Kijakazi
Platinum Member
- Jun 26, 2007
- 9,363
- 15,096
dhahabu inatumika kama mapambo mbona thamani yake ipo juu ??
hayo magadi yangekua dili kama unavyotaka kumaanisha watu wangekua washagawana vitalu acha uj.inga hebu changanya na zako
magadi matumizi yake hasa ni nini ukitoa kupikia
Duh! wewe mshikaji! Anyway ngoja nijaribu kukupa darasa! Dhahabu matumizi ya urembo nisehemu ndogo sana matumizi makubwa ya dhahabu yako kwenye mambo ya finance nchi nyingi huwa zinahifadhi dhahabu matani na matani kama usalama inapokuja kuna kushuka thamani kwa fedha kiasi cha fedha kupoteza thamani basi nchi nyingi hutumia dhahabu, ndio maana kila nchi huwa zinaweka Benki kuu dhahabu nyingi sana, matumizi mengine kwenye mambo ya microelectronics, dhahabu hutumiwa sana ktkna na tabia zake za kimetali kwenye simu yako mkononi kuna dhahabu Ag metal, kwenye computer yako kuna dhahabu, TV yako kuna dhahabu n.k hivyo Dhahabu ina matumizi makubwa sana!
Magadi kazi yake siyo kupikia ndugu yangu hizi ni chemicals kama umesoma Kemia ya form II nafikiri magadi ni sodium Carbonate (Na2CO3) na matumizi yake nikianza kuyaorodhesha hapa nitajaza kurasa lkn nakupa mfano sabuni za kufuilia (za unga) krb zote zinatengenzwa na Magadi soda, kwenye viwanda vya kutengeneza glass za aina mbali mbali unahitaji magadi soda, kwenye Viwanda vya kutengeneza karatasi unahitaji magadi soda, chemical industries zote zinahizaji magadi soda kwa kifupi matumizi ni mengi sana hivyo kwa kutumia tu Magadi soda Ghafi tunaweza kujenga viwanda hata ishirini TZ kwa matumizi mbali mbali na kuongeza thamani na kutoa Ajira (kwa hali ya kawaida) uhalisia wake wa kufanyika hapa kwetu hilo ni swala lingine lkn nimekwambia jinsi inavyopaswa kuwa!