Lowassa apigwa shinikizo kali

Lowassa apigwa shinikizo kali

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

Lowasa-24July2015.jpg

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa


Kwa ufupi
Washirika wake wataka maamuzi sasa, Mkewe, Rostam Aziz wadaiwa kumzuia.


Shinikizo dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, la kumtaka akihame Chama Cha Mapinduzi (CCM) linazidi kuongezeka na katika timu yake ya ndani ni watu wawili tu wanaonekana kumtaka abakie ndani ya chama hicho.

Habari za ndani ya vikao vya kujadili hatua za kuchukuliwa na Lowassa baada ya jina lake kukatwa kwenye mchakato wa kugombea urais kupitia CCM, zinasema kuwa wandani wake wanaamini kuwa hana atakachopata kama ataendelea kubaki kwenye chama hicho tawala.

"Kaka sikiliza, inavyoelekea shinikizo dhidi ya Lowassa ni kubwa sana. Watu wake wa ndani wanataka aondoke CCM. Wanaona kama amedhalilishwa mno," kilisema chanzo chetu ndani ya vikao hivyo.

Chanzo hicho kilichoomba kutokutajwa jina kwa sasa, kilisema kuwa watu wake wa ndani wanaamini Lowassa akiendelea kubaki CCM atakuwa amewavunja moyo wale wote waliompigania, hasa vijana waliojaa matumaini ya kumuona akiongoza taifa hili.

Wandani wa Lowassa wanaamini kuwa kama akiamua kujiunga na chama chenye nguvu cha upinzani anaweza kutimiza ndoto yake ya kuwatumikia Watanzania kama rais wa awamu ya tano.

Chanzo chetu kinasema kuwa Lowassa mwenyewe amekwisha kuamua kufanya uamuzi mgumu, ila kuna msuguano juu ya namna ya kuondoka CCM.

Taarifa zaidi zinasema kuwa watu wawili katika timu ya ndani ya Lowassa ndio wanaelekea kuwa na mawazo tofauti. Hawa ni Rostam Aziz, mwanasiasa na mfanyabiashara mashuhuri nchini na mtu mwingine anayetofautiana na mkakati huu mpya wa kung'oka CCM ni mkewe, Mama Regina Lowassa.

Chanzo chetu kinasema kuwa wawili hao wanaamini mapigo ambayo Lowassa amekumbana nayo ni mengi na yanatosha, kwa maana hiyo ingefaa tu apumzike.

"Sijui ni kwa nini RA (Rostam Aziz) anakuwa skeptical (shaka). Si unakumbuka ndiye aliyesema amechoshwa na siasa uchwara... sasa sijui kwa nini anapunguza makali," chanzo kilisema.

Hata hivyo, vyanzo vyetu vinaongeza kuwa pamoja na upinzani huo Lowassa anadaiwa kuwa amekwisha kuamua na kinachosubiriwa sasa ni muda tu wa kutamka anakokwenda.

Wakati hali ikiwa hivyo ndani ya kambi ya Lowassa, kuna taarifa za kuaminika kuwa kumekuwa na mashauriano baina ya watu wake na viongozi waandamizi wa kambi ya upinzani juu ya mwelekeo wake wa kisiasa.

Mwandani mwingine katika kambi ya Lowassa alisema kimsingi yeye (Lowassa) amekwisha kuamua, anachofanya ni kuona kwamba watu wake wa karibu hawadhuriki na uamuzi wake huo.

Chanzo hicho kiliiambia NIPASHE kuwa wenye msimamo mkali katika kambi ya Lowassa wanaamini utabiri wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuwa upinzani utatoka ndani ya CCM utatimia mwaka huu.

"Mnakumbuka ya Mrema (Augustino) alipoondoka CCM siasa za Tanzania zilibadilika mpaka leo? Sasa safari hii ni zaidi," alisema.

Takriban wiki mbili sasa, Lowassa amekuwa na jambo kubwa moyoni analitaka kuwaambia Watanzania.

Mara ya kwanza alikuwa afanye mkutano na waandishi wa habari Julai 13 mwaka huu mjini Dodoma majira ya asubuhi, lakini mkutano huo ukahamishiwa Dar es Salaam ambako pia ukaahirishwa kwa muda usiojulikana.
Tangu wakati huo kumekuwa na tetesi kuwa alikuwa atangaze kujiondoa CCM.


Lowassa ni miongoni mwa makada 38 waliojitosa kuwania kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi ya urais wa CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu. Hata hivyo, jina lake halikuwamo katika orodha ya makada watano waliopitishwa kwenye vikao vya juu vya chama hicho ambavyo mwishowe vilimteua John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais atakayekabiliana na wagombea wa upinzani katika uchaguzi mkuu huo.

CHANZO: NIPASHE
 
Akitoka ndani ya CCM hata maisha yake siyo mbali kufika mwisho.
Halafu mimi sielewi kama walikuwa 38 akachaguliwa mmoja mbona hao wengine wote wameamua kukijenga chama chao hata kama kinaonekana kuwa na Siha mbaya mbele ya Hadhira?

Yeye ana kitu gani cha pekee alichonacho asichoweza kumshauri Magufuli kama ni kizuri kikafanyiwa kazi?mpaka atake kuingia ikulu mwenyewe?

Sasa ndiyo naelekea kuamini kuna kitu kimejificha moyo mwa Lowasa na siyo kizuri kwa Watanzania Lowasa atatugharimu.

Mtu mmoja alisema kuwa "Sumu hainjwi"ila huyu jamaa akihama na kwenda Upinza halafu Watanzania tukamchagua kuwa raisi tutakuwa tumeonja Sumu na kiukweli ukionja Sumu kuna matokeo ya kufa tu na utakufa tu maana hamna namna nyingine.
 
Kama sio Hofu "Ebu tupia Hints na Ushahidi wa ufisadi wa Eddo Lowassa, ambao Unadhani Walioko CCM ni Wasafi. Jiongeze ndg yangu

ndani ya CCM Hakuna kitu kiitwacho Rushwa bali Takrima. Hakuna Msafi ndani ya CCM, Hiyo Tuhuma ya Richmond Haina Uhalisia na

Serikali nzima Ilikuja Kujua Tayari Imeingizwa Mjini.
 
Mzee Lowasa kama mzee wangu tuna toka njia moja nina kushauri achana na kuhama chama maana kwa hakika hutofanikiwa sana sana unajiandalia matatizo ambayo hata dkt wakukutibu hatokuwepo at that time.
kwa nini na sema hivyo nasema hivyo kwakuwa ukweli unaujuwa na mfumo wa serikali unaujuwa na kamwe serikali haiwezi kutengeneza watu wakushindana nayo sana sana nikukutengenzea zengwe zaidi ya lile la kwanza
1. Hafai
2. Hafai
3.Hafai
4 Hafai na NIMTU HATARI KTK SERIKALI
5.?
Soma vitabu vyote nasasa ni zaidi ya miaka hamsini ya uhuru wetu ni nani alie wahi kupingana na serikali akafanikiwa ukimpata nijuze nifute kauli
Nikupe mfano mdogo tu Mh Mrema yupo wapi mtu alie tikisa taifa hili kila mtu akajuwa hakuna kama mrema yupo wapi yupo wapi wapo wapi maadui wa ccm ndani ya ccm? achana na hii habari kuwa mpole Mungu akupenda utawale hili taifa na wala sio Kikwete maana hata Kikwete hakujuwa vile atakuwa rais ila ilijulikana atakuwa rais kama ilivyojulikana hutokuwa rais.
Simama na utafakari na uone maamuzi yako ni kiza kinene kwa familia yako na watu wako na ni jambo la busara kuwa mjinga nakuendelea kumuunga mkono mgombea alie pitishwa maana mwisho wa yote nilazima utahadhirika kias napata shida kama atakuwepo dkt wakukutibu madhara utakayo yapata.
Mungu anaupima utii wako ktk hili kabla ajashuka nakukwambia kwa makofi sikukuchaguwa wewe!!!!!
 
Kama sio Hofu "Ebu tupia Hints na Ushahidi wa ufisadi wa Eddo Lowassa, ambao Unadhani Walioko CCM ni Wasafi. Jiongeze ndg yangu

ndani ya CCM Hakuna kitu kiitwacho Rushwa bali Takrima. Hakuna Msafi ndani ya CCM, Hiyo Tuhuma ya Richmond Haina Uhalisia na

Serikali nzima Ilikuja Kujua Tayari Imeingizwa Mjini.


Lowassa ameshindwa kutambua kuwa watu wanamsukuma kwa sababu ya maslahi yao binafsi? Lowassa alikatwa mwaka 1995, mwaka 2005 akaunda mtandao ambao ulisambaratika miaka mitatu baadae (2008) ambapo alilazimika kujiuzulu. Sasa leo hii anapata wapi ujasiri wa kushinikiza kuwa anafaa kuongoza watu waliomkaa, kipi kimebalika kwenye kabati la Lowassa? Inajulikana kuwa watu wanaweweseka mjini kwa sababu Lowassa aliwapa pesa na kuwaahidi vyeo, sasa wanataka kumtoa kafara ili waneemeke! Ukiishi kwa upanga, utakufa kwa upanga!
 
Kweli kabisa kwani na sisi wana UKAWA tutawauliza kuwa mmemchagua
kwa vigezo vipi. Ikizingatiwa kuwa ALIISHA KATWA mahala flani hivi hapa mjini.
na CHADEMA ikijiroga kumchukua na kumsimamisha babu mamvi ntachana chana kadi yao.
kama akija huku kwetu inabidi awe "common man" tu kwa miaka isiyopungua 5 tukimuweka
under probation mpaka tujiridhishe juu ya maisha yake mapya.
 
mwacheni aende cdm. maana mz lowasa ana kipaji cha kupiga kampeni na kufadhiri..

lkn sio ktk nafasi ya uraisi.
 
Roryo achana na wenye akili za kuvuta na kamba
 
Akitoka ndani ya CCM hata maisha yake siyo mbali kufika mwisho.
Halafu mimi sielewi kama walikuwa 38 akachaguliwa mmoja mbona hao wengine wote wameamua kukijenga chama chao hata kama kinaonekana kuwa na Siha mbaya mbele ya Hadhira?

Yeye ana kitu gani cha pekee alichonacho asichoweza kumshauri Magufuli kama ni kizuri kikafanyiwa kazi?mpaka atake kuingia ikulu mwenyewe?

Sasa ndiyo naelekea kuamini kuna kitu kimejificha moyo mwa Lowasa na siyo kizuri kwa Watanzania Lowasa atatugharimu.

Mtu mmoja alisema kuwa "Sumu hainjwi"ila huyu jamaa akihama na kwenda Upinza halafu Watanzania tukamchagua kuwa raisi tutakuwa tumeonja Sumu na kiukweli ukionja Sumu kuna matokeo ya kufa tu na utakufa tu maana hamna namna nyingine.

Kwani yeye magufuli ana nini hicho kwa nini asimwachie lowasssa tu? Acha ujinga wewe. Lowassa anavision na vision kwa taharifa yako ni some form of energy ambayo mtu anakuwanayo...haiwezi kuktoka hivi hivi na haswaa ndo inayotoa msukumo. Kwa mtazamo wangu energy na msukumo aliokuwa nao lowassa ni mkubwa sana kuliko magufuli. Ukitaka kupima angalia hamasa na mihamko ya watu katika kila kona....ni lowasa lowasa.. upinzania..uraisi. Huu msikii yeboyebo kabisa akitajwa. It s just natural so usiumie. Watu wanataka kile kitu kinacho wastimulate bwana ...magufuli hapana..BIG NO!
 
YALE YALIKUA YAKISUBIRIWA KWA HAMU YAMETIMIA!!! EDWARD LOWASSA SASA RASMI UKAWA

BAADA ya vuta nikuvute katika vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kuhusu kukubaliwa au kutokubaliwa kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa kujiunga na umoja huo ili kuongeza nguvu ya kisiasa, hatimaye mwanasiasa huyo maarufu nchini amekubaliwa na tayari amejiunga rasmi Ukawa akiwa mwanachama halisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imefahamika.​

Taarifa rasmi kutoka Ukawa na kwa msemaji wa Lowassa ambaye hakutaka jina lake litajwe, imeeleza kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya majadiliano ya kina katika Mkutano Mkuu wa Ukawa uliofanyika mapema wiki hii huku ajenda kubwa ikiwa ni kumpokea Lowassa ili kuimarisha kambi ya upinzani ikiwa ni pamoja na kumsimamisha kama mgombea urais wa umoja huo.
Taarifa rasmi zilizolifikia gazeti hili zimeeleza kuwa Lowassa anatarajiwa kutangazwa rasmi Jumapili hii hivyo maadalizi ya mkutano mkubwa wa aina yake yanaendelea. Chanzo chetu kutoka katika mkutano huo kilisema kwa moyo mmoja, wenyeviti wa vyama vyote vinavyounda umoja huo, yaani Freeman Mbowe (Chadema), ProfesaIbrahim Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCRMageuzi) na Emmanuel Makaidi (NLD), wameridhia kuungana na Lowassa katika safari yao ya kuking’oa CCM madarakani huku wakiamini kuwa wakimsimamisha kuwa mgombea wa Ukawa watafanikisha azma ya vyama vya upinzani kuingia ikulu.
“Katika kikao chetu tulijadili mikakati kadhaa ya kuchukua dola lakini kubwa zaidi lilikuwa ni jinsi ya kuungana na Lowassa ili kutimiza azma hiyo, ikizingatiwa kwamba hivi sasa anaungwa mkono na Watanzania wengi na hasa jinsi ambavyo hawakuridhishwa na mchakato wa kumuengua kuwania urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo tuna uhakika kwa mkakati huu lazima tuking’oe CCM madarakani,” alisema mjumbe mmoja wa Mkutano Mkuu (jina limehifadhiwa).

TUNDU LISSU AFUNGUKA
Akizungumzia suala hilo, Mnadhimu Mkuu wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, aliliambia gazeti hili kuwa majadiliano kuhusu Lowassa yalikuwa ya lazima kwa kuwa katika muungano wa vyama kila kiongozi ana mtazamo wake hivyo, kila jambo la muhimu lazima lifanyike kwa majadiliano ili kufikia mwafaka kwani lengo ni kuhakikisha kwamba kunakuwapo na mkakati wa pamoja kuhakikisha kuwa CCM kinag’olewa madarakani ili makada wa chama hicho waelewe kuwa sasa Watanzania wanahitaji mabadiliko na si maneno matupu ya majukwaani.
LIPUMBA NAYE ANENA
Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba alisema kwamba Ukawa hivi sasa wamejipanga kimkakati kuhakikisha wanachukua dola na kuongeza kwamba waliokuwa wakieneza propaganda kuwa anawakwamisha wataendelea kuumbuka kwa kuwa vyama vyote vinavyounda Ukawa ni kitu kimoja.
Aliongeza kwamba, kamwe umoja huo hauwezi kusambaratika kwani ajenda kuu ni kuindoa CCM madarakani na kuongeza kwamba, mambo mengine kama mgawanyo wa ruzuku yatafuata baadaye kwani yanazungumzika katika ngazi ya uongozi.
MSIMAMO WA LOWASSA
Msemaji wa Lowassa ambaye kawa sasa ndiye gumzo la taifa ukiachana na Dk. John Magufuli aliyepitishwa na CCM kuwania kiti cha urais amelihakikishia gazeti hili kuwa Lowassa ameamua kuingia Ukawa ili kuendeleza siasa za kistaarabu kutimiza azma yake ya Safari ya Matumaini kama ambavyo amekuwa akiwaahidi Watanzania.
Alisema ameamua kuungana na Ukawa kwa kuwa anaamini kuwa lengo la vyama vyote vya siasa ni kuhakikisha vinatimiza malengo yao ya kuwahudumia wananchi, hivyo inapotokea katika chama kimojawapo, bado kuna nafasi ya kutumia vyama vingine kutimiza malengo ya kisiasa. Msemaji huyo aliongeza kwamba baada ya kuenguliwa alikuwa na kazi ngumu ya kubaini nini cha kufanya ili kutimiza azma yake ya kisiasa, ndiyo maana alikaa kimya ili kuepusha mivutano kati yake na CCM lakini hakuwa amekata tama kuhusu jinsi anavyoweza kuwakomboa Watanzania kutoka katika dimbwi la umaskini, jambo ambalo alikuwa akiwaeleza katika safari yake ya kusaka wadhamini nchi nzima.

MKAKATI WA KAMPENI
Msemaji huyo alisema kuwa akiwa katika Ukawa, Lowassa ameandaa mkakati kabambe wa uhamasishaji wananchi ili watambue kwamba azma ya kuwakomboa ipo palepale na kuongeza kuwa ana uhakika watamuunga mkono kwani anatambua kwamba wapo pamoja naye katika safari ya matumaini.
Alisema kwamba kazi iliyo mbele yake ni kuhakikisha kuwa anaisuka upya ‘Team Lowassa’ na atakuwa makini na baadhi ya watu waliomsaliti ili wasiharibu mkakati wake na kuongeza kwamba watazunguka nchi nzima kufanya kampeni za kistaarabu, zisizokashfu wanasiasa wengine ili wananchi wapime ni kiongozi gani anafaa kati ya yeye na wengine.

TATHMINI YA USHINDI
Chanzo chetu ndani ya Ukawa kilieleza kwamba, tathmini iliyofanywa hadi sasa inawapa uhakika wa kuchukua dola kwani katika maeneo mengi, Lowassa anaungwa mkono zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote yule. Kilisema kuwa katikamaeneo mengi CCM haikubaliki kutokana na kuendesha siasa za kibabe na mizengwe, jambo ambalo limekuwa likiwakera wananchi kwani kinachotokea ni kwamba wanachaguliwa viongozi badala ya wao kuchagua viongozi wanaowataka.
Kilisema Lowassa ana nguvu zaidi katika Mikoa ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa, Kusini, Nyanda za Juu Kusini na Zanzibar hivyo CCM kama inataka kushindana naye ijipange vyema.

ZITTO AJUMUISHWA
Katika mkakati huo wa ushindi, inaelezwa kwamba, umoja huo utamjumuisha kundini Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye chama chake nacho kitaongeza nguvu ya ushindi.
Lowassa alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM kati ya wagombea 38 ambao walichukua fomu lakini jina lake lilikatwa katika kikao cha Kamati ya Maadili na Usalama ya CCM, jambo ambalo lilizua sintofahamu miongoni mwa wanasiasa wengi waliokuwa wakimuunga mkono, hatua ambayo ilisababisha mtikisiko wa kisiasa nchini.
 
Lowassa ameshindwa kutambua kuwa watu wanamsukuma kwa sababu ya maslahi yao binafsi? Lowassa alikatwa mwaka 1995, mwaka 2005 akaunda mtandao ambao ulisambaratika miaka mitatu baadae (2008) ambapo alilazimika kujiuzulu. Sasa leo hii anapata wapi ujasiri wa kushinikiza kuwa anafaa kuongoza watu waliomkaa, kipi kimebalika kwenye kabati la Lowassa? Inajulikana kuwa watu wanaweweseka mjini kwa sababu Lowassa aliwapa pesa na kuwaahidi vyeo, sasa wanataka kumtoa kafara ili waneemeke! Ukiishi kwa upanga, utakufa kwa upanga!


Lowassa ni kiongozi bora na mwenye mvuto mkubwa kwa sasa katika siasa za tanzania. Maamuzi yeyote atakayochukua yatakiathiri sana ccm na pengine kukiongezea majeraa zaidi ya iliyonayo sasa na itakayoyapata baada ya uchaguzi. Hili magufuli hana uzoefu nalo na hata liweza labda baada ya miaka mitano au sita.

Kura yangu bado inabaki kwa lowassa na kama siyo lowasa basi dr slaaa. Hao wengine nitafikiria
 
Magazetini

ajihadhari sana na rostam..kweli alikywa nae ukweli halisi alitumwa kundini nawajanja kuja kumharibia..note.enl huyu jamaa ulishakorifishana nae toka alipopelekewa hellicoter kubebwa mzobemzobe kwa makosa aliyokufanyia..sikuamini amerudi tena wazo tu.sio mtymzuri kwako

kuhusu mama unamaamuzi yakumsikiliza ama lah kwakymwelekeza manufaa yakuhama na madhara yakubaki ccm hope ataelewa
 
Last edited by a moderator:
Tangu wamkata jina mapema huyu Mtu abakia kuwa na nguvu tena nathubutu kusema ndio kwanza nguvu zake zimeongezeka zaidi na ile hali ya kukubalika kwa Wananchi ndio inajidhihirisha zaidi kuliko Mwanasiasa awaye yote ndani ya CCM.

CCM wanajuta!!! kwanini waliamua ovyo kiasi hicho,wanahaha kusikia LOWASSA aweza hamia CHADEMA/UKAWA.Ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI hali sio shwari wamebaki kutupiana lawama.Lakini pamoja na hayo yote,Inaonekana kila kitu kinaharibika upande wa CCM,vichwa vyao vinauma,Walidhania kulikata jina la LOWASSA lisiingie hata kwenye tano bora huko ndio kuyazuia Mafuriko kwa Mkono.Mbaya zaidi hawataki kusikia LAIGWANANI aweza kutua CHADEMA.

Ni hatari zaidi ikitimia kweli ikawa hivyo ndivyo ilivyo EDWARD LOWASSA kuhamia upinzani,ENYI MACCM hamkuliwaza hilo???
Je! Litabakia jiwe juu ya jiwe huko CCM?
Hamkujua kuwa anakubalika na kupendwa sana na wengi ndani na nje ya ccm?

Siasa za kweli hazina adui wala ndugu wa Kudumu,sio ajabu Laigwanan kupokelewa UKAWA,Ukizingatia Intelejensia ya CHADEMA iko juu sana kuliko ya CCM,Siku zote wamewazidi kete kwa mambo ya Msingi ccm hukosa point lakini chadema huonyesha njia ama majawabu kwa UMMA wa WATANZANIA.Maana yake CHADEMA wanajua vizuri sana Lowassa sio FISADI vile,ila kwa kuwa alikuwa kwenye Mfumo mbovu ilipendeza kwa wakati huo kumjumuisha na Magamba yote.

Ni shauku yangu kubwa kusikia EDWARD NGOYAI LOWASSA KAHAMIA RASMI CHADEMAUKAWA.
Najua wabaya wake hamtaki nisema maneno haya.
Ila Lugha hii inasound vizuri sana kwa wapenda mabadiliko.

JARIBU KUFIKIRI KIDOGO

Chadema wamekuwa na mikakati mikali sana na hakika wamejiandaa vema kuiongoza Nchi hii,I SEE THE NEW COUNTRY WAS CAME IN OCTOBER 2015 AFTER ELECTION.
CHADEMA walishandaa siku mingi sana,kila kata watu mia mbili ambao hata ufanya nini kamwe hawawezi kukisaliti chama, hizo ni KURA za uhakika na bado wafurukutwa,wapambe,wakereketwa na wanachama wengine hai jumlisha UKAWA jumlisha LOWASSA kwa mtindo huo CCM haitaweza kusimama kamwe mbele ya UPINZANI.

Hata sasa pamoja na Mh.LOWASSA yuko kimya hicho kimya chake kina mshindo mkuu,Na hio inabainisha huyu mtu ni mbeba tu mpaka kesho.Hapa tulipofika ni patamu sana tena sana kilichobakia ni WANANCHI kushuhudia kuona LOWASSA akifanya Maamuzi magumu ya kuhama CCM na kuhamia CHADEMA.

WANANCHI WANAFURAHIA MABADILIKO KULIKO WAKATI WOWOTE ULE.
 
Wakuu salama
Nimekuwa nikiona post nyingi sna zinazo anzishwa na maccm zinazoishauri chadema wasimpe lowassa nafasi ya kwenye chama chao kwani wakimpa nafasi chama kitakufa,kwa akili tu ya harka haraka wala huitaji kutumia nguvu kama kweli nikweli chadema itakufa si wanyamaze kimya ili wapate ushindi??hivi unawezaje kutoa siri za ushindi wako hadharani??si wanayamaze ili lowassa atakapo simamamishwa na cdm wapite kirahisi?na toka lini ccm wakaishauri chadema mambo mazuri ya kufanya??Ccm wameona moto wa lowassa hauzimiki,ni hivi majuzi tafiti ilikuwa zikitoka utakuta ni lowassa na dr slaa wanaongoza,sasa leo unaenda kuwaweka sehem moja hivi unategemea huo moto watakao uwasha ccm watauzima??tafakari chukuwa hatua
 
Big up mkuu.
Umetoa analysis nzuri sana
Kama kweli CCM Wanaona lowassa akihamia Cdm itakufa hawakuwa na sababu ya kuanika siri zao hadharani.
Wangepiga kimya ili wapite hapo hapo
 
Chadema mwendo mdundo. Hamia Chadema ndiyo habari ya mujini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom