Lowassa Hafai! Yes I said It - Sababu ya I

Nani anafaa?

UKAWA hii nchi sio ya kupeana kama pipi watu wanawachukulia poa wananchi haya kama yeye hahusiki na richmond nani muhusika mpaka wakina karamagi nao wanasafishwa wacheni hizo sasa hivi kila mtu tunaaminishwa ni msafi utadanganya watu wawili kwa wakati mmoja lakini sio kumi kwa wakati mmoja tunataka mabadiliko.
 
Kwa kuwa marais masikini wameshatuongoza vya kutosha,na wametufikisha tulipo. Kwa nini tusimpe urais tajiri ili nae tuone atatupeleka mpaka wapi!? Akizingua si tunammwaga tu muda ukifika!
 
Mada za kumchafua EL zimekua nyingi sasa. Inanifanya nijue yy ni bora kwa jinsi mnavyokesha kumchafua
Mdau usipate hofu kabla ya kufika darajani. Pumba na mchele zitaeleweka badae. Let political analysts put things on silver plate. Nitashangaa kama EL hatsfuata na kuheshimu ilani na sera ya chama chake. Badala yake a invent za kwake.
 
Hoja iliyo mezani ni je, Lowasa anatambua kuwa tatizo kubwa sana katika nchi yetu ni ufisadi uliokithiri? Yupo tayari kuupiga vita kwanza? Wewe acha kupiga kampeni za kitoto, jadili hoja kama msomi na kwa wasomi. Hatupo hapa kusikiliza upuuzi wako tunataka mjadala wa hoja na sio lamli zako dhidi ya Mzee Mwanakijiji.
 
Kujua au kufahamu kuwa lowasa hafai kuwa kiongozi wa nchi hakuhitaji kuvaa miwani ya kuona


Binafsi sipendi uchoyo au umimi. when you work as teamwork then kila mtu hulazimika kufanya juu chini kuhakikisha lengo linafanikiwa na sio nani kafanya nini. Watanzania hatuhitaji kumpa Edo nafasi nyingine ya kufanya! nasema hivi nikiwa na maana moja.

huyu mtu alikuwepo serikalini kwa muda mrefu, ameyaona matatizo ya taifa kwa jicho tofauti na wengine ambao hawajawahi kukaa juu huko. na ufumbuzi wa matatizo hayo anayosema/kujidai anayajua vyema ni kwa nini hakutoa ushirikiano kwa team yake (CCM) ku-overcome hayo matatizo?

Edo ni mchoyo, mbinafsi, ana umimi, ni jeuri. bora angekuwa na yote hayo huku anajua angalau tungesema anataka kutengeneza system yake afanye nayo kazi ila kiukweli hajui uongozi. Kiongozi hawi na sifa hizi. mabadiliko sio lazima uyalete kwa kukaa ikulu. hata huko nje ukiweza kuhamasisha usafi mtaani kwako ni mabadiliko! ukiwa na elimu ya kilimo ukawasaidia wanakijiji wa ulikozaliwa njia bora za kilimo tutasema unafanya mabadiliko! ukiweza kuongoza watu wakafikia lengo la kimaendeleo ni mabadiliko pia.

kwa atakaesema misaada makanisani na misikitini ni mabadiliko anakosea maana inagusa tabaka flani tu. naona ni kazi ya kueneza injili au uislamu.

Edo is FAKE. he is just trying to use some guys kufanikisha malengo yake, kwanza abadilishe jamii yake,

 
Sipingani na hoja ya MWANAKIjiji well said ila tatizo ni hizi mada naona ni nyingi mno na ni kuhusu lowassa tu. Kwani c kunawengine walio onesha azma ya kutaka urais. Je nani ni bora mbadala wa Lowassa??. Ndo kitu watu wanataka kujua.
Hao wengine hawajaweka ajenda zao kama alivyofanya Lowasa. Kinachojadliwa hapa ni hizo ajenda zake, mbona hilo lipo wazi wala halihitaji diploma kulifahamu.
 

Elimu bila kushughulikia ufisadi kutakuwa na tofauti gani na sasa? au unafikiria hawaweka mkazo kwenye elimu? si watakuonesha shule, vyuo na idadi mbalimbali "nyingi" tu? Hili la nani mwingine siyo hoja ya sasa wala haitusumbui sana; hakuna ambaye ameenda mbali katika kujinadi sana kama Lowassa. Hata kwa wenzetu US.. kwa demokrati anayefuatiliwa sana ni Hillary Clinton.. simply kwa sababu anaonekana ndiye mwenye uwezo wa kupitishwa kule... Hawaulizwi watu mbona wengine "hamwajadili"? labda hawana umuhimu kama wa Lowassa?
 
Kwa kuwa marais masikini wameshatuongoza vya kutosha,na wametufikisha tulipo. Kwa nini tusimpe urais tajiri ili nae tuone atatupeleka mpaka wapi!? Akizingua si tunammwaga tu muda ukifika!

yaani miaka mitano mingine au kumi baadaye? ukimwaga akatokea tajiri mwingine unafanyaje?
 
Unclean candidate with support of unclean people will deliver unclean products.
 
Nani anafaa?


mawazo yangu,nadhani tunaitaji rais aliyerizika,maana rais aliyekuwa masikini na akawajali masikini wenzake ni NYERERE tu baada ya hapo, maana kuanzia kwa wabunge wote wanaingia wakijidai masikini wenzetu wakifika huko wanafanya harakati za kuanga umasikini na kutusaau sisi masikini wakati sisi ndo tunawapereka bungeni,
 
Sipingani na hoja ya MWANAKIjiji well said ila tatizo ni hizi mada naona ni nyingi mno na ni kuhusu lowassa tu. Kwani c kunawengine walio onesha azma ya kutaka urais. Je nani ni bora mbadala wa Lowassa??. Ndo kitu watu wanataka kujua.

Kama kuna mtu mwingine anataka kujadili wengine si awajadili; ndio uhuru wa maoni. Kwani lazima mtu mmoja awajadili wote ili kuonesha aina fulani ya kuwa sawa? Tukisema huyu "hafai" kwani lazima tuseme "yule anafaa". Hizi siyo hesabu za 2 + 2 = 4...
 
Yes, Unclean candidate with support of unclean people will deliver unclean products.
 
Kama hauwezi kusema nani anafaa ili anye ajadiliwe kama Lowasa hoja yako inakosa nguvu. Hakuna anayekataa ufisadi ni kitu kibaya, hata hivyo sekta nyingine zote haziwezi kusimama ili kupanambana na ufisadi. Sitaki kuamini kuwa unamchukia Lowasa hata hivyo kwa kutokuwaambia watanzania na wasomaji wa JF wazi kuwa kama Lowasa hafai, yupi unayedhani anafaa utakuwa hautendei haki Watanzania na JF kama jukwaa. Kinsingi ufisadi hauhitaji kuwa sera ya maendeleo ya nchi. To me kiongozi ambaye ana nia nzuri na nchi ni lazima awe na sera na mikakai imara inayolenga kuondoa umaskini na kuipelekea nchi yetu kwenye uchumi wa kati. Endapo kutakuwa na mifumo dhabiti na dhamira ya kweli kusimamia kila hatua na kuwajibishana ufisadi unakufa wenyewe na wala hauhitaji kuwa ndiyo kipaumbele cha kulikomboa Taifa kwenye Wimbi la umaskini. Kwangu mimi ufisadi unakosa dhamira tu ya kusimamia misingi. Imekuwa ni hulka kwa vijana wengi kukaa vijiweni asubuhi hadi jioni bila kijishughulisha, na pindi anapotokea mmoja wao akajishughulisha na kuwa na maisha tofauti basi hupewe jina ufisadi. Kwa mantiki hiyo siungi mkono matumizi ya neno ufisadi kwa waliwengi Tanzania kwa kuwa linatumiwa kukatisha tamaa kwa vijana kutumia ubunifu na rasimali ili kujiletea maendeleo kwa hofu ya kuambiwa wao ni mafisadi. Suala la ufisadi linahitaji maamuzi na nia na haliwezi kuwa ndiyo msingi wa ukombozi wa Mtanzania.
 

hadithi ndefuu kuonyesha upeo wako wa kufikiri ulivyo mdogo,umekurupuka but kukurupuka kwako kutakusaidia leo...

Elimu kwanza ndio msingi,,elimu inabeba dhana zote ambazo wewe unapinnga,,watu wakielimika vyema watafundishwa kujiajiri,,wakielimika vyema wataffundishwa namna bora ya kilimo,,wakifundishwa vyema watajua namna ya kusaka masoko na kushindana,,usipoelimika vyema huwezi jua hata kama unaibiwa na haki zako,elimu itasaidia kufuta ufisadi unaosema wewe
 
Lowassa alishapigwa chini Uraisi the moment amemaliza hotuba ya kujiuzuru
 
Huwa mara nyingi siungani na hoja za kaka yangu Mwanakijiji. Lakini katika hili umenena ipasavyo.

Lowasa is charming unemployed youth na issue ya ajira. Yaani huku mitaani vijana huwaambii kitu juu ya huyu jamaa.

Tumaini langu na wale wote wanaoliombea mema taifa letu ni CC ya CCM kutenda haki kutuletea mtu sahihi kwa nyakati hizi.
 
Zitto , alikuwa akiwalaghai tu , muulize kama zilikuwa haziendi kwenye Akaunti yake ......Kachukua posho zote kama atabisha tuweke nyaraka hapa.......Mlaghai tu Zitto......

mkuu uhakika zitto alikuwa achukui hizo hela, wengine wote hovyo tu walinikera sana,jiulize unataka ml 289 kwa utumishi wa miaka mitano na wengine hawafiki kwenye majimbo yao lkn hawapandishi posho za madakitali walimu ambao wanatunikia zaidi ya miaka 35 inaingia akilini kweli?
 

Kwanza kaka mukubwa naomba katika mifano tumia mifano yenye uwiano! kufananisha siasa za US na TZ,hapo hapana...tuna level tofauti tena kubwa sana hasa katika siasa,still we have a long way to go....

Mimi nadhani labda unafikiri katika uchache,kwamba rasilimali za nchi ni kama nyumba yako au yangu au ya yule...angalia jiografia ya nchi ifikiri na kuielezea kwa upana uo,ni mpumbavu tu ndio ataingia hofu kwamba mafisadi wawili au mia au mia mbili watamaliza neema ya hii nchi,nasisitiza ni 'MPUMBAVU PEKEE'...tupo katika kipindi cha mpito kukua,kuna watu ao waTanzania wa baadae wataneemeka,tusisubiri mabadiriko kwamba lazima tuyaone sisi,sasa nguvu zetu zote,akili zetu zote,rasilimali zetu zote zijikite katika kupata ELIMU ya kiada na ziada.

Lowasa ana kitu (yaweza kuwa kibaya au kizuri) ndio kimecreate mvuto wetu wooote wa kumjadili...uoni hilo?usibeze,mbona atujamjadili mwingine?kwani hatufaham kwamba yupo nani na nani nao wanataka nafasi io?why EL?trust me,ana kitu...kilichovuta hisia zetu na za wengine.

Okay boss kazi,sina neno zaidi.
 
CCM inabidi waweke mtu mwenye very low profile lakini mkali na ana uwezo wa kukemea rushwa na hata akifanyiwa vetting atakuwa safi mpaka kwenye mirija ya moyo wake. Vinginevyo wajiandae kuwa wapinzani maana hakuna msafi kwenye list yao ya sasa hata mmoja.
Ufisadi kila kona kuanzia bandarini, richmond/iptl, serikali za mitaa, ujenzi, usafiri, mawasiliano, jumba jeupe sasa pamebaki wapi!!??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…