Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,443
- 40,537
Kuna Propaganda zinazoenezwa na CCM na humu JF na "List of 46" wako bize kwa hilo, kwamba Lowassa alijiunga na CHADEMA baada ya kukataliwa na CCM kutokana na "Ufisadi" wake jambo ambalo si la kweli kwa asilimia mia moja. Lowassa alijiunga na CHADEMA baada ya kukataa kuwa Kondoo wa kafara kama walivyofanya kina John Malecela na Gharib Bilal walipoonewa na CCM.
Malecela na Bilal walikubali kukaa kimya hata pale taratibu za chama chao zilipopindwa ili kuwazuia kugombea Urais,lakini Lowassa alijua kuwa "Once beaten twice shy" ni heri kufa umesimama unapigania haki yako kuliko kufa umepiga magoti kwa kusubiria makombo!! Kama kuna mtu ataleta ushahidi hata wa kimazingira kwamba Lowassa aliwahi kukataliwa na CCM kutokana na "Ufisadi" wake naweza kubadili msimamo wangu kuhusu uhalali wa CHADEMA kumpokea Lowassa na kumfanya awe mgombea wake Urais!!