Lowassa ashusha neema kwa wanaotafuta ajira

Lowassa ashusha neema kwa wanaotafuta ajira

October 18, 2010

MGOMBEA urais wa CCM, Jakaya Kikwete jana alihamishia kampeni zake jijini Dar es salaam ambako aliahidi kuwajengea wafanyabiashara ndogondogo majengo ya kufanyia shughuli zao kwenye wilaya zote, huku akiahidin chanjo ya saratani kwa wanawake.

Tayari wafanyabiashara hao wameshajengewa jengo kubwa la ghorofa pacha linaloitwa Machinga Complex ambalo liko Mtaa wa Lindi kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo ambao wameshaanza kulitumia, ingawa biashara bado haijapamba moto.

Akihutubia mkutano wa hadhara jana jijini Dar es salaam, Kikwete alisema wamachinga wataendelea kupata neema kwa kuwa atawajengea majengo mengine kama hilo lililo eneo la Karume ambalo ni kwa ajili ya wilaya.

"Hii ni ahadi yangu naitoa tena na tena... tayari tumeshapata wafadhili kutoka China ambao watatoa Sh100 bilioni za kujengea majengo hayo na kila wilaya, tutayajenga mawili," alisema Kikwete.

Kikwete alitaja maeneo ambayo yatajengwa majengo hayo kuwa ni eneo la soko la Buguruni kwa ajili ya jengo jingine la wilayani Ilala, Tazara na eneo la Temeke Stereo kwa ajili ya wilaya ya Temeke wakati wilayani Kinondoni majengo hayo yatajengwa maeneo ya Magomeni Kondoa na Mbezi Luis, akibainisha kuwa kila moja litakuwa na uwezo wa kuchukua watu 7,000.

Kwa kuangalia uywezo wa mejngo hayo matano na lile la Mtaa wa Lindi, majengo yote yataweza kuchukua wafanyabiashara 35,000 kwa wakati mmoja.

Tayari Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilishasema kuwa majengo hayo yako kwenye mpango wake na kwamba lilikuwa linasubiri maombi kutoka halmashauri za wilaya za Dar es salaam ili lipate baraka za kuendelea na mradi huo.

Kikwete, ambaye anawania kurejea Ikulu kumalizia ngwe ya pili ya miaka mitano, pia aliahidi kusimamia ugawaji wa maeneo hayo ya biashara mara baada ya kumalizika kwa ujenzi wa majengo hayo akitaka kudhibiti ubabaishaji ambao ulijitokeza kwenye jengo la Machinga Complex.

Kikwete alisema kwamba katika ugawaji wa maeneo kwenye jengo la Machinga, watu wasio na sifa walipewa nafasi kutokana na kuwa na undugu ama urafiki na wagawaji.

"Ndiyo maana ugawaji ulichelewa sana kipindi kile eneo lile la Ilala kwa kuwa niligundua kuna ujanja unaoendelea pale lakini nilisimama kidete wakapata wahusika," alisisitiza Kikwete.

Kuhusu wanawake, Kikwete aliahidi kuwa watapatiwa chanjo ya saratani nchi nzima ifikapo mwakani baada ya kuliona tatizo hilo kuwa linazidi kuwa sugu.

Alisema kwa sasa serikali inatoa chanjo kwa kutumia hospitali ya Ocean Road ili kupunguza tatizo hilo hapa nchini.
"Hili ni tatizo ambalo limeshakuwa sugu kwa kuwa saratani zipo aina tatu; kuna ya koo, matiti, na ngozi, sasa imegundulika kuwa akina mama ndio wanaopata saratani kwa kiasi kikubwa hapa nchini. Tunaanza nao mwakani kwa kutoa chanjo nchi nzima," alisema mgombea huyo.

Kikwete pia alisema kuwa katika kuboresha elimu nchini, serikali ijayo itahakikisha inatilia mkazo masomo ya sayansi na kwamba kila mwanafunzi atapata kitabu chake.

Alifafanua kwamba tayari vitabu vimeshaagizwa kwa ajili ya kutatua tatizo la upungufu wa vitabu katika shule za sekondari zenye mchepuo wa sayansi.

Kikwete pia aliahidi kujenga miundombinu kwenye eneo la Tazara wilaya Temeke ambako wafanyabiashara ndogondogo wapatao 40,000 wataweza kujenga viwanda vidogodogo.

source: KIKWETE KUJENGA 'MACHINGA COMPLEX' TANO ZAIDI DAR - Global Publishers
October 18, 2010
 
Njaa mbaya, yani unavyoongea utafikiri huyo Lowasa ndo anaanza kuja kutumikia nchi kwa mara ya kwanza, umeacha kutumia akili Mungu alizokupa unakuja kutueleza pumba, pumba ambazo zinaendeshwa kwa sababu ya njaa zako.

Lowasa ni mwanachama wa ccm, sera ndo hizohizo kila siku no changes, alishakuwa waziri wa wizara mbalimbali, alishakuwa waziri mkuu tena kwa kushinikizwa kujiuzuru na ndio waziri Mkuu pekee aliyejiuzuru kwa kashfa kubwa na kutuhumiwa tena na Kamati iliyoundwa na Bunge.

EL Kiafya hayuko vizuri, namtakia maisha mema na umri mrefu anapaswa kupumzika na kula pensheni yake taratibu, huko mnapotaka kumpeleka mtamsababishia matatizo.

YOTE NI NJAA ZENU TU

Du hii sasa imemaliza kila kitu..Jana jioni nilipata bahati ya kukutana na think tank ya Lowassa ambao ni wahadhiri wa vyuo vikuu maarufu hapa Tanzania, kama UDSM, Mzumbe, IFM, SUA, CBE na Tumaini.

Kikubwa kilichonifanya kuona hii kambi ni noma na hatari, ni sera mbali mbali zilizo kwenye maandalizi na jana walikuwa wanaangalia tatizo la ajira kwa ujumla.

Katika hilo Lowassa aliahidi kuwa, akiingia magogoni kila mwezi atakuwa anatoa allowance (kaela kadogo), kwa vijana ambao hawana kazi, na kwa awamu ya kwanza ataanza na waliomaliza vyuo ili waweze kupata ela japo ya kutoa photocopy na chakula ili waweze kuwa na nguvu za kufanya application na ili wawe fiti kufanya kazi katika viwanda vitakavyooanzishwa.

Kisha ataangalia utaratibu gani wa kutoa kwa wengine pia alizidi kusisitiza kuwa gesi ikitumika vizuri hakuna kisichowezekana katika hili na hiyo gesi ni neema kubwa sana kama itatumika vizuri.

Moja wa wajumbe katika kutetea hoja hii ya Lowassa, alitoa mfano wa libya enzi za Gadafi, ambapo wanafunzi waliokuwa wanamaliza vyuo walikuwa wanapata allowance za kusogeza maisha yao huku wakisubiri kupata kazi za kudumu na sio miujiza ni mafuta tu ndio iliweza kufanya haya yote, hivyo basi ni wazi katika mpango huu vijana mumeombwa kuendeleza mjadala na kuchangia mjadala na kuona ni namna gani uweze kuboreshwa kwa faida ya Taifa.

NB: Kwa hakika mimi kama kijana nasema asilimia 100% nimepokea hizi jitiada za Lowassa kwa furaha zaidi na zaidi, kwani kama kijana hili tatizo limekuwa ni janga na bomu sio tu litakalolipuka bali ambalo limeshalipuka (rejea interview ya Uhamiaji, watu 16000 kwa nafasi 70).

Ebu fikiria kijana katoka familia maskini, kamaliza chuo, ajira ni isuues, hana mahali pa kuishi hapa mjini, na kama ana mahali pa kuishi chakula ni tatizo, na kama hivyo vyote vipo basi ela ya photocopy ni issues.

Basi tunakushukuru Lowassa kwa kuona hili, sisi kama vijana hatuna la kukulipa zaidi ya kusema tuko na wewe katika harakati zako, umeonyesha wewe ni kiongozi wa namna gani, unauwezo wa kuthubutu, katika hili umethubutu kueleza vission yako yenye uamuzi mgumu sana sana, Baba tuko na wewe pamoja daima, na kamwe hatutakutupa mpaka mwisho.


 
Rafiki yangu, charity begins at home. Wizarani kwenu mmetenga 1.2b kwa ajili ya chai, wewe kwa njia moja au nyigine ulihusika katika kuandaa hiyo budget na unaitumia kwa njia moja wapo. Ulifanya nini ku convince wenzako wizarani kukataa?Wizarani kwenu hamna watu wanaodai?
 
Mafisadi Kama wewe na kna makonda mnamuogopa lowasa cz mnamchafuaga na mnajua akshka nchi atawanyoosha mpaka mrudshe pesa za ghadafi na mafuta wanayouza na kula pesa za ewura na iptl...pia atakomesha biashara yenu ya sembe
Wewe ni msukule wa Lowasa tu.Mwambie arudishe fedha za Richmond.Kama Nyerere alimwita Lowasa fisadi,wewe msukule wake unalalamika nini? Kwa taarifa yako Lowasa hawezi kuwa Rais wa nchi hii hata angefanyaje.Ana laana ya Nyerere huyu.
 
Hakuna kitu kama hiki banaaa!!!! Sasa hivi kulipa mishahara tu kunawashinda wataweza kulipa allowances!!!!! Tafakari kwa kina chukua hatua muafaka

Nafkiri hapa hujaelewa hoja mkuu....hawa vijana watakuwa wanapewa allowance katika kipindi kigumu cha kutafuta ajira, which means hili swala ni katika kipindi cha mpito... at the same time uchumi utakuwa unazidi kukuwa kwa kasi, tena ukuwaji utakuwa ni wa kugusa wananchi wa hali ya chini (Economic growth will definitely reduce poverty), sio hali ya sasa ambapo economic growth ipo ila bado kuna idadi kubwa ya walalahoi.....ndio mana agenda zake kuu ni kwenye viwanda vikubwa na vidogo vidogo, elimu na kilimo.
 
Duh! hii kali sijapata kuona! allowance ya photocopy kwa ajili ya application? hivi hao wasomi kawatoa wapi lowasa? kweli TZ tuna wasomi!
 
Acheni kuleta mada za kufikirika humu,huduma tu za jamii zimewashinda wanaongea vitu vigumu kabisa,bajeri ya serikali wanategemea wahisani.
 
Kwa upeo wako unafikiri unaweza kutatua matatizo ya Ardhi kwa mwaka moja na nusu aliyokaa, (Then nimekusoma vizuri kuwa alianzisha mpango, du kumbe jamaa ni noma aliweza kuanzisha mpango unazidi kutoa tu credit kwa jamaa, nilikuwa sijui hili kuwa alianzisha mpango wa kutatua Ardhi, basi take a promise kuwa akiingia 2015 tatizo la ardhi litakuwa historia kama tatizo la watoto wa masikini wa vijijini kupata access ya shule ilivyo historia saizi kwa juhudi za Edo boy)

kaka ebu jiongeze kidogo aisee usidhalilishe upeo wako.......hakuna swala lililo tite sio tu Tanzania bali ulimwengu wote kama issue ya Ardhi angalia Africa nchi nying are in chaos kutokana na maswala ya Ardhi, angalia mashariki ya kati....jiongeze kdg kamanda...Land management and solving needs allot of time...

Huyo hafai kabisa hata umtetee vipi, ni Mtanzania mgonjwa ambae atamchagua huyo ni mgonjwa mwenzake.

Lakini uelewe kuwa, ikiwa atapita kura za maoni za CCM na alichaguliwa kuwa ndiye mgombea Urais wa CCM, mimi ntamuunga mkono. Kwa sasa nope.
 
Hii nchi ya wawaza posho na allowance tuu


Sent from my iPhone 5 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom