CASTRO PEMBA
Member
- Jul 29, 2015
- 85
- 50
Katika mkutano wa kihistoria, mh" rais mtarajiwa amesema JK ameharibu uchumi, watu weng wamekua maskini, bidhaa juu, hoi
Akizungumza na wafuasi wa Chadema na UKAWA katika ofisi za Chadema mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho amesema, "rafiki yangu Jakaya Kikwete ameuharibu uchumi wa nchi yetu," ameongeza: "Wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani kilo ya sukari ilikuwa Sh. 600 leo ni Sh. 2,300. Mchele ulikuwa Sh. 550 leo ni Sh. 2,300. Sembe ilikuwa Sh. 250 leo ni Sh. 1,200."
Aidha Lowassa amesema, katika kipindi cha utawala wa Rais Kikwete ndipo Tembo na kila aina ya wanyama wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya Tanzania.
"Katika utawala wa Rais Kikwete, Tembo wameuawa kuliko kipindi chochote katika historia duniani kote. "Kila aina ya mnyama ameuawa kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi yetu.
Nitaijenga serikali yenye uchumi kwa speed (kasi), ambaye hawezi akae pembeni," amesema Lowassa.
Chanzo: MwanaHalisi Online