Lowassa alikuwa campaign manager wa rais wa awamu ya nne, alikuwa na influence kubwa sana. Nadhani hiyo ni sababu hata JK alikuwa anatumia ule mtindo wa "handle with care", kwa sababu kwa kumgusa mtu ambaye ametumia maisha yake yote katika kujenga networks za watu, unakuwa umekitingisha chama. JK alikuwa leo anakula huku, kesho anakula kule. Leo anakwenda Butiama na kucheka na Mama Maria Nyerere, kesho anakaa na wafanyabiashara wapigaji watoto wa mjini. Hivyo pamoja kuwa alikuwa ni rafiki na Lowassa alikuwa anahakikisha hawaudhi wazee wa Nyerere (ambao ukweli ni kwamba alishawaudhi siku nyingi).
Hivyo Lowassa kuondoka mwenyewe ni sawa na kuondolewa kwa sababu aliyemuwekea zengwe mpaka akaondoka, alihakikisha kuondoka kwake hakuwezi kuigharimu CCM kiasi cha kushindwa uchaguzi mkuu. Lowassa alianza kutengeneza mazingira ya kuwa mtu fulani mkubwa baadae tangu enzi za ujana wake, tangu enzi za awamu ya kwanza alishaanza kuwafuata watu kwa nia ya kuwataka wawe upande wake. Hivyo kumuondoa kwa kumfukuza isingewezekana. Ilibidi utafutwe wakati muafaka wa kumvunja kabisa moyo, kwa kutegemea mikakati ya kisiasa ili hasira zake mwenyewe ziwe ndio kiongozi wa maamuzi yake.