Lowassa: Awamu ya pili inakuja

IamPrince George

JF-Expert Member
Nov 22, 2014
412
168
Trust me Lowassa ndio Rais wa hii Nchi,Wananchi wameamua, hakuna mfumo unaotoka kirahisi, nimesoma gazeti la mwananchi linasema Lowasa asema safari ya kuelekea ikuli ndo imeanza.

Yeah.... Safari ndo imeanza wakuu, hiyo ndio kauli ya shujaa wetu Edward Lowassa

Aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa amesema awamu ya pili ya safari yake ya kuelekea Ikulu ndio kwanza imeanza na kuwataka watu wote wanaomuunga mkono kutokata tamaa.

Lowassa, ambaye ameshika nafasi ya pili katika mbio za urais wa Jamhuri ya Muungano akiweka rekodi ya kukusanya kura milioni 6.07 ambayo ni rekodi kwa mgombea wa upinzani, alitoa kauli hiyo jana mchana katika hafla ya chakula cha mchana ya kuishukuru timu yake ya kampeni iliyofanyika Kawe, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa vyama vinavyounda Ukawa, wanahabari na familia yake.

"Nimefarijika sana, asanteni kwa msaada mlionipa, sina cha kuwalipa," alisema waziri huyo mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne aliyeihama CCM na kujiunga na Chadema mwezi Julai.

"Ukweli ni kwamba kila mmoja alifanya kazi yake. Tujiandae kwa awamu ya pili na safari ndiyo imeanza," alisema na kushangiliwa.

"Unaweza kuchelewesha bahati ya mtu, lakini hauwezi kuiondoa," aliongeza.

Hata hivyo, Lowassa hakueleza awamu ya pili itahusisha mambo gani.

Tangu kumalizika kwa uchaguzi huo, Lowassa amezungumza na vyombo vya habari mara mbili, mara ya mwisho akieleza jinsi alivyowasilisha pingamizi lenye hoja tatu kuhusu mwenendo wa uchaguzi kwa mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva ambalo liligonga mwamba.

Katika tamko lake, Lowassa alikuwa akipinga matokeo ya kura za urais yaliyokuwa yakitangazwa na NEC akidai kuwa si halisi na kuitaka isitishe kutangaza, lakini tume hiyo haikueleza lolote na badala yake iliendelea kutangaza matokeo ya majimbo na baadaye mshindi wa urais.

Mambo hayo matatu yaliyowasilishwa NEC ni kupunguzwa kwa kura zake, kuongezewa kura kwa mgombea wa CCM na kutangazwa matokeo batili kwa wagombea wa Ukawa.

Lowassa aliyeanza kwa kuwatambulisha watu wake wa karibu waliomshauri masuala muhimu na nyeti katika kampeni, akiwemo waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, alizungumza kwa kifupi, akitoa mfano wa jinsi majeshi ya ukombozi wa nchi mbalimbali barani Afrika yalivyorudi nyuma kujipanga baada ya kushindwa.

Muda mfupi kabla ya Lowassa kueleza hayo, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliufananisha Uchaguzi Mkuu na vita, akisema kulikuwa na njama za makusudi za kuhakikisha Lowassa hapati ushindi.

Alisema wagombea ubunge kutoka vyama vinavyounda Ukawa vya NCCR-Mageuzi, Chadema, NLD na CUF, waliibiwa kura na ushindi kupewa wagombea wa CCM.

Mbowe alisema kwa kuwa hawawezi kupinga matokeo ya urais mahakamani, watafungua kesi za kupinga matokeo ya ubunge.

"Tunachofanya, tunarudi nyuma, tunajipanga kukata rufaa kupinga matokeo katika majimbo zaidi ya 30," alisema Mbowe.

"Wagombea wetu waliokuwa wabishi na kupigana kwelikweli walitangazwa washindi, lakini kuna majimbo ambayo wagombea wetu waliporwa ushindi waziwazi kabisa. Kwa kuwa ubunge unapingwa mahakamani tutafanya hivyo," alisema Mbowe.

Miongoni mwa majimbo ambayo matokeo yake yalikuwa na ubishi ni Nyamagana, ambako mbunge maarufu wa Chadema, Ezekiah Wenje alishindwa na mgombea wa CCM,Stanslaus Mabula baada ya mvutano uliochukua muda mrefu. Pia mbunge wa NCCR Mageuzi, David Kafulila wa Kigoma Kusini aliangushwa baada ya matokeo kuibua mzozo mkali uliosababisha polisi kuingilia kati.

Mbowe pia alisema kuwa wanahamishia nguvu Zanzibar kuungana na mgombea urais kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad kudai haki yake.

Mbowe alisema kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi huo kina mkanganyiko mkubwa na kusisitiza kuwa kuanzia wiki ijayo Ukawa itapiga kambi kwenye visiwa hivyo kuhakikisha haki inatendeka.

Baadhi ya viongozi wa Ukawa waliohudhuria hafla hiyo ni makamu mwenyekiti wa Chadema –Bara, Profesa Abdallah Safari, mwenyekiti wa NCCR na mbunge mteule wa Vunjo, James Mbatia na kaimu katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu.

Chanzo: Mwananchi
 
Trust me Lowassa ndio Rais wa hii Nchi,Wananchi wameamua.Hakuna mfumo unaotoka kirahisi.Hata smartphone ukibonyeza button ya kufactory reset ama kuupdate software Simu lazima Izimike kwanza alafu Ijiwashe Upya ,Kipindi hiki ni Kipindi kile ambacho
unaweza kusema Kazi ya kudownload System Software Ya Mabadiliko imekamilika Sasa Simu Imejizima Ili Ikiwaka IWAKE NA MABADILIKO.Plz Above Plz Usiguse Simu wala kufanya Lolote Subiria Kidogo Inajiwasha Yenyewe Sasa Hivi.

Makamanda Peooopleeeessss

Nimesoma gazeti la mwananchi linasema Lowasa asema safari ya kuelekea ikuli ndo imeanza.

Yeah.... Safari ndo imeanza wakuu, hiyo ndio kauli ya shujaa wetu Edward Lowassa

Huku kwetu ni jumapili,vipi huko uliko
 
UKAWA mnajitia aibu mnavyoendelea kulia lia banah!Lowassa ndio mwisho wake mwaka huu kisiasa hasa za uraisi maana umri utakuwa umemtupa mkono ifikapo 2020!

Poleni jamani mtazoea tu hii hali
 
ikulu IPI kamanda KWA ninavyowafaham ukawa pigo kubwa walilopigwa ni lile LA kuwakamata vijana wao wa IT hawana mpya ccm wamewazidi kila kona.
mm ninachopata hasira zaidi jamaa waliwapa taarifa kuwa lazima wawachezee rafu na hata huko wanakotaka kwenda kushtaki walisikia hayo mambo ya rafu wao wakalegea na kubweteka wamepigwa rafu now wanalalamika nini??

lowasa alisema tupige kura kwa wengi tukapiga akasema kazi ya kurinda kura tumwachie yy kashindwa kazi yake sasa tufanyeje??

wakubali yaishe wajipange upya 2020 sio mbali sana kukijenda chama sehem ambazo ni ngome za chadema wajihakikishie wanajiimalisha vilivyo aisee.
 
UKAWA mnajitia aibu mnavyoendelea kulia lia banah!Lowassa ndio mwisho wake mwaka huu kisiasa hasa za uraisi maana umri utakuwa umemtupa mkono ifikapo 2020!

Poleni jamani mtazoea tu hii hali

Tutalipiza kupitia Zanzibar.Maalim akiwa raisi anaitishsa kura ya maoni kuamua kama wazanzibar wanataka muungano au hawautaki.Baada ya hapo Magufuli atakuwa hana kazi-tafakari utaelewa.
 
Tusipeane moyo, Lowasa hawezi tena kuwa rais wa nchi hii,

Ila nawaambieni hawa waliolewa madaraka iko siku yao mana wamejisahahu hadi wanatuma watoto wao watutukane mitandaoni
 
Trust me Lowassa ndio Rais wa hii Nchi,Wananchi wameamua, hakuna mfumo unaotoka kirahisi, nimesoma gazeti la mwananchi linasema Lowasa asema safari ya kuelekea ikuli ndo imeanza.

Yeah.... Safari ndo imeanza wakuu, hiyo ndio kauli ya shujaa wetu Edward Lowassa



Chanzo: Mwananchi
Huenda wanajiandaa kwenda ikulu kivuli au wanahamu na Segerea
 
Trust me Lowassa ndio Rais wa hii Nchi,Wananchi wameamua, hakuna mfumo unaotoka kirahisi, nimesoma gazeti la mwananchi linasema Lowasa asema safari ya kuelekea ikuli ndo imeanza.

Yeah.... Safari ndo imeanza wakuu, hiyo ndio kauli ya shujaa wetu Edward Lowassa



Chanzo: Mwananchi

Please!!!! majibu yameshatoka.Shocking.
 
Ajiandae hata atengrneze jeshi lake kama anaweza ila atambue kwambwa hii nchi inaitwa Tz na yeye hatakaa awe rais wa nchi yetu
 
Tutalipiza kupitia Zanzibar.Maalim akiwa raisi anaitishsa kura ya maoni kuamua kama wazanzibar wanataka muungano au hawautaki.Baada ya hapo Magufuli atakuwa hana kazi-tafakari utaelewa.

Umeeleweka vizuri sana.sasa tegemeo la ukawa ni maalimu sef je wao wenyewe wanajua kuwa maalimu sef ndio kete ya mwisho kabisa wanayoihitaji?
 
UKAWA mnajitia aibu mnavyoendelea kulia lia banah!Lowassa ndio mwisho wake mwaka huu kisiasa hasa za uraisi maana umri utakuwa umemtupa mkono ifikapo 2020!

Poleni jamani mtazoea tu hii hali

lowassa bmpaka sasa ana miaka 62, na samweli sitta ana miaka 70, prof. mwandosya ana miaka 67 na bado amegombea Uraisi. Wewe Vip?
 
Back
Top Bottom