Lowassa awaandalia dinner waandishi wa habari

Kasent

Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
57
Reaction score
7
Baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutangaza nia ya kugombea Urais, kasha kuungwa mkono wa Wabunge na wajumbe wengi wa Bunge maalum la Katiba, imezusha hofu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa, ambapo jana usiku aliwakaribisha waandishi wa habari nyumbani kwake kama njia ya kujuana na kubadilishana mawazo.

Hafla hiyo imefanyika nyumbani kwake mjini Dodoma na kushirikisha waandishi kutoka vyombo mbalimbali, kati ya mazungumzo hayo yualiegemea zaidi kujua namna siasa zinavyooonekana nchini na jinsi nafasi ya Urais inavyozungumza.

Njia hiyo ilipatia nafasi kufahamu nguvu za wapinzani wake zilivyo hasa Pinda ambaye amewavutia watu wengi kutokana na kuwa na sifa ya kutokuwa na makundi pamoja na tabia yake ya kufanya kazi kwa uadiulifu na maadili.

Hafla hiyo ambapo waandishi walikula na kunywa hawakutakiwa kupiga picha wala kutoa habari kwa kile kinachoelezwa ilikuwa kirafiki zaidi
 
Mtapoteza muda na fedha bure, Pinda hawezi kuwa raisi wa Tanzania. Kama uwaziri mkuu amekuwa dhaifu zaidi katika historia ya Tanzania kwenye uraisi bora tuchukue ushauri wa Mrema Lyatonga na kumuongezea muda JK kama tumekosa kabisa mtu wa kutuongoza.
 
mchungaji alimtabiria kuwa raisi asimuhofie pinda acheze na kamati kuu ya ccm
 
Rushwa nyingine hii ya ubwabwa na vinywaji ili wasimuandike vibaya kuelekea safari ya kutimiza adhma yake ya kuingia nyumba nyeupe 2015.
 
Ha ha ha
ubwabwa na soda???
kweli makanjanja
 
Pinda anawaogopa hata wakuu wa wilaya alafu anataka ukuu wa nchi.....
 
Propaganda hz mbaya, kwanini Lowasa anakua hajiamini? atulie
 
Muda ukifika nami ntaandaa MBEGE na KIMPUMU niwakaribishe walevi wenzangu na kubadilishana nao mawazo na kuomba waniunge mkono kwenye nia yangu ya kugombea URAHISI wa Chama Chetu. Ndoto hii nitaoteshwa tu hivi punde kama bwana Meeembe anavyosubiri kuoteshwa.
 
hii ni aina fran ya takrima na kujipendekeza anajua atapata promo aaaaah wap tunamjua huyu mtu ata mia anaokota huy sio mtu mzuri kabisaaaaaaaaaa
 
Baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutangaza nia ya kugombea Urais, kasha kuungwa mkono wa Wabunge na wajumbe wengi wa Bunge maalum la Katiba, imezusha hofu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowasa, ambapo jana usiku aliwakaribisha waandishi wa habari nyumbani kwake kama njia ya kujuana na kubadilishana mawazo.

Hafla hiyo imefanyika nyumbani kwake mjini Dodoma na kushirikisha waandishi kutoka vyombo mbalimbali, kati ya mazungumzo hayo yualiegemea zaidi kujua namna siasa zinavyooonekana nchini na jinsi nafasi ya Urais inavyozungumza.

Njia hiyo ilipatia nafasi kufahamu nguvu za wapinzani wake zilivyo hasa Pinda ambaye amewavutia watu wengi kutokana na kuwa na sifa ya kutokuwa na makundi pamoja na tabia yake ya kufanya kazi kwa uadiulifu na maadili.

Hafla hiyo ambapo waandishi walikula na kunywa hawakutakiwa kupiga picha wala kutoa habari kwa kile kinachoelezwa ilikuwa kirafiki zaidi

siku pinda akiwa rais natembea uchi mikoa mitano Tz
 
Back
Top Bottom