alimfadhili? Tunafanya kosa hapa. Alichofanya yule bwana ni kutafuta nguo za khaki na kuvaa juu ya suruali nyeusi na shati la kijani. Hali ya hewa ikibadilika na jua kuzidi tutamuona akivua nguo za khaki.Kama mwadilifu yupi mkuu...si unaona bandari isiyo na tija inajengwa Bagamoyo wakati ya Dar ipo mita chache kutoka hapo...hiyo ni amri ya mkubwa kwa mwadilifu Mwakyembe kupitia baraza la mawaziri ambalo halikupinga. Lowassa nani apinge mamlaka ya juu
Kuna jamaa yangu hampendi Lowasa kwa sababu alisababisha picha na video ya harusi yake ziharibike.
Kipindi Lowasa PM alipita halmashauri moja akatikisa mbaya, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri aliachwa hana uhakika wa ajira yake.
Sasa sehemu ya pili kwenda ilikuwa kwa mshkaj ambaye yeye alikuwa District Treasury, alikaliwa kooni wiki nzima kuweka mambo sawa hadi siku moja kabla ya harusi. Alikuwa anakesha kuziba mapengo na viporo, siku ya harusi alikuwa na usingizi mbaya
Tusubiri tuone...acha tumpe benefit of the doubtSuala la utendaji wa Lowassa halipimiki kwa muda ambao Kikwete amekuwa madarakani. Lowassa anahistoria ndefu saana. Anaweza kutuambia ana mali kiasi gani na amezipataje? Anaweza kutuambia ule msafara kwa kura za maoni mpaka kuchukua fomu ni nani alimfadhili? Tunafanya kosa hapa. Alichofanya yule bwana ni kutafuta nguo za khaki na kuvaa juu ya suruali nyeusi na shati la kijani. Hali ya hewa ikibadilika na jua kuzidi tutamuona akivua nguo za khaki.