Lowassa awaomba wananchi wa Monduli wamlindie heshima asiyostahili

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Kati ya Mambo anayoyasisitiza Edward Lowassa kwenye Kampeni za kumnadi mgombea wa CHADEMA ni kuwa wananchi wa Mondululi wampigie kura mgombea wa chama hicho ili kumlindia heshima yake(yeye Lowassa)

Swali ni je ni heshima ipi hiyo Lowassa anaiomba kutoka kwa wananchi wakati Maisha anayoishi Lowassa na familia yake ni ya hali ya juu huku wakazi wenzake aliowaongoza kwa miaka ishirini wakiishi kwa maisha ya dhiki miaka yote. Jirani yake wa karibu kabisa eneo la NGARASH MONDULI MJINI hana huduma ya maji wakati kwa Lowassa maji yanabubujika masaa 24. Huruma ipi unaweza kumuonea mtu mbinafsi na mchoyo kama huyu?
Lakini swali kubwa la kujiuliza, tunapiga kura kumlindia mtu heshima au kumchagua kiongozi atakayeshughulika na kero za wananchi?

Wana Mobduli tujiongeze, muda wa kupelekwa pelekwa na Lowassa kama mazuzu umekwisha, ametunyanyasa sana ametudhalilisha sana na ametuonea sana. Inatosha
 
Mleta mada umeonyesha dhahiri chuki yako dhidi ya mh ENL. Kinachoendelea sasa ni siasa na mwishoni wananchi was Monduli watalinda heshima yao na siyo ya mtu fulani.
hata mimi ndiyo hoja yangu, watu wa Monduli tulinde heshima yetu kwa kumchagua kiongozi atakayetufaa siyo kwa sababu ya kulinda heshima ya Lowassa ambaye ametufikisha hapa tulipo. Lazima tumuoneshe sasa tunaweza kujiamulia mambo yetu wenyewe
 
Lowassa kategwa kaingia Mtegoni

Mwenzie Mbowe kule Hai Kila Siku watu wanarejea CCM lakin kauchuna
 
Majaribio ya Makombora yakifanikiwa Monduli yatajaribiwa Pia Pemba Kwenye Ngome ya Sultan Mwingine wa Ukawa
 
Acha kuwasemea watu, watu wa monduli wataamua wenyewe mbona kuna majimbo yanaongoza na sisiem toka uhuru mpaka leo hayana maendeleo .
 
Lowassa anapasa kujilindia heshima yake mwenyewe, heshima alio ipata akiwa mbunge kwa muda mrefu na baadaye PM
Kama anajielewa ni bora alinde heshima yake kwa kutopanda kwenye majukwaa ya kisiasa, kwani kujisogeza majukwaani ni kujipalia makaa mikononi mwake, angeyataka hayo angejifungia kwake aache vijana tung'atane wenyewe.
 
Mi nadhani huyu mtoa thread Naye ni mwanasiasa hivi unadhan mtoa thread n ccm.
 
Kwahiyo kwako wewe heshima ya Mh Lowassa ni kuishi maisha ya kimasikini kama walivyo Watanzania wengi?! Hakika mawazo ya kimasikini hayajamuacha mtu salama
 
Back
Top Bottom