Mh. Laigwanan Edward Ngoyai Moringe Lowassa anastahili ulinzi wa ziada ili kumlinda na wabaya wake (CCM) kwani hawa waovu hawakawii kumfanyia kitendo cha kigaidi kama kile walichmomfanyia Horace Kolimba.Ni jambo lililo wazi kwamba CCM hawana namna nyingine ya kupambana na UKAWA zaidi ya kushiriki vitendo viovu kama hiki.
Sasa hivi Mh Lowassa ndiye adui namba moja wa CCM na waovu hawa wako tayari kufanya kila hila yoyote dhidi ya UKAWA bila kuzingatia gharama ya uovu huo.
Baada ya kumchakachua matokeo kwenye kura za maoni na kisha kushindwa kumtisha abaki CCM, kuna kila dalili CCM kufanya kitendo kiovu kwa Mh. Lowassa.
Hivyo basi, ulinzi madhubuti na makini unatakiwa kutolewa na wanaUKAWA na kila mtanzania mpenda maendeleo kwa kuwa Edo ndiye tumaini pekee kwa watanzania kujikomboa kutoka utumwa wa CCM.
Nitoe rai kwa uongozi wa UKAWA kumpa ulinzi wa ziada kiongozi huyu wa kitaifa na kimataifa ili kumlinda na kila uovu na hila za CCM. Ikiwa CCM walitupa mabomu kwenye mkutano wa siasa na kuhatarisha maisha ya raia, hawashindwi kumfanyia ugaidi kama huo kamanda Lowassa.
Lowassa ndiye mboni pekee inayowapa nuru watanzania itakayowaangazia na hatimaye kuwawezesha kutoka msitu wa giza nene (CCM) ambamo wamekuwa wakiogelea tangu enzi na enzi.
Ni jambo la kawaida kwa CCM kucheza rafu ya aina yoyote, bila kujali madhara kwa mhusika au wananchi, ilmradi tu malengo yao ya kisiasa yatimie.
Kwa kuwa tuna uzoefu wa kutosha na hawa waovu, ni bora tahadhari ichukuliwe mapema kuhakikisha kwamba hawapati nafasi ya kuendeleza uovu wao.
Tafakari, chukua hatua!
:israel:
tunamsubili alichowafanya mwakyembe na mwandosya na yeye zamu yake,