Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,701
- 6,931
Katika ibada ya kuwekwa wakfu askofu wa kanisa la KKKT, mgombea urais wa chini chini kwa ticket ya CCM Edward lowassa ametoa matamshi makali sana dhidi ya watu wanaodhani nchi hii wana hati miliki nayo " Hii ni nchi yetu sote, hamna mtu mwenye hati miliki na nchi hii" Bila shaka alikuwa anapeleka ujumbe mzito sana kwa familia ya Rais, waache kabisa kumpigia debe waziri Membe kinyume cha utaratibu unaoeleweka na chama.
My take: huyu mtu akija pata madaraka atalipiza kisasi kibaya sana...ana hasira sana sana...
Hapa nakubaliana na Lowasa kuwa wenye nchi hii ni watanzania wote na katiba inasema wazi. Katika kugombea uongozi wowote ule demokrasia lazima itamalaki.
Kwenye kuvua gamba walimshindwa, barua ilienda kwa JK mpaka leo hiko kwenye draw; sasa kwenye Urais watamzuia? Kwa sababu sifa zake ni sawa na za hao walipo madarakani.
Nahisi saa ya CCM kukatika vipande viwili umewadia!!!