Lowassa hakuonewa; alichelewa kujiuzulu! - | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa hakuonewa; alichelewa kujiuzulu! -

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 4, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  • [FONT=&quot]Alipewa nafasi ya kujitetea, akatumia kujiuzulu[/FONT]
  • [FONT=&quot]Angejiuzulu kabla ya Kamati Teule kuundwa, angekuwa shujaa[/FONT]
  • [FONT=&quot]Wanaoamini kaonewa hawajui "natural justice"!
   [/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Kuna baadhi ya watu ambao wanaamini mioyoni mwao kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa alionewa na Kamati Teule ya Bunge na kuwa alilazimishwa kujiuzulu kutokana na kutotendewa haki na Kamati hiyo iliyoongozwa na Dr. Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Kyela. Watu wenye imani hiyo wanaamini kabisa kuwa Lowassa hakutendewa haki na hivyo wanafanya kila jitihada ya kuhakikisha kuwa Lowassa anasafishwa na hatimaye kujengwa tena ili kuweka rekodi iwe sahihi. [/FONT]

  [FONT=&quot]Katika makala hii ambayo nimeitengeneza kwa mtindo wa maswali na majibu nina kusudio la kuonesha kuwa Bw. Lowassa hakuonewa na mtu yeyote, alitakiwa kujiuzulu hata kabla ya Kamati Teule kuundwa na kuwa mjadala way eye kuonewa na chombo chochote ni mjadala unaotokana na mtazamo finyu, wenye ushahidi dhaifu, na kwa kipimo chochote unajaribu kutengeneza kitu ambacho hakipo. Ni makusudio yangu kuonesha kuwa Bw. Lowassa alistahili kujiuzulu mapema zaidi na hata pale alipochelewa alitakiwa kukubali adhabu aliyojipa yeye mwenyewe kutokana na kutokuwajibika kwake, uzembe wa ofisi yake, na kutokuonesha usimamizi unaomstahili Waziri Mkuu katika jambo nyeti kama la nishati. [/FONT]

  [FONT=&quot]Lengo kubwa ni hatimaye kulazimisha kwa nguvu za hoja kufunga mjadala huu baada ya kuzipima hoja zote [/FONT][FONT=&quot]kama[/FONT][FONT=&quot] zilivyo. Fuatana nami ukiwa na fikra huru ili uweze kuona kuwa nafasi aliyonayo sasa hivi Bw. Lowassa ndiyo nafasi ya juu kabisa ambayo anastahili kuishika katika Jamhuri yetu, ceteris paribus. [/FONT]
   

  Attached Files:

 2. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Du! Kama tungekuwa na rasli mali zisizokuwa na kazi... ingebidi tuchunguze

  "Kuna nini zaidi kati ya Mzee MwanaKijiji na Mh. Lowassa"

  Maana post zinazomuhusu Mh. Lowassa toka kwa Mwanakijiji ni nyingi sana, kuna nini? si tayari sio waziri mkuu? sasa mwatafuta nini?
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kuna watu wanaamini alionewa; nimeamua kufunga mjadala ili EL asiwe mtu wa kutufanya tuumize vichwa vyetu.. kila wakati "Lowassa, Lowassa, Lowassa".. Hivyo, makala hii inakusudia kulazimisha kwa nguvu za hoja kuufunga mjadala wa Lowassa kuonewa au hakutendewa haki au sijui nini!
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  In short ni kwamba Lowassa hakutegemea yaliyotokea kuwa yangetokea. Alifanya maamuzi bila kujali anavunja au anafuata sheria probably kwa sababu ndio utaratibu wa viongozi wetu. By the way who's gonna ask??????? Muungwana? His mate? Hamjasikia kwamba hawakuktana barabarani? Tumetoka naye mbali bwana. Alikuja kugundua or else kugundulishwa when it was too late!!!!!! Jazba, kutapatapa, na egoism ndiyo vilimfanya ajiuzulu na si eti kwamba he loves Tanzania or watanzania that much.

  Huyu jamaa hana hata chembe ya usafi na haiwezekani kusafishika. Na kama kuna kiongozi atajaribu kumsafisha direct na kiuwazi basi na yeye political future yake itakuwa matatani.

  By the way on what recordz kuzishinda za kina Mrema, Sokoine na hata Magufuli zinazotufanya watanzania tusimsahau huyu mtu???????
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ndio sababu ya kuandika hii makala. Lowassa is history. As far as I can tell, I don't see any possibility (even remotely) of Lowassa being a force in the future. He had his chance to clear his mess and has chosen not to.
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nadhani hata yeye analijua hili. Otherwise kwa ile calibre yake katka kipindi hiki cha karibu mwaka na nusu angekuwa tayari amesha-stand out from the crowd mwenyewe na si kutumia vikaragosi. I guess the first six months or even a yr alikuwa confused and hallucinated and therefore could blv ths myth of him coming back but as of now sidhani!!!!!!!
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,583
  Trophy Points: 280
  Wakati nasubiri kuisoma makala yako nikiwa nimetulia. pamoja na kuhusika kwake kote, principle za natura justice is 'no one is condemned unheard'. Lawassa walimcondem bila kupewa nafasi ya kusikilizwa. Mzee, Mwanakijiji, Mwakiembe ni mwalimu wangu, ukimwamini sana, utapotea. Nikisha kusoma vizuri nitakujibu vizuri.
  Siko kwenye kundi la kumtetea Lowasa na ufisadi wake, but was serious, firm na practical, jamaa ana uwezo mara 10 ya JK.
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Man, the dude is not gonna give up the fight so easily, he seems not to be a quiter. Despite the fact that his political life is in tatters, do not under estimate him. He has been written off before but he bounced back. He still commands a huge number of Lowassites in the party, military and the government, do not just write him of.
  Bado kuna mazingira mazuri sana ya yeye kuweza kurudi, kuna rutuba nyingi sana ni kuangalia karata zake tu. Akicheza mbili tu unaweza kushangaa kizunguzungu kitakachotokea.
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Heshima mbele mkuu MM,hongera kwa kazi nyingine nzuri yenye uchambuzi uliokwenda shule, huyu Lowassa hajaonewa bali anapendelewa na kulindwa; katika nchi yeyote ile yenye ustaarabu huyu bwana asingekuwa anaumiza vichwa vya watu mpaka sasa angekuwa amekwishafikishwa mbele ya vyombo vya sheria kwa kutumia madaraka vibaya yaliyosababisha uchumi wa nchi kuhujumiwa!! Kikwete anamlinda kwa sasa lakini akumbuke kuwa kwa yeyote yule atakayekuja kutawala hapo baadae kesi hii inaweza kuja kufufuliwa na huyu bwana kufungwa;sheria za nchi yetu zinaruhusu hivyo inawezekana hawa vilaza hawajui hilo!!
   
 10. S

  Samwel JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 25, 2007
  Messages: 224
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu,
  Je na yule mwenye domo kubwa la maneno.
  Kila saa Mwakyembe, mwakyembe,mwakyembe.Hapo hatumizi vichwa?
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  I do not believe that Lowassa is not a quitter because he was given a chance to present his side of the story in the presence of a full BUNGE house but chose to throw in the towel instead!! He was heard as the law of natural justice dictates but in doing so he never defended himself against the allegations levelled against him in the report.!! Unfortunately, his handlers are convincing him that he should do now what he was supposed to do then as a way of cleansing his political dung!! It is a pity that he is being ill advised and he is swallowing the advice wholly bait, hook and sinker!! He is a nut.
   
 12. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  hata kama angepewa kusikilizwa angesema kitugani? Na wale mnaosema EL anauwezo mara 10 ya JK, nakubali, anauwezo wakuiba dola mil 100 kwa siku zaidi ya JK, kwani EL ana guts sana. Ana ubabe na kufukuza watu kazi bila kuwapa nafasi za kusikilizwa, kisa wakishindwa kutaja takwim katika miadhara aliyotembelea.
   
 13. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hata mimi naona Hakuonewa alitakiwa kujiuzulu mapema tu.
   
 14. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Alitakiwa awe Segerea by now!

  Respect.


  FMEs!
   
 15. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,674
  Likes Received: 21,903
  Trophy Points: 280
  Kamanda, nani wa kumpeleka? maana Segerea mtu haendi mwenyewe mpaka apelekwe ati!
   
 16. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Kuna baadhi ya watu wapo kuharibu na kuvunja hizi sheria kama hii ya manunuzi ya umma kwa makusudi, EL akiwa mmoja wao.

  Halafu sheria ya dharura nayo ipo na haitumiki inavyotakiwa na EL alidhani kwamba dharura ni kwamba kwa kuwa yeye ni waziri mkuu basi ataidhinisha tu kwa kuwa raisi hatosema kitu kutokana na kwamba wao ni marafiki.

  Lakini behind the scenes inaonekana walibishana sana na mkuu akamwambia kuwa sheria ni sheria na ilivunjwa kwa hio kamati lazima iundwe.

  Ikitokea mambo kama haya ya kuvunja sheria hata kama ni mimi ni rafiki yako na nafahamu kuwa wewe ni rafiki yangu ni lazima ntakutema tu.
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Imefika sehemu sasa tuachane na hii mijadala isiyoisha ya kudeal na watu wale wale as if kama watakuwa hawapo basi na Tanzania nayo itakwishilia mbali. Tunao wakati mgumu sana wa kuandaa viongozi wa baadae wa Taifa letu. Zile asasi ambazo huko nyuma zilitumika kuwaandaa viongozi sasa hivi haziaminiki kutumika kama ilivyokuwa siku za nyuma.
  Kitu kimoja nacho kifurahia mimi binafsi ni hii clash of ideas ambayo Kina Lowassa na mbinu zao mbalimbali za kubaki kwenye siasa wamezileta. Tunaona tulipo kila muhimili unataka nafasi yake ionekane na kuheshimiwa.Na kama wahenga wanavyosema, maji yakimwagika hayazoleki, mbele ya safari tutaona streamline ya kila mtu anatakiwa kufanya nini na suala la intergrity halitachukuliwa kwa masihala kama lilivyo sasa.Bila kujua naona kama hizi debate zimekuwa kama blessings in disguise!!
   
 18. mabina

  mabina JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
   
 19. GreatConqueror

  GreatConqueror Member

  #19
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ile haikuwa 'mahakama' bali chombo cha 'uchunguzi' kwa hiyo walichokuwa wanatafuta ni ukweli, na walipopata ushahidi mzito dhidi ya Lowassa hakukuwa na umuhimu sana kumhoji so wakamshauri accordingly... Kuyumba kwa ujasiri wa Lowassa issue ya Richmond-leaves a lot to be desired!! Lazima kuna kilichomfanya kuwa extremely lenient kwa Richmond (tofauti na Lowassa wa City Water). That may be all we need to know!
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  I wish viongozi wetu wangekuwa na uthubutu wa namna hii... JK original (Julius Kambarage) aliweza hili

  Big up FMES!!!
   
Loading...