Lowassa atua Mwanza kusaka wadhamini, umati wampokea

Lowassa atua Mwanza kusaka wadhamini, umati wampokea

Jana, EL kazomewa na baadhi ya wananchi wa Mwanza waliofika kwenye viunga vya Gandhi Hall kwa kusema fisadi ilikuwa kabla ya kuingia ukumbini, baadhi ya waliosema ni Mr.Bahame Katibu wa vijana wa ccm tawi la Luchelele wakiwemo na vijana wengine wengi tu!

Pia, vijana wahuni wamepigana uwanja wa ndege Mwanza walipokuwa wakimsubiria, chanzo walipewa hela wakadhulumiana. Hela waligawana France Corner Bar mitaa ya Uhuru zoezi likifanywa na M/Kiti wa mtaa huo.

habari za kutunga bana......
sasa france corner ndo wapi?,mwanza hakuna france corner bana
 
Lakini mbona ITV wameonesha watangaza nia wote kasoro Makongoro? Ila taarifa ya habari walimuonesha lakini pia tuwe wa kweli ITV wapo kibiashara hiyo sio TBC.
Nilidhani nimeliona mwenyewe....ITV ni unafiki tu unafanyika...mzee Mengi kumbe ndio maana mamlaka zinampuuza.
Na kulialia kuwa anatishiwa maisha.
 
Mkuu mpk,hao si kama wale wa Sheikh Amri Abeid Arusha? Nina wasiwasi kuwa walitangulia au kutangulizwa

Watu wamesafirishwa kutoka arusha, moshi kuja kumsupport boss wao
 
Last edited by a moderator:
Jana, EL kazomewa na baadhi ya wananchi wa Mwanza waliofika kwenye viunga vya Gandhi Hall kwa kusema fisadi ilikuwa kabla ya kuingia ukumbini, baadhi ya waliosema ni Mr.Bahame Katibu wa vijana wa ccm tawi la Luchelele wakiwemo na vijana wengine wengi tu!

Pia, vijana wahuni wamepigana uwanja wa ndege Mwanza walipokuwa wakimsubiria, chanzo walipewa hela wakadhulumiana. Hela waligawana France Corner Bar mitaa ya Uhuru zoezi likifanywa na M/Kiti wa mtaa huo.

safi sana.....siku imeanza vyemaaaaaa kwa khabar hii
 
HERI SHETANI TUNAYEMJUA KULIKO MALAIKA MPYA"/Wapo watu au wagombea wengi tu ambao lengo lao kuu ni ili wawe MATAJIRI,

hivyo basi ni heri kumweka aliye tajiri kuliko kumweka MSAKA UTAJIRI

IKUMBUKWE TUHUMA NYINGI ZA MH.NA RAIS MTARAJIWA NI ZA MAJUNGU NA UONGO NA UNAFIKI


KUJIUZULU KWAKE ILI AINUSURU SERIKALI NDICHO LABDA KILICHOMPONZA HAKIKA MAJUTO MJUKUU!


***LOWASSA FOR PRESIDENCY***
 
Mimi nimeacha kununua magazeti na kusikilza redio flan mpaka uchaguzi uishe,habari natafuta vyanzo binafsi kipindi hiki mpaka uchaguz uishe sababu staki kuchezewa akili yangu na wahariri dhaifu
 
Tuache ushabiki wa kijinga. Kweli nawaambia alipokelea na watu wengi sana. Ila on a serious note... Lowassa looks sick and tired. Na vurugu ndo kwanza zinaanza.
 
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amechukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku akisema hana mpango wa kushindwa.

Lowassa aliwasili katika Makao Makuu ya CCM mjini hapa jana saa 10:20 jioni akiambatana na mkewe, Regina huku akisindikizwa na wabunge mbalimbali pamoja na wanachama wa CCM. Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wanachama waliokuwapo katika Ukumbi wa Makao Makuu ya CCM mara baada ya kuchukua fomu, Lowassa alisema hawezi kuzungumzia upande wa kushindwa katika safari yake. “Swali rahisi sana, sina mpango wa kushindwa,” alisema Lowassa alipokuwa akijibu swali aliloulizwana waandishi wa habari kama atashindwa katika kinyang’anyoro hicho.

Alipoulizwa kuhusu hali ya nchi kuwa na watu wanaoshambuliwa, Lowassa alisema atajenga Serikali itakayojali utu na uhuru wa vyombo vya habari. “Kwanza nimpe pole yule mwandishi wa MTANZANIA aliyeteswa. Sikubaliani na mambo ya kuingilia uhuru wa watu kuteswa. Serikali yangu itaheshimu uhuru wa vyombo vya habari,” alisema Lowassa huku akishangiliwa na wanachama wa CCM waliokuwa wamefurika ndani na nje ya ukumbihuo.

Alipoulizwa kwanini anahusishwa na vitendo vya ufisadi, Lowassa aliyekuwa akijibu maswali kwa ufupi, alisema kama kuna mtu ana ushahidi na tuhuma hizo amtaje jina.“Kama hawakunitaja hawakunihusisha… Mtu anayejiamini aseme, na anitaje. Nachoka na siasa za tuhuma, hatupimi viongozi kwa rekodi za matusi ila tutawapima kwa matendo yao,” alisema.

Kada huyo wa CCM alivitaka vyombo vya habari kutoshabikia tuhuma zisizo na ushahidi, huku akisisitiza kuwa kila mtu apimwe kwa rekodi yake.Kuhusu uteuzi wa mawaziri, Lowassa hakutaka kulizungumzia akisema bado hajavuka daraja. “Nitavuka daraja nitakapolifikia,” alisema.

Kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alisema ni seraya CCM iliyotekelezwa baada ya kutokea mgogoro kati ya vyama vya CCM na CUF. “Angalieni kule Marekani, vyama vya Democrat na Republican, vinashindana kwa kura chache sana. Hata sisi tunapishana kwa kura chache, mimi nadhani kama hatupishani sana hivyo hilo ndilo suluhisho,” alisema.

Awali Lowassa aliwashukuru wana CCM waliofurika katika ukumbi huo akisema anajua kero za chama hicho na atakapokuwa rais atazishughulikia. “Nawashukuru kwa kunileta nyumbani, nimeitumikiaCCM kwa muda mrefu. Nilieleza Dodoma na Arushania yangu. Naelewa matatizo wanayopata watumishiwa CCM, nayaelewa. Mishahara midogo, hawakopesheki, hawana fedha za likizo na hawana uchumi mzuri. Wakati wengine wanajengewa nyumba na mikopo wenyewe hawapati,” alisema Lowassa. Hata hivyo, alimsifu Rais Jakaya Kikwete kwa kuimarisha uchumi ndani ya chama hicho, lakini akasema akiwa rais atafanya zaidi. “Tunaweza kufanya zaidi, tusiwe ombaomba. Nilipokuwa mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini tumejenga jengo la ghorofa 22 Dar es Salaam. Tuna viwanja na maeneo mengi. Nikichaguliwa kuwa rais na mwenyekiti nitaangalia hilo…Bila CCM madhubutinchi yetu itayumba,” alisema.Baada ya mkutano huo, Lowassa alikwenda kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Dodoma kupata udhamini wa chama hicho ambapo Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pancras Ndejembi alikuwa miongoni mwa wanachama waliomdhamini, akiwamo mlemavu wa miguu, Idd Omari.

Baadhi ya vigogo waliokuwa ukumbini ni pamoja na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba na Mbunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah.

Chanzo: Mtanzania
 
Ukweli juu ya lowasa utatuweka HURU!
Ukizingatia historia yake kiuongozi, elimu yake na matokeo ya madarasani, hoja zake, sauti yake, upangaji wa mada, maana za hotuba anazotoa, na hasa ukiangalia hotuba yake siku ya kutangaza nia utaona kuwa ana upeo mdogo sana na hana uelewa wa kutosha wa mambo. Ana chuki sana, mdomo sura na matendo yake viko mbalimbali, ana hasira sana, ni mtu wa kukurupuka sana bila kufanya utafiti, ni jeuri na ana kisasi sana. Utafiti umeonesha kuwa IQ ya lowasa ni below 30%. Uwezo wake ni kuongoza ng'ombe wala sio watu.
ANAAMINI PESA NI KILA KITU KWAMBA INAWEZA KUWANUNUA WATZ NA AKAWA RAIS WAO.
Nahisi lowasa hata bange anavuta.
Jambazi sugu na fisadi papa na mgonjwa lowasa kamwe hawezi kuwa rais.....

Ukwel mtupu
 
Sijui kama ataweza kuendelea kuwanunua watanzania ipo siku atapoteza pesa nyingi mwisho wake atapigwa mweleka mkubwa sana ngoja tusubiri.
 
Acha mambo ya kike dume zima unaandika umbea utaolewa wewe

We mrundi rudi kwa Nkurunzinza huna uzalendo hilo tumbo kwa laki utufanye sisi wakimbizi kama kwenu.Br.use ragione è non pancia.
 
Watanzania wenzangu kumbukeni maneno ya waasisi wenu 'mwogopeni kama ukoma' mkiyakataa basi msimuite yule baba wa Taifa mwiteni mamvi baba wa Taifa. 'asiye sikia la mkuu...'.
 
Nimeipenda hii.. tukianza kufikiri kisayansi tutaweza kuchagua kisayansi......
 
Wengi wanaomponda lowasa ni timu tiifu kwa padri wa kichaga

Tumbo na njaa vinakukosesha uzalendo.pole na wewe ni hatari kwa vizazi vya kesho,hufikirii kwa kichwa bali tumbo la laki uliyo pewa.
 
Kashaanza kuongea? Maana huyu jamaa ni kama betri ichajiwe kwanza.
 
Back
Top Bottom