Lowassa: Hatutakubali Matokeo ikiwa...

Lowassa: Hatutakubali Matokeo ikiwa...

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
57,950
Reaction score
134,021
Lowassa mgombea urais CHADEMA amepiga mkwara kuwa CHADEMA hatutakubali matokeo ya Uchaguzi,ikiwa hakutakuwa na mazingira ya uchaguzi huru na haki.

Kamanda Lowasa akiwa anajiamini kushinda amesema kuwa kama uchaguzi huru na haki hawana budi kukubali matokeo.Bali kama kuna goli la mkono hawawezi kukubali.CCM hakuna mteremko mwaka huu.

Chanzo: Mwananchi
 
Mh.Lowasa mgombea urais Chadema amepiga mkwara kuwa Chadema hatutakubali matokeo ya Uchaguzi,ikiwa hakutakuwa na mazingira ya uchaguzi huru na haki.Kamanda Lowasa akiwa anajiamini kushinda amesema kuwa kama uchaguzi huru na haki hawana budi kukubali matokeo.Bali kama kuna goli la mkono hawawezi kukubali...CCM hakuna mteremko mwaka huu.Source:Mwananchi
Wasikusikie Chato.
 
Ukiona ivi ujue kashanusa harufu ya goli la mkono. Simmeskia huko Mwanza kilichojiri kati ya mkuu wa mkoa na wasukuma bodaboda.
 
Tume mjiandae ujanjaujanja utatufikisha pabaya mtanzania anaweza kila kitu
 
Kwan atakuwa wa kwanza kukataa. Hata Dr Slaa alikataa na akasema hamtambui rais lakin nchi iliendelea. Kwa EL hizo no dalili mbaya kama za mgonjwa anaejiona hali mbaya sasa anaanza kuniuliza hivi ntakufa. Yy kakubali kuingia mchezon akubali kushindwa pia.
 
Kwa Tume Hii ya Uchaguzi Jinsi wanavyoenda...Wabavyotaka Matokeo yakubaliwe Kwa Njia yoyote Ile..Machafuko Makubwa Hayaepukiki.

CCM Wasifanye UjanjaUjanja Vinginevyo..time will tell.

CCM Wakijidanganya Kupora Ushindi basi UKAWA Watanzania tupo Nyuma yetu. Tumeichoka CCM.
 
Kwani lini wapinzani walishawahi kukubali matokeo? Mjiandae mapema kisaikolojia.. Na mkikaidi mtapigwa tu na mm nasema mmpigwe tu maana hamna namna sasa.
 
msipofanya uchaguzi wa haki mnategemea nini?? yani mpite kiujanjaujanja tu, chezeni kote ila msichezee kura zetu pimbi nyie
 
Copy and paste👇👇

Viongozi wakuu wa umoja wa katiba ya wananachi UKAWA wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Mh FREMAN MBOWE pamoja na makamu mwenyekiti wa CHADEMA Profesa SAFARI na kaimu mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF ambaye pia ni mbunge wa bunge la Africa mashariki Mh TWALHA TASLIMA leo jioni wamehudhuria Baraza la kuu la idd lililoamndaliwa na Taasisi za kiislam Tanzania shughuli iliyofanyika katika hotel ya LAMADA Jijini Dar es salaam.

Katika shughuli hiyo ambayo iliambatana na dua mbalimbali pamoja na hotuba za viongozi mbalimbali pia walialikwa wagombea urais wa vyama vyote Tanzania lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kufika huku mgombea wa UKAWA akiwakilishwa na Mh FREMAN MBOWE.
Mh mbowe alipata nafasi ya kutoa Hotuba fupi ambayo iliwagusa mamia ya waislam ambao walikuwa katika shughuli hiyo na hapa nimekunukulia baadhi ya mambo ambayo mbowe aliyazungumza na kushtua wengi


1-Nashukuru sana kwa ukaribisho wa shughuli hi,mgombea wetu ndugu EDWARD LOWASA alitamani kuwa nasi jioni hii lakini kutokana na ratiba ya kampeni kubana imebidi aunganishe kwenda kwenye kampeni za kesho huko manyara--MH MBOWE

2-Swala la mashekh ambao wapo jela bila hukumu yoyote,tulisema siku ya ufunguzi wa kampeni na tunaendelea kusema kuwa tumewaagiza wanasheria wa chama chetu kufwatilia kwa makini na kuona nini hasa kimetokea kwao kama kuna mahali kunahitajika msaada wa kisheria tupo tayari kulishuhulikia hilo kwani sisi lengo letu ni kurudisha umoja na mshikamano Tanzania. --MH MBOWE

3-Zimebaki siku takribani 30 sasa kabla ya watanzania kufanya maamuzi halisi,ni muda wa maamuzi ndugu watanzania. --MH MBOWE

4-TANESCO imefilisika na watanzania wengi hawajui hili,sasa shirika la umeme halina hata sent na wameamua kufanya mgao wa kimya kimya lakini ukweli ni kwamba huu mgao ni mkubwa sana huko tuendako kwa sababu hawana hela na wanaficha ukweli,kuna mgao mkali sana sasa wa kimya kimya na utaendelea kuwa mkali kadiri siku zinavyokwenda. --MH MBOWE

5-Kuna wizi mkubwa sana wa mafuta Tanzania na kuna baadhi ya watu wakubwa wanauratibu wizi huo,Tanzania ina akiba ya mafuta hadi mwezi wa 11 lakini serikali imetoa hati ya kuingiza mafuta nchini ambapo baadhi ya wahusika ni familia ya Rais KIKWETE. --MH MBOWE

6-Serikali yetu ya awamu ya tano sio serikali ya visasi kama inavyodhaniwa,ila ni serikali ya kuwarudisha watanzania pamoja kwa maridhiano,na maelewano,ila kuna watu itabidi washughulikiwe kwa mijibu wa sheria kutokana na kuligharimu taifa hao tutafanya hivyo. --MH MBOWE

7-Tume ya uchaguzi ya miezi miwili iliyopita sio tume ya sasa,mwenyekiti yupo ila watendaji wengi wameondolewa bila sababu za msingi. --MH MBOWE

8-Mtendaji mmoja mkuu wa tume juzi tumepata taarifa kuwa ameondolewa na kupelekwa kusikojulikana na amerudhishwa na kutakiwa kukabidhi ofisi mara moja. --MH MBOWE

9-Tume ya sasa inaongozwa na wanajeshi na usalama wa taifa,mimi mbowe ndio nasema kama kuna mtu anabisha waje wanikamate leo,hatuwezi kuvumiliana kiasi hiki ni wakati wa kuwekana wazi ili watanzania wafanye jambo wanalolitaka. --MH MBOWE

10-Nasema hivi hatutakubai hujuma hizi ambazo zinaendelea sasa tutasema hadi mwisho. --MH MBOWE

11-Mwisho kabisa nasema hivi ni wajibu wetu kutafuta kura,kupiga kura na kulinda kura hivyo ndugu zangu waislam nawaomba tushirikiane katika hili,ASANTENI KWA KUNISIKILIZA--MH MBOWE
 
This is silly!.. alisema ni lini Uchaguzi haujawahi kuwa Huru na wa haki? Mbona hatujawahi kumsikia akiungana na wapinzani walipopiga kelele ya kukosekana uhuru na haki kwenye chaguzi mbalimbali; au anafikiri tumesahau yaliyotaka kutokea Arumeru Mashariki?
 
Ukiona ivi ujue kashanusa harufu ya goli la mkono. Simmeskia huko Mwanza kilichojiri kati ya mkuu wa mkoa na wasukuma bodaboda.

Mimi nilikuwepo miongoni mwa hao Bodaboda ,acheni kuzusha MAMBO ,mkuu wa mkoa haku udhuria Mkutano huu alipata dharura ,na mkutano huo haiku husiana kabisa na masuala ya uchaguzi.
Ulifanyika jengo la PPF ukiongozwa na mkuu wa wilaya pamoja na Meneja wa mfuko wa jamii wa LPF,USHAWISHI ULIKUWA WAJIUNGE NA HUO MFUKO,AMBAPO WENGI WALISEMA TAYARI WAMESHA JIUNGA NA NSSSF.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Kwa Tume Hii ya Uchaguzi Jinsi wanavyoenda...Wabavyotaka Matokeo yakubaliwe Kwa Njia yoyote Ile..Machafuko Makubwa Hayaepukiki.

CCM Wasifanye UjanjaUjanja Vinginevyo..time will tell.

CCM Wakijidanganya Kupora Ushindi basi UKAWA Watanzania tupo Nyuma yetu. Tumeichoka CCM.

😛😛😛😛
 
Back
Top Bottom