Lowassa Atoshaa: Wajumbe wa NEC YA CCM Wanena

Lowassa Atoshaa: Wajumbe wa NEC YA CCM Wanena

Mkuu ocampo four mimi kila siku ninajiuliza huyu babu ataenda kujijitetea vipi kwa mungu kwa kosa la kumuasi na kula kondoo alioahidi kuwachunga tena kwa kiapo.

Mkuu hiyo ni hatari sana hivi unawezaje kumuamini mtu alimkana Mungu wake aliyempa pumzi na uhai sembuse wewe binadamu usiyemfaa kwa lolote?
 
Last edited by a moderator:
Kuna fisadi kama Dr Slaa aliyeiba mke wa mtu, kuna fisadi kama Mbowe aliyempa Gekul mimba?, kuna fisadi kama Mdee anayesaga wadada wadogo wadogo kwa kuwarubuni na posho za bunge?

Du Kweli UJINGA HAUNA KIKOMO, Naona huelewi maana ya fisadi, Kwa jina jingine mnaitwa 'MANYANG'AU'
 
hivi watanzania mmekuajeeeeeeeeeee h
aaa??????????? yani hauwezi kuongea bila kuweka kizunguuuuuuuuuuuuuu?????? mnashangaza sana

 
Eti Lowasa ndio rais,kuna watu walishaapa kuwa Lowasa hawezi kuwa rais wala m/kiti wa CCM na akiwa rais wanahama nchi wala hawezi kutoka kaskazini,prince na Paul Makonda mtawaua kwa pressure ooohoo!
 
kwa iyo imefahamika ...ni Lowasa V. Slaa (2015), CA TLR .............eh eh eh

Lakini, si inasemekana rais ajaye hawezi kutoka KASKAZINI, au???????
 
Ikulu ni mahara patakatifu,ikulu siyo guest house ya kulaza wezi na majambazi!!!
 
Mkuu ocampo four mimi kila siku ninajiuliza huyu babu ataenda kujijitetea vipi kwa mungu kwa kosa la kumuasi na kula kondoo alioahidi kuwachunga tena kwa kiapo.

Unaijua historia ya mfalme Suleiman?
 
Last edited by a moderator:
Nikushukuru sana Ocampo kwa mtu yoyote aliekuepo dodoma ni shaidi kuwa nguvu ya lowasa ni kama upepo aina ya yura kilo
 
Pamoja na kile kinachodaiwa kuungwa mkono na wajumbe wengi wa NEC, utashangaa jina lake halitafika NEC. Anaweza akapigwa ngwala CC. Muulize John S. Malechela. Achana na CCM bwana!
 
EL ataikatakata CCM vipande vipande kama watadhubutu kukata jina lake. Sisi tunamsubiria mshindi wao aje ajipime nguvu na mgombea wetu wa wananchi.
 
Kuna fisadi kama Dr Slaa aliyeiba mke wa mtu, kuna fisadi kama Mbowe aliyempa Gekul mimba?, kuna fisadi kama Mdee anayesaga wadada wadogo wadogo kwa kuwarubuni na posho za bunge?

Wewe ni mchafu na akili yako chafu. You should be ashamed of yourself! Unaweza kukuta ni mtu mzima na una familia na hii inaonyesha jinsi ulivyokosa malezi bora. nakuonea huruma maana inaelekea hujui usemalo labda ulikuwa victim wa sexual na physical abuse ulivyokuwa mdogo. You should seek help because you really need some psychological help!
 
Hivi we saa nane umepewa kitengo gani saizi?
Cha kubeba sumu nani ameachiwa?

kwikwikwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! kwikwikwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! kwikwikwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! mbavu zangu mie! jamani jamani mbavu zangu mie! kwiiiiikwiiiiiiiiiiiiiiiiiiikwiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!! opfuuuuuu! ah! jamani!
 
Haiingii akili kabisa kwa mtu mwenye akili timamu kumpigia chapuo eti Edo awe raisi wa nchi hii, wakati kihasilia hafai ata kuwa jirani au kupanda nae gari moja. Ukiicheki record ya Edo utagundua kuwa huyu jamaa ni aina fulani ya Ebola katika uchumi wa nchi yetu. Cha kushangaza ni huyu anayetumia ID ocampo four kumpigia chapuo hili janga la taifa.

Ila mimi na familia yangu tunajivunia Mungu wetu na siku zote tunamtumaini yeye. na hata kama hiki kirusi kikipita najua kwa indicator aliyowashiwa na mwenye mamlaka tutafanya uchaguzi mwingine baada ya miezi michache na sio miaka 5.

Bwana edward inaonekana ww unamfahamu sana Lowasa hebu tusaidie na sisi tufahamu mabaya yake..ila tafadhali swala la richmond tunalijua nje ndani..tupe mengine ili tumuepuke mtu huyu.
 
Tumetoka Dodoma, katika kikao cha NEC-CCM, watu wakiwa na faraja tele, wakiwa na furaha tele, wakiwa na matumaini tele, wakiwa wamejazwa nguvu mpya, taa zao zimejazwa mafutao tayari kabisa kwa kuangaza hata usiku wa giza nene…

Kama ulikuwa mgeni katika mji wa Dodoma kuanzia jumatatu iliyopita picha ya kwanza ambayo ungepata ni kana kwamba huo mji unaitwa Lowassa…..Nilikutana na mzungu moja (alikuwa anatoka katika mbuga ya wanyama-Swagaswaga game reserve), swali aliloniuliza huu mji unaitwa Lowassa or Dodoma, kwa kweli nilishangaa sana ila kama mtafiti nilijiuliza kwa nini kaniuliza hili swali?. Kabla ya kuanza kufanya utafiti nilimuliza why are you asking me that question? Akanijibu kuwa kila anapopita anaona kuna mashati na tshirts nyingi za njano na kijani wanachozungumza ni lowassa lowassa lowassa, ndicho nilichokuwa nasikia, infact niligundua kuwa huyu mzungu anapenda utani ingawa mwishoni tulikaa pale Dodoma Hotel na kuanza kupiga stori za siasa, alinipa stori nyingi sana za Tony Blair (aliyekuwa PM wa Uingereza) hakuishia hapo tu bali alikiri wazi kuwa 2015 lowassa is going to be the president…..

Baada ya hayo maongezi Ocampo four kama kawaida yangu napenda kudadisi na kufanya utafiti kuhusu maswala ya kisiasa, bila shaka nilichukua hili jukumu na kuanza kufatilia kwa undani….Kwa kweli ndugu zangu nilichokiona ni zaidi ya alichonieleza mzungu (Kumbuka, inawezekana hii ndio NEC ya mwisho kabla ya mkutano mkuu wa kumpata mgombea urais).

Nilipita maeneo hayo ya Dodoma Hotel jina lililotawala ni Lowassa, nikaenda maeneo ya Nyerere Squire jina lililotawala ni Lowassa, nikaenda maeneo ya sokoni (kwenye mitumba) jina lililotawala ni la Lowassa, nikaenda katika viunga vya jengo la makao makuu ya CCM jina lililotawala ni la Lowassa, nikaenda katika mnada wa ngo’mbe jina lililotawala ni la Lowassa, nikaenda area C, D, E jina lililotawala ni la Lowassa, nikaenda Hotel kama St Gasper, Gift Land, Dodoma Canival, Summit, Mvita jina lililotawala ni Lowassa, nikaenda sehemu maarufu kama Chako ni Chako hapa ndipo niliweka mikono juu kila meza, kila kiti jina la Lowassa lilitawala sana, hapa nilipata fursa ya kuongea na wazee kadhaa wa idara ya pale Makumbusho na marafiki zangu vijana wa Hosea walisadiki wazi kuwa 2015 rais ni Lowassa….

Ila kama mdadisi na mtafiti nilitaka kujua kwa nini katika hizo sehemu ninazopita watu wanamuitaji Lowassa, nimepata kunukuu baadhi ya watu nao wakasema, “Unajua kijana kwa sasa tulipo na tunapotaka kwenda lazima tuwe na rais mwenye maamuzi magumu sana, na mwenye uwezo wa kuchukua hatua za haraka na mwenye uwezo wa kusema na kutenda na ndani ya CCM mtu wa jinsi hiyo ni Lowassa pekee” Mwingine kutoka Mwanza ambaye ni mzee ninaemueshimu sana na tajiri mkubwa mwanza aliweza kusema “bwana mdogo hapa tulipo hatutafuti mtu wa kuwa rais tu bali huyo mtu awe na uwezo wa kuwa mwenyekiti wa CCM at the same time, sasa wewe sii umesoma unafikiri nani anaweza kuvaa hizo kofia mbili kwa wakati moja kama sio Lowassa”. Sikuishia hapo nilitafuta wajumbe wa kanda ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania waliweza kusema “Tunamtaka Lowassa kwa sababu rekodi yake katika utendaji ndani ya serikali na kwenye chama iko wazi, tokea 1990’s amekuwa waziri wa maamuzi magumu na yenye tija kwa wanachi, nashangaa kuna wengine walikuwa nje huko ulaya hawajui hata kuna matawi mangapi ya CCM afu leo wanataka urais, we subiri tutakutana may 2015”.


Sikuishia hapo nilienda waliposhukia wajumbe wa Shinyanga ambapo nilipata bahati ya kupeana mkono na Mgeja, ila nikamwambie mkuu Mgeja nina maswali kwa hawa wajumbe wako tupishe kidogo (nilifanya hili kwa sababu nilitaka objective answers, kumbuka Mgeja ni front man) wajumbe hao waliweza kusema “Unaona hili shati bila Lowassa leo nisingelivaa hapa kwa sababu nimelinunua tokea mwaka jana na yasingekuwepo maji ya ziwa victoria aliyotuletea Lowassa lingeshachafuka na kuwa jekundu kabisa, maji ya Lowassa yamekuwa ukombozi mkubwa sana kwetu watu wa shinyanga; kwa kweli sisi watu wa Shinyanga tunawaomba wagombea wengine wasipite kabisa kutuomba kura tushaamua kura zote za Lowassa, na tunamuomba kijana wetu Ngeleja arudi tuwe pamoja” Sikuishia hapo nikaenda kwa wajumbe wa Zanzibar nao walisema “Kijana imefikia kipindi tunataka rais mwenye msimamo, ebu angalia kama hili issue ya katiba tumeyumbishwa sana, mara chama kinasema hiki, serikali kinasema hivi, wananchi wanasema hivi, yaani kila kona ni kelele kelele za katiba, ila tukipata rais mwenye msimamo akisema hii ni tisa na ni tisa kweli kweli haijalishi umekaa upande gani” ……


Wengine walisema, katika msingi wowote ule wa upendo kuna uhuru wa kuchagua, hivyo tunakipenda CCM kwa dhati, hivyo watupe na sisi uhuru wa kuchagua rais tunayemuitaji, na kama uhuru huo ukiwepo bila mizengwe ya aina yoyote lazima Lowassa atashida tena round moja tu trust me my friend, ngoja nikupe siri NEC kuna wajumbe 360 mpaka sasa lowassa anauhakika wa wajumbe 289 naomba unielewe ana uwakika wa wajumbe (karudia tena)…Hivyo ushindi ni wazi kabisa na ni huyu mtu pekee atakayeweza kupambana na Dr.Slaa, kwa akili yako wewe unafikiri nani anaweza kupambana na Dr. Slaa zaidi ya Lowassa. Kwa sababu kuna dhana moja kwa wananchi ambayo ni mabadiliko, katika hiyo dhana ya mabadiliko wananchi wanaona ni Lowassa tu ambaye anaweza kuwapa mabadiliko na naomba ukumbuke Nyerere alisema kama mabadiliko hayatapatikana ndani ya CCM watayafata nje ya CCM, hivyo wakileta mizegwe na kunyima watu uhuru wa kuchagua mabadiliko wanayoyataka sio siri mchakato utakuwa mgumu sana sana ndugu yangu ila tusiombee hilo, naamini chama chagu wanajua kwenda na upepo.

​
1995 Jakaya alishinda kutokana na upepo wake na kumbuka Jakaya ilifikia kipindi mchakato wake ulikuwa mgumu sana ilifikia kipindi wakatoleana maneno makali na katibu mkuu wa wakati huo Lawrence Gama (kama mtafiti sikuweza kuchukua haya maneno for granted bali nilienda katika secondary data na kubahatika kupata Gazeti la Majira ya tarehe 14, julai, 1994 la siku ya ijumaa yenye kichwa cha habari Vigogo kuigawa CCM-KIKWETE) katika andiko hili nanukuu maneno ya jakaya “Haiwezekani refa (Gama) agawe uwanja sehemu mbili: wengine wacheze kwenye uwanja wenye magugu marefu na wengine wachezee kwenye uwanja mzuri na tambarare” alisema Kikwete. 2005 Kikwete akakumbana tena na kizingiki kikubwa safari hiyo walikuwa Mangula (makamu wa ccm wa sasa) na Mapuri (alikuwa katibu wa sera na uenezi) ila Kikwete akatoboa kutokana na upepo wake. Watu wa namna hiyo leo hii pia wapo wanaojaribu kupunguza nguvu za lowassa ila tunawaambia kama jinsi Kikwete alivyotoboa mwaka 1995 na 2005 hivyo hivyo Lowassa atakavyotoboa.

ANGALIZO
Huyo mzungu niliyekutana nae Dodoma Hotel aliweza kunipa nukuu moja ya Tony Blair kuhusu opinion polls, Tony Blair alipata kusema kuwa kuna kipindi mhusika au kundi lake wanapata furaha zaidi kuhusu opinion polls na wakajisahau hilo litakuwa pigo kubwa sana……Hivyo basi natoa rai kwa wataka mabadiliko wote kamwe tusibweteke na hiyo hali iliyokuwa Dodoma ingawa mioyoni mwetu lazima tufurai kidogo…….. Acha watutukane sana, acheni watupe kashfa sana, acheni watupake matope, ila sisi tuzidi kujipanga na kujiimarisha, na wala tusiwatukane, tusiwajibu na kashfa zao, na tusipoteze muda wa kuzozana nao hata kidogo.

WITO
Kama mtafiti huru naomba niwatie moyo vijana wa EL, hii ni safari ya matumaini sio kazi nyepesi kwa hakika tulianza safari yetu naweza kusema UKEREWE kuja IKULU saizi tumefika pale maeneo ya IFM bado mita chache sana kuweza kuingia ndani ya Ikulu kamwe tusirudi nyuma, kamwe tusikate tamaaa, inawezekana viongozi wachache wa juu wanafanya hujuma, wagombea wengine tunasikia wameletwa na mke wa rais, wengine ndio wanadola saizi, ila kamwe tusirudi nyuma hata kidogo. Katika mapambano yetu tusikubali watu watupoteze kwenye FOCUS kwa maana nyingine tusithubutu kutoka kwenye FOCUS, nawatia moyo na faraja kuwa ushindi tayari tunao, tunapoenda katika mapambano tukumbuke zile nyimbo zilizowaunganisha walionyonywa kama zile za Sarafina (RSA), tukumbuke nyimbo za solidarity forever, tuzidi kutiana hamasa, tuzidi kufanya maombi na dua kwa pamoja, ‘tukumbuke nyimbo za umoja na zaidi ya zaidi tupambane usiku na mchana..
Tunashukuru sana sana kwa wajumbe wa NEC kwa kusema Lowassa atosha, uso kwa uso nimeongea na nyie kwa ujumla wenu (wajumbe 263) tunasema ahsanteni sana sana na Mungu awabariki.

Asanteni sana…
Ocampo four

Ocompo four Edward is my favourite candidate for presidency, but I am bit worried about his health status. He appears physically weak. What do you say this on a sincere and serious note.
 
Back
Top Bottom