Lowassa aondoke tu. Ni kauli ya vigogo wa CHADEMA

Lowassa aondoke tu. Ni kauli ya vigogo wa CHADEMA

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
1,056
Reaction score
1,086
Kauli ya aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Edward Lowassa, ya kwamba chama hicho ni cha kiharakati, inaonekana kuwakera wengi wa vigogo wakubwa ndani ya CHADEMA.

Mara kadhaa, kwa chini kwa chini na hadharani, Lowasa amekuwa akikiita CHADEMA chama cha kiharakati.

Mwanasiasa huyo ambaye katika kuusaka urais aliungwa mkońo pia na vyama vya CUF, NCCR Mageuzi na NLD, akiwa mto wa mbu, Monduli, Arusha hivi karibuni kwenye mkutano wa hadhara aliamua kupaza sauti kwa kuwaomba wananchi wa eneo hilo kumuunga mkono katika juhudi zake hizo za kutaka kukikiondoa chama chake kipya hicho kutokuwa chama cha kiharakati na kuwa chama cha siasa kwa madai ya kukiandaa kikamilifu kukamata dola mwaka 2020.

Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wetu kwa siku kadhaa sasa, umebaini kuwa kauli ya Lowassa ya kukiita chama hicho cha kiharakati kwa kiasi kikubwa inaonyesha kuwakera mno baadhi ya vigogo wahadhifina wa chama hicho kiasi cha baadhi yao kutokwa na kauli "Lowassa aondoke tu atuachie chama chetu cha kiharakati na uhanaharakati wetu".

Baadhi yao hao ,wakioneka kujawa na jazba, wamesikika wakisema: "Leo ndio amebaini CHADEMA chama cha kiharakati?

Wakati anakuja kutafuta hifadhi kwetu mwaka jana, hakuona CHADEMA wala viongozi wake kama ni wanaharakati, ila sasa?

Chanzo: Tazama
 
Chadema hawana ubavu wa kumfukuza Lowasa. Maana ile bei aliyoinunua chadema ni kubwa mno. Na leo hii ukisema warudishe hawana maana walishaigawana yote (mfano Mh. mchungaji wa iringa alipata mil 300) na sasa ukisema airudishe itakuwa majanga
 
kauli ya aliyekuwa mgombea urais wa Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Edward Lowassa, ya kwamba chama hicho ni cha kiharakati, inaone kuwakera wengi wa vigogo wakubwa ndani ya chadema.

Mara kadhaa, kwa chini kwa chini na hadharani, lowasa amekuwa akikiita cha chadema .

Mwanasiasa huyo ambaye katika kuusaka urais aliungwa mkońo pia na vyama vya Cuf, Nccr mageuzi na Nld, akiwa mto wa mbu, Monduli, Arusha hivi karibu kwenye mkutano wa hadhara aliamua kupaza sauti kwa kuwaomba wananchi wa eneo hilo kumuunga mkono katika juhudi zake hizo za kutaka kukikiondoa chama chake kipya îcho kutokuwa chama cha kiharakati na kuwa chama cha siasa kwa madai ya kukiandaa kikamilifu kukamata dola mwaka 2020.

Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wetu kwa siku kadhaa sasa, umebaini kuwa kauli ya Lowassa ya kukiita chama hicho cha kiharakati kwa kiasi kikubwa inaonyesha kuwakera mno baadhi ya vigogo wahadhifixa wa chama hicho kiasi cha baadhi yao kutokwa mwa kauli "Lowassa aondoke tu atuachie chama chetu cha kiharakati na uhanaharakati wetu".


Baadhi yao hao ,wakioneka kujawa na jazba, wamesikika wakisema: "leo ndio amebaini chadema chama cha kiharakati?

Wakati anakuja kutafuta hifadhi kwetu mwaka wa jana, hakuona chadewa wala viongozi wake kama ni wanaharakati, ila sasa?


Chanzo tazama
Joining date yako ni kiashiria muhumu kwamba ndio kundi lileeeeeeee!

Last Activity:10 minutes ago
Joined:May 27, 2016
Messages:201
Likes Received:175
Trophy Points:60
Liked:0
Siasa sa kuandama watu zimmesha pitwa na wakati kwa sasa, tudadili namna gan tutamuunga mkono rais wetu kukabiliana na changamoto anazo kutana nazo kwenye uongoz wake mapema namna hii dhidi ya wasio litakia mema taifa letu achana na mambo ya kujadili watu
 
Katika magazeti ya kipumbavu kabisa kuwahi kutokea hapa Tanzania TAZAMA linaongoza likifuatiliwa kwa karibu na Uhuru na Habari Leo.
 
Katika mambo ambayo mara nyingi nimekua nikimshukuru Mungu kwa Kutenda maajabu basi ni kutuepusha na pepari, fisadi na katili Lowas kuwa Rais wa Tz. Watu masikini nchi hii isingekuwa yetu tena, ingekua ya mabepari, wapiga madili makubwa. Unajua, baadhi yetu hatujui, fuatilia mambo ya huyo jamaa vizuri utatambua kwamba Sio rafiki kwa masikini. Ni mnyonyaji na kweli hapendi yeye na mafisadi wenzake wawe masikini. Asante Mungu kwa kutuepusha na janga hili. Hapa kazi tu.....
 
Back
Top Bottom