Lowassa aongezewe ulinzi

Lowassa aongezewe ulinzi

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,985
Reaction score
25,375
Mh. Laigwanan Edward Ngoyai Moringe Lowassa anastahili ulinzi wa ziada ili kumlinda na wabaya wake (CCM) kwani hawa waovu hawakawii kumfanyia kitendo cha kigaidi kama kile walichmomfanyia Horace Kolimba.Ni jambo lililo wazi kwamba CCM hawana namna nyingine ya kupambana na UKAWA zaidi ya kushiriki vitendo viovu kama hiki.

Sasa hivi Mh Lowassa ndiye adui namba moja wa CCM na waovu hawa wako tayari kufanya kila hila yoyote dhidi ya UKAWA bila kuzingatia gharama ya uovu huo.

Baada ya kumchakachua matokeo kwenye kura za maoni na kisha kushindwa kumtisha abaki CCM, kuna kila dalili CCM kufanya kitendo kiovu kwa Mh. Lowassa.

Hivyo basi, ulinzi madhubuti na makini unatakiwa kutolewa na wanaUKAWA na kila mtanzania mpenda maendeleo kwa kuwa Edo ndiye tumaini pekee kwa watanzania kujikomboa kutoka utumwa wa CCM.

Nitoe rai kwa uongozi wa UKAWA kumpa ulinzi wa ziada kiongozi huyu wa kitaifa na kimataifa ili kumlinda na kila uovu na hila za CCM. Ikiwa CCM walitupa mabomu kwenye mkutano wa siasa na kuhatarisha maisha ya raia, hawashindwi kumfanyia ugaidi kama huo kamanda Lowassa.

Lowassa ndiye mboni pekee inayowapa nuru watanzania itakayowaangazia na hatimaye kuwawezesha kutoka msitu wa giza nene (CCM) ambamo wamekuwa wakiogelea tangu enzi na enzi.

Ni jambo la kawaida kwa CCM kucheza rafu ya aina yoyote, bila kujali madhara kwa mhusika au wananchi, ilmradi tu malengo yao ya kisiasa yatimie.

Kwa kuwa tuna uzoefu wa kutosha na hawa waovu, ni bora tahadhari ichukuliwe mapema kuhakikisha kwamba hawapati nafasi ya kuendeleza uovu wao.

Tafakari, chukua hatua!

:israel:
 
Ile thread ya familia ya Lowassa kuchunguzwa Uingereza imeondolewa.? Kusema kwamba kuna mtu anatishia maisha yake Lowassa wakati wale ni Crime Family,that is an insult.
 
Aongezewe au abadilishiwe? Mbona nimeona bado analindwa na yule Mlinzi wake wa usalama wa taifa Bwana Tendewa.
 
we una usafi gani

Mimi msafi. Kwani mimi nimefunguliwa mashtaka ya money laundering? Kwani mimi nagombea urais sasa hivi. Lowassa amesema kama kuna mjinga ana ushahidi aende mahamakani,24 hrs later mtu amekwenda mahakamani.
 
Mimi msafi. Kwani mimi nimefunguliwa mashtaka ya money laundering? Kwani mimi nagombea urais sasa hivi. Lowassa amesema kama kuna mjinga ana ushahidi aende mahamakani,24 hrs later mtu amekwenda mahakamani.

Wewe jamaa njaa inakusumbua, badala ya kuifungulia mashtaka hii familia ya kwanza inayomiliki Simba Trust mnahangaika na mtu aliyekuwa nje ya system yenu ya kifisadi kwa miaka saba. Zile fedha za escrow kupitia stanbic bank statement yake imefichwa na wanafiki kama wewe wanaojaribu kujenga picha ouwa Lowassa ni fisadi huku wao wanakwapua bila huruma. Go to hell
 
Redbrigedi wawepo kama 100 kila anapotembea security group compony 200 mzizi wa fitina uishe
 
Mimi msafi. Kwani mimi nimefunguliwa mashtaka ya money laundering? Kwani mimi nagombea urais sasa hivi. Lowassa amesema kama kuna mjinga ana ushahidi aende mahamakani,24 hrs later mtu amekwenda mahakamani.

Kwani kutokugombea urais ndo kunafanya mtu awe msafi? Mtu kwenda mahakamani haimaanishi mtuhumiwa ni guilty. Wazungu wanasema a suspect is innocent until proven guilty.
 
Kweli usiopingika lowasa ndye mkombozi wa taifa letu kwasasa kutoka kwa mafisadi ccm, anasitahili kulindwa kwa nguvu zote kwani hawa jamaa wamebanwa sio wakuamin hata kidogo...
 
Naomba tuaminiane kama watanzania tusijenge woga na hofu katika maisha yetu. Tumtangulize Mungu kwa kila tufanyalo, na sidhani tumekuwa mashetani kiasi cha kutafuta roho za wengine kwa sababu ya kutafuta madaraka. Tuwaache wananchi wamchague wanayempenda hapo taifa litakuwa limepata tiba!
 
Kwanza nilazima ulimwe, kisha upuliziwe dawa nakupaliliwa ukisha maliza hapo tunakuvuna nakukuwekea dawa yakuku ifadhi, kisha tunakuchambuwa nakupeleka sampo tbs tayari kwa kibali cha mlaji. Sasa ikishindikana hapo lazima ukatwe tangu shambani. Kwa bwana Lowasa alikatwa tangu shambani baada yakujilikana yeye alikuwa ni uyoga wenye sumu kali katikati ya uyoga mzuri.
 
Back
Top Bottom