Lowassa aondoke tu. Ni kauli ya vigogo wa CHADEMA

Lowassa aondoke tu. Ni kauli ya vigogo wa CHADEMA

Chadema hawana ubavu wa kumfukuza Lowasa. Maana ile bei aliyoinunua chadema ni kubwa mno. Na leo hii ukisema warudishe hawana maana walishaigawana yote (mfano Mh. mchungaji wa iringa alipata mil 300) na sasa ukisema airudishe itakuwa majanga
Wafumkuze wakati alifika bei?
 
mwenyekiti wa CCM ameshawaambia wanaCCM kuwa Lowasa bado ni tishio kubwa sana kwa CCM.
sishangai hiazi sarakasi.
Vision ni kuwa tishio ama kushika hatamu za uongozi.....tishio its nothing but authority.....hata ukimwi ni tishio
 
Katika magazeti ya kipumbavu kabisa kuwahi kutokea hapa Tanzania TAZAMA linaongoza likifuatiliwa kwa karibu na Uhuru na Habari Leo.
Na magezeti makini kabisa duniani ni Tanzania Daima likifuatiwa na Mwanahalisi na Mawio.
 
kauli ya aliyekuwa mgombea urais wa Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Edward Lowassa, ya kwamba chama hicho ni cha kiharakati, inaone kuwakera wengi wa vigogo wakubwa ndani ya chadema.

Mara kadhaa, kwa chini kwa chini na hadharani, lowasa amekuwa akikiita cha chadema .

Mwanasiasa huyo ambaye katika kuusaka urais aliungwa mkońo pia na vyama vya Cuf, Nccr mageuzi na Nld, akiwa mto wa mbu, Monduli, Arusha hivi karibu kwenye mkutano wa hadhara aliamua kupaza sauti kwa kuwaomba wananchi wa eneo hilo kumuunga mkono katika juhudi zake hizo za kutaka kukikiondoa chama chake kipya îcho kutokuwa chama cha kiharakati na kuwa chama cha siasa kwa madai ya kukiandaa kikamilifu kukamata dola mwaka 2020.

Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wetu kwa siku kadhaa sasa, umebaini kuwa kauli ya Lowassa ya kukiita chama hicho cha kiharakati kwa kiasi kikubwa inaonyesha kuwakera mno baadhi ya vigogo wahadhifixa wa chama hicho kiasi cha baadhi yao kutokwa mwa kauli "Lowassa aondoke tu atuachie chama chetu cha kiharakati na uhanaharakati wetu".


Baadhi yao hao ,wakioneka kujawa na jazba, wamesikika wakisema: "leo ndio amebaini chadema chama cha kiharakati?

Wakati anakuja kutafuta hifadhi kwetu mwaka wa jana, hakuona chadewa wala viongozi wake kama ni wanaharakati, ila sasa?


Chanzo tazama
hizi hadith siku hizi hazinogi! labda utafute mambo yake binafsi.....
 
hahahah sikuelewi. tishio kwa ufisadi au. fafanua nini mantiki yake au tumuulize alikuwa anamaanisha nini

Muulize mwenyekiti wako jk alimaanisha nini kusema kwamba Lowassa baddo tishio.
 
Na magezeti makini kabisa duniani ni Tanzania Daima likifuatiwa na Mwanahalisi na Mawio.


Una akili sana wewe, hivi walikurudishia lini akili zako? maana wenzako wamebakishiwa za kuvukia barabara tu.
 
mwenyekiti wa CCM ameshawaambia wanaCCM kuwa Lowasa bado ni tishio kubwa sana kwa CCM.
sishangai hiazi sarakasi.
Wako wachangiaji 3 ambao akili zao zimepimwa kwenye mizani na zimeonekana kulingana. Lizaboni, TataMandiba na Rutashobolwa. The best thing one can do is to ignore them. Wanaweza kujinasibu ni makada wa chama chao lakini ukweli ni kwamba wana tatizo katika kudadavua jambo hata kama halihitaji akili kubwa. Wimbo wao ambao umechuja siku niyingi ni ule ambao ubeti wa kwanza ni : Lowassa Fisadi. Ubeti wa pili ni: Mbowe DJ. Nothing more. Wapuuzeni hao. Don't even bother to read what these three post.
 
Fisad

Fisadi fisadi fisadi
Ufisadi wake muliujua alipohamia upinzani? Mbona mulikuwa naye siku zote kimya? Basi kundi lenu ni mafisadi ndo maana munampigia kelele mwenzenu aliyeamua kuokoka na kuhamia kwa wapinga ufisadi.
 
Acha uongo, CDM hakuna kigogo anayeweza kumnyooshea kidole Lowassa. Hili gazeti la fundi viatu Mapunda ni la kupuuza. Mabilioni aliyotoa Lowassa kununua bidhaa, Chadema huwezi kumtoa hivi hivi labda Kingunge.
 
Chadema hawana ubavu wa kumfukuza Lowasa. Maana ile bei aliyoinunua chadema ni kubwa mno. Na leo hii ukisema warudishe hawana maana walishaigawana yote (mfano Mh. mchungaji wa iringa alipata mil 300) na sasa ukisema airudishe itakuwa majanga
Chadema wakisema iuzwe leo haiwezi hata kunuliwa kwasababu mafuriko yamekauka.labda wagawane fito tu.
 
Kuondoka kwa Lowassa bado kinaenaendelea kuwaumiza CCM....kila siku hawaishiwi kumzungumzia Lowassa....Poleni sana MACCM.
 
Kushabikia Jina la Lowasa ni aina nyingine ya kujitoa ufahamu...hata kama JPM hakushida uraisi kama wasemavyo wapinzani wake, basi sala, maombi mema yaliyofanyika misikitini na makanisani ndiyo yaliyosababisha tukampata JPM wala si kwa uwezo wetu, Mungu alitusikia ndo maana JPm yuko hapo kama raisi, vinginevyo ENL asingetufaa kabisa, ana mvuto tu, na analazimisha kupendwa kwa kutumia pesa.
 
mwenyekiti wa CCM ameshawaambia wanaCCM kuwa Lowasa bado ni tishio kubwa sana kwa CCM.
sishangai hiazi sarakasi.

Kama shetani alivyokuwa tishio kwa watu wa Mungu ndivyo Mh Lowassa alivyo tishio kwa CCM.
 
Lowassa yuko sawa kabisa, chadema wengi ni wanaharakati. Msigwa, lissu, mdee na wengineo ni wanaharakati.... Mwanasiasa ni mbowe peke yake....
 
Back
Top Bottom