Nashauri, kwa vile sasa ni rasmi Lowasa yuko Ukawa na Chadema zaidi basi haya yafanyike. Kwanza jukumu la ulinzi sasa liratibiwe na Red Brigade lote kwa ujumla wake, wale waliokuwa walinzi wake akiwa CCM wafanyiwe vetting upya na katika hilo Lowasa hatakiwi kuleta za kuleta kabisa, yeye sasa ni Property ya Chadema na Chadema wanapaswa kuilinda wao kwa kadiri watakavyo ona ni muhimu kama taasisi.
Pia kuna kundi lilikuwa linajiita "Friends of Lowasa" hilo kama lipo na linaendelea basi IWE NI MARUFUKU KULIINGIZA KATIKA RATIBA ZA CHAMA AU KULITAMBUA RASMI. Hilo liendelee na kazi zake lakini nje ya mfumo wa chama maana chama kisipoangalia kundi hilo linaweza kufanya madudu yake na yakakigharimu chama kwa gharama kubwa.
Jambo jingine ni kuhusu kuihusisha familia katika kampeni. Hapo ni mama Regina tuu anayepaswa kuonekana anahusishwa na kampeni za mgombea wetu, hatutaki sijui huyu MTOTO wake mara huyu sijui nani wake, hayo mambo ni ya huko ccm pekee. Hivyo kama kuna Mtoto ( yupo mmoja nasikia kule CCM kahusika sana) tafadhali akae mbali akiachie chama kiratibu mambo yake, hatukumsimamisha Lowasa kugombea Uchifu bali Urais.