Lowassa atoa mpya.............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa atoa mpya..............

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 5, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,655
  Trophy Points: 280
  Lowassa awaonya vigogo wanaojali matumbo yao


  na Violet Tillya, Arusha


  [​IMG] WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ametoa wito kwa wabunge na madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi mkuu uliopita kuhakikisha wanafanya kila liwezekanalo kubadilisha hali ya maisha ya wananchi wao kiuchumi. Kadhalika amewataka viongozi hao kuweka kipaumbele katika kujali matumbo ya wapigakura wao ikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kuwakopesha ili waweze kuanzisha miradi ya kujikwamua kiuchumi kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili wananchi wengi hapa nchini.
  Lowassa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika kijiji cha Manyire, Kata ya Mlangarini, wilayani Arumeru alipokuwa akizungumza katika sherehe za kuwapongeza na kuwashukuru wananchi wa kata hiyo kwa kumchagua diwani wao Mathias Manga (CCM).
  "Wakati umefika kwa viongozi katika maeneo mbalimbali hapa nchini kubadilika na kuacha tabia na mazoea ya kujinufaisha wao wenyewe na familia na jamaa zao na kuhakikisha kuwa wanajikita zaidi kuwatumikia wananchi hususan kujali wanakula nini"� alisema Lowassa.
  Pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uamuzi wake wa kukubali mabadiliko ya Katiba na kutoa wito kwa wananchi kuhakikisha kuwa wakati ukifika wajitokeze kwa wingi kutoa maoni yao.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,655
  Trophy Points: 280
  kweli nyani haoni kundule.......yaani huyu Lowassa sasa amekuwa ni mtu wa kuhimiza maadili ambayo yeye mwenyewe wala hayafuati.................Is this not a case of preaching water while swilling wine when nobody is watching?
   
 3. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  It is a mark of an educated mind to be able to entertain a thought without accepting it

   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 5. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mnashangaa nn wakati ninyi mnaomwona mmbaya ndo ninyininyi mnaompa kura?
  BTW anajiandaa kwa 2015!
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ashindwe!
   
 7. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Kwani kama baba yako akiwa na tabia ya ulevi wa kupindukia,hawezi kukuambia mwanangu usinywe pombe fanya moja,mbili,tatu........???Hii inaonyesha anajua lile lililo sahihi na wanalostahili kufanyiwa wananchi na ndo anachohamasisha.........wachungaji wangapi wanatuambia tusizini nao wana wanawake nje ya ndoa zao?????????????Mwenzenu kaliona........................anafanya na kuhamasisha wenzake.........LOL
   
 8. hee-wewe

  hee-wewe Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  alegee
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Kwani kulewa sawa na wizi?....walevi wanafungwa?
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Sehemu gani ya mwili?
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kwa jinsi wadanganyika tulivyo vishoka/ wasahaulifu huyu 2015 atakuwa tayari mtakatifu na anachukua nchi.
   
 12. G

  Godwine JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  lakini ka mtu haka kanachukua urais hivi hivi kimchezo mchezo

  ha ha ha kweli bongo si nchi
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  i love this one...

  Aanze kwa mfano tu, arudishe japo asilimia 50% aliyochuma kuneemesha tumbo lake kwanza na pia atusaidie kujua dowans ni ya nani
   
 14. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Lakini nae atataka aonje ajue ladha yake kwanini baba yeye anywe halafu mimi anikataze kama ni mbaya mbona haachi...........Yeye ndio alitakiwa atoe mfano wa uongozi bora ndio awaelekeze na wengine. Anasubiri gawio la bil. 189 Dowans halafu anawaambia watu wafuate maadili ya uongozi, wawatumikie wananchi na wasijiangalie matumbo yao?

  Angalizo langu ni kuwa huyu bwana anajisafisha na ndio Rais ajaye wanaempandikiza maana kwasasa amekuwa mstari wa mbele kuonya mabaya (narejea kauli yake aliyosema wiki chache zilizopita wakati wa mbio za umeya kuwa vyama vya siasa ccm/ chadema visijaribu kutibua amani iliyoko Arusha pamoja na hii ya leo kuwataka viongozi wasijali matumbo yao bali wawatumikie wananchi). Amini nakwambia Wadanganyika tutamchagua tu huyu 2015 kama akipitishwa.
   
 15. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,382
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  Lowasa huyuhuyu naye anaweza kutoa ushauri?.........watu wengine km lowasa na rostamu wangeendelea kukaa kimya tu km wafanyavyo wakiwa bungeni na waendelee kuongoza majimbo yao ya watu vipofu
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aanze yeye kuonyesha mfano!Huwezi kumwambia mtu asiibe wakati wewe mkono wako uko kwenye mfuko wa mtu mwingine tayari!!
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ni vizuri akianza kwa kusema kwanini yeye anafanya ambacho hataki wengine wafanye, anatakiwa kuwa wa mfano. Sio kuwaambia watu wafanye alichoshindwa kufanya.
   
 18. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Bwashee umenichekesha nn. Huu msisitizo nimeukubali.............
   
 19. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Katika Biblia Takatifu kuna kuna mstari unasema, "Toa kibanzi/boriti katika jicho lako ndipo uweze kuona kibanzi/boriti katika jicho la mwenzio"
   
 20. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hahahaha MONTESQUIE! Thats a gud 1.
   
Loading...