Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa amechangia Sh. milioni 11 katika miradi ya maendeleo katika vijiji

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
634
1,000
Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa amechangia Sh. milioni 11 katika miradi ya maendeleo katika vijiji vya ujenzi wa nyumba ya daktari wa wilaya hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake kwa wapiga kura wa jimbo hilo.

Aidha Lowasa alisema fedha hizo ni mchango wa ofisi yake kwa kushirikiana na Taasisi ya ECLAT ambapo ofisi yake ilitoa Kiasi cha sh. Mil. 6.8 hukuku taasisi hiyo ikitoa sh. mil. 5.

Fredrick ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, alitoa mchango huo jana alipotembelea eneo litakalojengwa nyumba ya daktari wa wilaya.

Katika ziara yake hiyo alitembelea eneo la shule ya Msingi ya Indonyonado iliyoezuliwa paa lake na upepo, pamoja na zahanati ya Kata iliyopo Engutoto kijiji cha Mlimani.

Alitumia fursa hiyo pia kuwashukuru wananchi wa Jimbo hilo kwa kumchagua katika uchaguzi mkuu uliopita na kuahidi ushirikiano wa kutosha kwa wakazi wa Monduli.

“Ninawashukuru sana kwa kutuchagua kwa asilimia kubwa ninachoomba kwenu ni ushirikiano lakini pia muendelee kuiunga Serikali mkono kwa shughuli zote za maendeleo na Mimi nitahakikisha ninatekeleza ahadi zote nilizoahidi kipindi cha uchaguzi" alisema.

Lowassa aliyebeba kauli mbiu ya baba yake ya Elimu Elimu Elimu, alimuomba mfadhili huyo kushirikiana na Ofisi ya Mbunge na Ofisi ya Mkurugenzi kusaidia kujenga Shule ya Msingi Endonyonaado ambayo wananchi walijenga madarasa mawili na kupauwa lakini upepo ukaiezuwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la ECLAT DC, Peter Toima alimshukuru Lowassa kwa kumkaribisha jimboni kwake na kuahidi kumuunga mkono katika shughuli za maendeleo.

Lowassa alieleza namna alivyofahamiana na taasisi hiyo huku akidai kuwa baada ya kutembelea makao yake makuu yaliyopo Simanjiro aliamua kuwakaribisha jimboni kwake ili waweze kushirikiana katika kuleta maendeleo yenye tija.

“Kwa heshima hiyo na umuhimu wake alionionyesha Mbunge wa Jimbo la Monduli ninamuahidi kumuunga mkono wa dhati, Mbunge naomba nikajiandae kwa kazi hiyo na niaahidi mwezi wa saba ikimpendeza Mwenyenzi Mungu nakuja na wafadhili eneo hili la Indonyonaado,” alisema Toima katika taarifa hiyo.
 

Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
2,664
2,000
Huyo dc mstaafu TOIMA mwambie aache kumpiga mke wake na aache kumla mfanyakaz wake wa hyo raasis ya ECLAT
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom