Elections 2015 Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya II " Hana Jipya"

Lowassa very soon atakua 'old news'
hata huko CCM hawamjadili tena
now wanamjadili Jaji Ramadhani na Makongoro na wengine
why Mwanakijiji unajaribu kumfanya aendelee kuwa 'relevant'?
au ni promo ya aina nyingine?
alichofanya nwanakijiji ni elimu ya uzalendo.. na kama usipoelewa andishi hili utakuwa na matatizo hilo la promo sidhani maana naona kammaliza zaidi.
Pasco ndugu yangu acha kumsapoti huyu mmasai mwenzangu.. waachie kina ocampo four ambao wanapata vihela vya maandazi
Ahsanta.
 
Last edited by a moderator:
MM we ni noma nmekuvulia kofia, wapinzani tumieni hoja za mwanakijiji kuwapiga ccm na mziweke ktk ushaidi mfano tembeeni na speech ya jk kwenye mikutano na muwasikilizishe watanzania na mfanye comparison na kinachosemwa na hawa wagombea....hakiamungu kabla ya misa ya pili ukawa wanachukua nchi
 
lowassa.jpg


Na. M. M. Mwanakijiji

Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani Edward N. Lowassa hafai kupewa nafasi ya Urais.

Watanzania hawajachoka bado? Bado hawajakoma?
Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

Sisi wengine sasa tumeanza kuchoshwa na hizi kelele za kila siku siku fulani hafai!, kusema tuu fulani hafai, hakuwasaidii Watanzania, waliochoshwa na umasikini huu uliotopea, kama ungeshauri nani anafaa, utakuwa unatusaidia zaidi kuli kuishia tuu kuse,ma fulani hafai.

Tangu lini CCM imetuteulia kiongozi anayefaa?!, Rais Jayaya Kikwete nie rais anayemaliza muda wake, jee amefaa nini?!, miaka kumi sini hii sasa anamaliza?!. Kama Lowassa kwako hafai, it is fine, kwa sisi tunaomuona anafaa, tutaendelea kusimama nae, vingine kama hakuna anatefaa z`aidi ya huyu ambaye hafai, then ni safadhali huyu huyu asiyefaa, kwa sababu japo hafai, lakini ndiye aliyepo!, kuliko hao wanaofaa ambao hawapo!. Ukimuondoa Nyerere, Mwimyi alifaa?!, Jee Mkapa ndio alifaa?!, na Kikwete jee amefaa?!.

Kama huna jina la anayefaa, then huyuhuyu asiyafaa ndie rais wetu 2015 kupitia ndani ya CCM au nje ya CCM.

Kuhusu kufaa kwa Lowassa. mimi niliwahi kusema hivi.

[h=3]Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa..[/h]Nilisema hivi

Wanabodi,

Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Dakika 45 cha ITV, kwanza nimemkubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005, Tanzania tusingefikia hapa tulipofikishwa sasa na utawala wa JK!, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai mwenyewe kuwa yuko fit, japo he looks sick!), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, then matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali!..., mkatae!.

Hizi ni baadhi tuu ya sababu, kwanini CCM itashinda tena kwa ushindi wa kishindo kikuu, endapo and only if itamsimamisha Edward Lowassa!.

1. Uwezo wa Kusema, Kupanga, Kutenda na Kusimamia!.
Viongozi karibu wote waliopo CCM, wana uwezo mkubwa sana kesema!, tutafanya hiki, tutafanya kile!, ni maneno tuu! na pia wana uwezo mkubwa wa kupanga mipango kwa maneno tuu na sii matendo, au usimamizi, mfano mipanga kamambe kama (Mkukuta, Mkuza, Mkumbita, Mkurabita, na sasa Dira 2025)!. Mipango yote hii ni mizuri kwa maneno tuu, lakini wengi hawana uwezo wa kutenda na kusimamia utekelezaji!. Mipango mingi iliyopangwa, inaishia kwenye maneno na mabuku na makabrasha tuu, lakini utekelezaji kwa vitendo ni sifuri!. Kwa Edward Lowassa, yeye sio msemaji sana, bali ni mtendaji kweli!, yeye sio mtu wa maneno mingi!, ni mtu wa vitendo virefu!, he is an action oriented man!. Mfano hai ni pale alipokutana na madudu ya City Waters!, aliwafurusha there and then!. Hata madudu ya Richmond, alitaka kuwafurusha na kutaifisha kila kitu ila alishindwa!, kutokana na "mwenye mitambo!".

Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Ujinga, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile misingi minne tulisahau capital kwa kudai "pesa sii msingi!".

Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo kidogo la utekelezaji wa siasa safi ya Ujamaa na Kujitegemea na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, ile miaka ya 60, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa kuliko sisi, with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Ujinga ni adui, lakini we never invested on Elimu because we had no capital!. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana Edwin Mtei na IMF, WB etc matokeo sote tunayajua!.

Lowassa na timu yake ya Boys II Men, walipoingia tuu madarakani, EL akafanya study tour ya nchi tulizoanza nao wakati wa uhuru!, kwanini wao wamefanikiwa, wako mbali na sisi wametuacha nyuma sana!, akagundua wali invest kwenye elimu!. Akarudi nyumbani, akahamasisha kila kata iwe na shule ya sekondari ili kila Mtanzania apate kwanza elimu, mengine yote, yatafuatia!. Baada ya kujengwa shule, zilikuwa zipatiwe vifaa na waalimu wa kutosha!.

Baada ya kujiuzulu, serikali ya JK ikazi abandon zile shule za EL ili kumkomoa!. Sasa zinaitwa St. Kayumba!. Mpango wa kufundisha waalimu wa ukweli, ukaachwa, nanachukulia wale failures wenye Div IV karibu na zero, na kuwa brush kwa miezi mitatu! (Waalimu wa Voda Faster!). Jana alipozungumzia umuhimu wa kuwaelimisha kwanza watu wetu, amenigusa sana!. Tungekuwa tumeelimika, tusingeibiwa hivi madini yetu!, tunaibiwa madini yetu huku tunaangalia kwa sababu hatuna elimu ya madini!, sasa tumegundua gesi,serikali inakimbilia kugawa vitalu kwa umiliki wa miaka 99 huku Watanzania hatuna hili wala lile kuhusu elimu ya gesi, hatuna sera wala sheria ya gesi!. Kwa kifupi, hutujui lolote wala chochote kuhusiana na gesi!, na tutaishia kuibiwa tena gesi yetu kwa kukosa elimu ya gesi!. Edward Lowassa ameshauri, hiyo gesi tuiache kwanza!, lets invest kwenye elimu kwanza kwa watu wetu, ili kuwa empower hawa watu wetu kielimu ndipo tuingie kwenye ambitious projects kama za kuvuna gesi, au kilimo kwanza etc!.

Kwa hili pekee, CCM ikimsimamisha EL, Tanzania itapata ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

Nimesema, CCM ikimsimamisha EL, 2015, itakuwa ni CCM tena, kwa sababu katika wapinzani wote, hakuna hata mgombea mmoja anayeweza kusimama na Lowassa kwenye urais wa 2015 na bado akaambulia kura!, there is no one!, none!.

Mwenye masikio na asikie!.

2. Dhambi Kubwa ya Lowassa ni Richmond Tuu!.

Najua wapinzani wa dhana ya ukweli, watakuja na hoja za dhambi kubwa ya Lowassa ni fisadi wa Richmond!, then time will tell, hiyo ni mizigo tuu ya watu, alijitolea kuibeba ili kwa kuteswa kwake, wao waokoke!, wakati muafaka ukifika, hili litawekwa wazi na Watanzania mtawafahamu wenye zigo lao haswa ni kina nani!. Wenye akili wameshang'amua ile metarmophosis process from Richmond -Dowans -Simbion na kwa msio jua, mkae mkijua Tanesco bado inailipa Simbion capacity charge ile ile ya dola 152 kama Richmond na Dowans, hivyo tumeruka majivu na kukanyaga moto, tumeruka maji na kukanyaga tope, na kwa usafi tumeruka nyasi, tukakanyaga ma..!.

3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hawana wa Kushindana Nae!.

Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli afya yake sii mgogoro kama anavyoonekana!, na CCM ikamsimamisha yeye, come 2015, then, mshindi wa uchaguzi wa 2015, ni CCM tena!, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yeyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulaini kama kumsukuma mlevi!.
Mwisho.
Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali ukweli huu mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa?! au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende huku inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kwa matarajio katiba mpya pia ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.

Asante.

Pasco.


 
* Hapo ndio nashindwa kuelewa watu wanaomshabikia Lowassa ni wa kundi gani hasa:


  • Je ni wale watakaopata au wenye maslahi kwa namna moja ama nyingine iwapo atakuwa Rais wa Tz....
  • Je ni wananchi wasiopenda mabadiliko na wanataka kupeleka business as usual...
  • Au ni watu wasiopenda upinzani kwa sababu binafsi na kwa vyovyote vile wanaona CCM iendelee kuwa madarakani tu..
  • Ni 'wanaolipwa' au marafiki zake ambao sio waadilifu wana 'ushawishi mkubwa kwa watu'....
  • Ni watu ambao hawajitambui tofauti za taarifa zilizopo kuwa wananchi wengi wanajitambua...
  • Ni wale wanaopenda kumsikiliza tu au wana imani kuwa anaweza kuleta mabadiliko....

* Siamini kama mtanzania anayeifikiria Tanzania miaka 10, 20 au 50 mbele anaweza kumshangilia Lowassa.....


Naamini hili umelisoma pengine itakupa jibu ya maswali yako.
Kwa namna mmoja isingekuwa vizuri kwa sasa kumponda Mhe.Lowassa maana bado chama haijampitisha kati ya waombaji 41.

Nadhani kupita kwa Lowassa ndani ya Chama chake na kuja huku nje kwa wananchi ni kipimo tosha kwa CCM na watanzania ndani ya CCM na Nje yake.

Idadi hiyo hapo chini ya Wadhamini DSM 212 150 imenifikirisha kuliko kitu kingine-kwamba wamejitolea bure kwa mapenzi yao na matumaini kwa mkombozi Lowassa.


CC Mzee Mwanakijiji.


[h=2]Kingunge anusa mchezo mchafu urais ndani ya CCM[/h]
Aiteka Dar

Lowassa aliwasili katika uwanja wa ndege wa zamani (Terminal 1), saa 2:00 asubuhi akitokea mkoani Arusha.

Mwenyekiti wa CCM wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alisema wanachama wa mkoa huo waliojitokeza kumdhamini ni 212,150, kati yao kutoka Kinondoni ni 95,251, Temeke (72,100) na Ilala (44,799).

Afananishwa na mtume, Yesu

Akimkaribisha Lowassa Dar es Salaam, Madabida alimfananisha waziri mkuu huyo wa zamani na Mtume Muhammad ambaye alikuwa akitangaza dini lakini alikuwa akipingwa na watu wake wa karibu na kufafanua kuwa kutokana na hali hiyo Mungu alimueleza kuwa hatamuacha na atakuwa pamoja naye.
 
Last edited by a moderator:

JIBU LA HOJA:
Inaonekana Lowassa bila kuwa na madaraka makubwa hawezi kufanya lolote. Amesema kuwa amekuwa Waziri kwa muda mrefu sana tangu wakati wa serikali ya Rais Mwinyi. Hivi kama Mbunge nahata akiwa Waziri ni sheria gani ambayo imetokana na mawazo yake ambayo ilipitishwa na Bunge kukabiliana na mojawapo ya changamoto anazozitaja?

Hapa ameishia hadi miaka saba hivi tu nyuma. Hivi baada ya kuondoka Uwaziri Mkuu Lowassa amefanya nini kitaifa? Ameleta mswada gani Bungeni, ametoa hoja gani kuhusu ajira Bungeni? Ametoa suluhisho gani? Au Watanzania wanatakiwa wampime kwa mambo aliyoyafanya akiwa Waziri tu lakini wasiulize aliyoyafanya akiwa Mbunge? Si mtunga Sheria yeye ametunga sheria gani kutuonesha angalau mwelekeo wa suluhisho la matatizo ya taifa letu?

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

Mkuu, hili ni swali la karne kama sio la milenia. ni wabunge wachache sana katika historia ya siku za karibuni waliothubutu kupeleka miswada binafsi. Wabunge wengi hawajui kazi ya kutunga sheria ni yao,wao kikubwa ni kulalamikaaaa na mwisho kusema " naunga mkono hoja"
 
Sisi wengine sasa tumeanza kuchoshwa na hizi kelele za kila siku siku fulani hafai!, kusema tuu fulani hafai, hakuwasaidii Watanzania, waliochoshwa na umasikini huu uliotopea, kama ungeshauri nani anafaa, utakuwa unatusaidia zaidi kuli kuishia tuu kuse,ma fulani hafai.

Tangu lini CCM imetuteulia kiongozi anayefaa?!, Rais Jayaya Kikwete nie rais anayemaliza muda wake, jee amefaa nini?!, miaka kumi sini hii sasa anamaliza?!. Kama Lowassa kwako hafai, it is fine, kwa sisi tunaomuona anafaa, tutaendelea kusimama nae, vingine kama hakuna anatefaa z`aidi ya huyu ambaye hafai, then ni safadhali huyu huyu asiyefaa, kwa sababu japo hafai, lakini ndiye aliyepo!, kuliko hao wanaofaa ambao hawapo!. Ukimuondoa Nyerere, Mwimyi alifaa?!, Jee Mkapa ndio alifaa?!, na Kikwete jee amefaa?!.

Kama huna jina la anayefaa, then huyuhuyu asiyafaa ndie rais wetu 2015 kupitia ndani ya CCM au nje ya CCM.

Kuhusu kufaa kwa Lowassa. mimi niliwahi kusema hivi.

[h=3]Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa..[/h]Nilisema hivi
Baada ya Edward Lowassa kusifiwa na rais Magufuli kuwa ni Superman, namdurufu kidogo Lowassa kwa kujikumbusha niliwahi kusema nini kuhusu mtu huyu.
P
 
Back
Top Bottom