Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Ndo tayari, labda usubiri magazeti yaipambe ili ipendeze kusomeka na kukupa raha ya kusoma ila aliyoongea ndo hayo!
Mi nahisi alikuwa ana jambo kuubwa la kuongea, alafu katishwa asilitoe ilhali kishawaambia wanahabari waende wakamsikilize hivyo imemuwia vigumu kusitisha akaona japo aseme lolote.
 
Kama Yale maswali ya msingi hana majibu yake,palikuwa na haja gani kuwaita waandishi Wa habari!?Si angesubiria tu akiandikwa vibaya aende mahakamani moja kwa moja kuliko kuwachimba waandishi mkwara?
 
...nadhani huyu mzee anatapatapa tu, maana inavyoonekana anataka awafurahishe akina Nape ili wamsamehe asijivue gamba. Maana kauli zake zinakinzana na yaliyo moyoni mwake, huyu mzee alikuwa na kampeni b4 kuachia uwaziri mkuu ya kuhakikisha anagain popularity miongoni mwa wapiga kura wa nec, ila akastukiwa!!
 
Nadhani kuna kitu kazuiliwa. Alikuwa kishakaa ili aanze kuongea mapema, akaondoka ghafla. Yawezekana alipigiwa simu na kupewa maelekezo tofauti? Matarajio ya wengi yalikuwa aongelee masuala mengi, Richmond/Dowans, hali ya usalama a nchi, afya yake (baada ya kudaiwa kuwa alikuwa nje kwa matibabu) n.k

Alichofanya kimenishangaza, not expected at all

Nilitegemea Kuna kipya ambacho atazungumzia, Sijafanya kazi zangu kwaajili ya kufuatilia hii thread ila mwisho nimeambulia patupu. Shame on You Lowasa.
 
Kwa nini hajajibu suala la dowans!
Well,

Pamoja na mwandishi wetu kumweleza umuhimu wa yeye kuongelea suala la DOWANS/Richmond kakataa katakata na kusema ataliongelea wakati muafaka na si leo.
 
Alisema atatoa yaliyoko moyoni mbona sijayaona kwani yote aliyosema kila mtu anayajua na hakuna jipya. Hivi anafikiri urais unapatikana kirahisi hivi? Kama anataka kujua jinsi mind set za waTZ kuanzia mijini hadi vijijini zilivyobadilika asubiri 2015. Kama hajajiandaa kama walivyoshauriwa na Mh. Jaji Joseph Sinde Warioba basi asubiri kupata stroke 2015
Kweli hakuna jipya, tofauti kabisa na nilivyotegemea!
 
fisadi fisadi tu hana jipya la kusema.

Ccm ina wenyewe bwana.

Samaki ana nguvu akiwa ndani ya maji, hakitolewa huko anakwisha kazi yake.
 
Nimewahi hudhuria mikutano ya Lowasa akiwa PM, hotuba zake hazina uzito wowote, ni pumba tu, tatizo liko kwenye vyombo vyetu vya habari ambavyo hupamba kwa kumtengenezea habari, na ndio maana siku zote huchagua waandishi wa habari kuzunguka nao. Sasa subirini kina Balile and the kibandas watakavyoiandika kesho, mliofuatilia mtazimia.
 
...nadhani huyu mzee anatapatapa tu, maana inavyoonekana anataka awafurahishe akina Nape ili wamsamehe asijivue gamba. Maana kauli zake zinakinzana na yaliyo moyoni mwake, huyu mzee alikuwa na kampeni b4 kuachia uwaziri mkuu ya kuhakikisha anagain popularity miongoni mwa wapiga kura wa nec, ila akastukiwa!!

Acha Kumkweza Nape hana Ubavu wa kupambana na Laigwan Lowasa
 
Mwandishi wetu pia kamwuliza juu ya 'Uvuaji Gamba', nalo kakataa katakata kuongelea, kasema si wakati muafaka.
 
Kama Yale maswali ya msingi hana majibu yake,palikuwa na haja gani kuwaita waandishi Wa habari!?Si angesubiria tu akiandikwa vibaya aende mahakamani moja kwa moja kuliko kuwachimba waandishi mkwara?
Kaita waandishi wa habari ili jamii itambue kumbe yupo na ana mpango wa kugombea uraisi mwaka 2015, hakuna cha maana alichoongea zaidi ya kuongelea mambo yale yale yanayojadiliwa kila siku mitaani. Inabidi ifike kipindi aachane na hizi siasa za ajabu ajabu. Mtu mzima ila vitu anavyovifanya kama vya kitoto.
 
Niliwaambieni tangu mwanzo kwamba huyu Lowassa na mkutano wake na Waandishi wa habari leo; bure kabisa, hakuna kitu pale!!

Lawassa hawezi kutuita kwa ajili tu ya kututaka kwenda kumsikiliza jinsi ambavyo ANAMUOMBA RAIS KIKWETE MSAMAAHA KWA VURUMAI ZILIZOTOKEA ARUSHA peke yake.

Ni dharau kubwa sana kwa Wa-Tanzania pindi anapochagua kuongea na wananchi wenzake bila kutuambia majibu ya msingi kabisa ya Dowans, kukosekana amani nchini kukiwa na mauaji kila pembe ya nchi ikiwemo Loliondo.

Sijamuelewa huyu bwana hata kidogo.

 
Unafiki uliopo ccm utawamamliza, mana Lowasa leo kaongea full mipasho na alikuwa anamnanga Nape na magazeti na kumsfia Kikwete kuwa hawakukutana barabarani.Kwa haya aliyoyasema leo huyu Lowasa nadhani akili yake bado anamtegemea sana Kikwete kwa uchaguzi ujao 2015.Hana jipya ni fisadi mkubwa.
 
Back
Top Bottom