Lowassa anajua uzalendo au ni ‘machozi ya mamba?’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa anajua uzalendo au ni ‘machozi ya mamba?’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiranja, Jan 18, 2012.

 1. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa wale waliokua wakisema Kubenea amenunuliwa na Lowassa sasa na waseme tena, maana watu wakisema huyu jamaa ni mtu asiyetabirika, hamuelewi. Leo kampa haki yake Lowassa.


  Lowassa anajua uzalendo au ni ‘machozi ya mamba?’
  *
  *
  Na Saed Kubenea
  *
  EDWARD Lowassa, yule aliyejiuzulu nafasi ya waziri mkuu kutokana na kashifa ya kuingiza nchi kwenye mkataba wa kinyonyaji wa makampuni ya Richmond/Dowans, sasa anasaka utakaso.
  *
  Katika kasi yake, anakemea hata asiostahili kukemea na anasema yale ambayo wengi wanajenga shaka kama anaweza kuyasimamia.
  *
  Akiwa mkoani Kigoma, kwenye harambee ya ujenzi wa Sekondari ya Kanisa la FPCT Bigabiro, Lowassa amenukuliwa akisema, “Nguvu ya umma inayotumiwa na baadhi ya vyama vya siasa kushinikiza serikali kutekeleza mambo mbalimbali, haiwezi kuleta maendeleo wala tija kwa taifa.”
  *
  Mbunge huyo wa Monduli, alifika mbali zaidi. Alidai kuwa hivi sasa wananchi wengi hawataki kujitolea kwa sababu “wamepoteza uzalendo.” Alisema kila wanachokifanya, ikiwamo kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao, wanataka kulipwa fedha.”
  *
  Jumla ya Sh. 125 milioni zikiwamo ahadi, zilichangwa kwenye harambee hiyo, huku taarifa zikisema Lowassa na wale aliowaita “marafiki zake,” walitoa Sh. 60.5 milioni.
  *
  Lowassa hakutaja jina la chama cha siasa ambacho ametaka kiachane na matumizi ya nguvu ya umma yanayolenga kushinikiza serikali kutekeleza matakwa ya wananchi. Wala hakutaja chama ambacho amekitaka kitumie nguvu ya umma kushinikiza wananchi kufanya kazi za kujitolea.
  *
  Bali kila mmoja anajua kuwa Lowassa amelenga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Hiki ndicho kinajitambulisha kwa kauli mbiu ya nguvu ya umma – “People’s Power.”
  *
  Je, Lowassa anaamini anachokisema? Anastahili kueneza anachokihubiri? Kama haamini anachokisema na anahubiri asichostahili kuhubiri, nini kimemsukuma kueleza haya sasa?
  *
  Kwanza, Lowassa haamini kwenye kujitolea “nguvu kazi.” Ndiyo maana kila anakopita, hakuna ambako aliweka nguvu kazi yake. Hakuna alikotoa jasho lake. Bali kote alikopita, kuanzia mkoani Singida, Mwanza, Arusha, Dar es Salaam, Pwani, Kilimanjaro na Kigoma, Lowassa amemwaga fedha, badala ya kujitolea nguvu kazi.
  *
  Pili, Lowassa anajua sababu za wananchi kupoteza uzalendo na kutaka kulipwa ujira kwa kazi wanayoifanya. Ni kwa sababu, wamechoshwa na vitendo vya viongozi wao waliowapa dhamana.
  *
  Kwa mfano, baraza la mawaziri liliagiza mkataba kati ya serikali na makampuni ya Richmond/Dowans uwe wa mwaka mmoja. Lakini baadhi ya viongozi, Lowassa akiwa miongoni mwao, walibadilisha maelekezo ya baraza la mawaziri na kuliamuru Shirika la Umeme la Taifa (Tanesco), kujifunga kwenye mkataba wa miaka miwili.
  *
  Aidha, kwa kisingizio cha nchi kutaka kuingia gizani, Lowassa aliamuru kubadilishwa kwa vigezo vya utoaji wa zabuni kutoka 24 vilivyowekwa awali hadi vinne ili kuweza kuibeba Richmond.*
  *
  Pale alipoona Richmond imeshindwa kukidhi hata kigezo kimoja kutoka miongoni mwa vigezo vinne vipya vilivyowekwa, kikiwamo kile kinachoweka sharti la kampuni kuwa na uzoefu wa angalau mwaka mmoja katika miradi ya umme, aliamuru kazi ya kutafuta mzabuni ifanywe na kamati ya serikali, badala ya Bodi ya Tenda ya Tanesco.
  *
  Mbali na hayo, Lowassa anafahamu thamani halisi ya mitambo ya Richmond/Dowans; *si zaidi ya dola za Marekani 40 milioni. Lakini kwa makusudi alikubali serikali kujifunga kwenye mkataba unaowalazimisha kuilipa kampuni hiyo, kwa kila siku, kama malipo ya kuweka mitambo – Capacity Charge – dola za Marekani 100,000; karibu Sh. 152 milioni.
  *
  Kiasi hiki ni nje ya fedha zinazotumika kununulia umeme; zitakazolipia matengenezo ya mashine na zitakazotumiwa kugharamia usafirishaji mafundi kutoka nje ya nchi.
  *
  Katika kipindi cha miezi 21 ya uhai wa mkataba, tayari Richmond/Dowans walishavuna kutoka serikalini, zaidi ya dola za Marekani 66.4 milioni (karibu Sh. 90 bilioni). Kiasi hiki cha fedha, ni mara mbili ya bei halisi ya mitambo.
  *
  Baadaye wanaojiita wamiliki wa Dowans wakaenda mahakamani kudai serikali kwa kisingizio cha kuvunjwa kwa mkataba wake wa miezi 24. Mahakama bila kuhoji uhalali wa fedha inayodaiwa; bila kuhoji sababu za Richmond/Dowans kutaka kulipwa mkataba wote, wakati uhai wa mkataba ulibaki miezi mitatu, ikaamuru Tanesco kulipa kiasi cha Sh. 90 bilioni.
  *
  Mahakama ikaweka hata sharti jingine la serikali kulipa riba ya karibu asilimia 30 kwenye viwango vya dola. Sasa deni linaendelea kukua siku hadi siku hadi kufikia Sh. *120 bilioni.
  *
  Ukichua kiasi ambacho mahakama imeamuru kilipwe kwa Dowans, ukakichanganya na fedha ambayo tayari serikali imelipa katika kipindi cha miezi 21 ya uhai wa mkataba, utapata jibu moja: Mashine zenye thamani ya dola za Marekani 40 bilioni, tayari zimevuna ama zinatarajiwa kuvuna dola za Marekani 258 milioni (Sh. 397 bilioni) ndani ya muda mfupi wa miaka mitano.
  *
  Kama hiyo haitoshi, serikali ikakubali kujifunga kwenye mkataba mwingine wa milele na milele na kampuni ileile iliyojibadili jina tu na kujiita Symbon Power LLC, lakini ikiwa inatumia mitambo ileile ambayo italipwa Sh. 365 bilioni.
  *
  Hadi hapa, nani anaweza kuitikia wito wa Lowassa wa “kujitolea?” Nani anaweza kumsikiliza? Kama kujitolea, mbona ni yeye aliyekuwa anatakiwa kufanya hivyo kwenye kipindi cha kusaini mkataba na kutafuta mzabuni?
  *
  Lowassa ameshindwa nini, wakati alikuwa analipwa na serikali; analishwa na serikali na anavishwa na serikali? Hata sabuni ya kufulia mto wa kitandani kwake, shuka la kujifunika, sabuni na makochi anayotumia, vyote vinalipiwa kwa fedha za wananchi?
  *
  Yule aliyeshitaki serikali; aliyelipwa mabilioni ya shilingi na serikali kwa mashine zenye thamani ya Sh. 60 bilioni; na ambaye sasa anashinikiza kulipwa mabilioni mengine, ni mmoja wa maswahiba wakuu wa Lowassa na mshirika wake mkubwa kisiasa, Rais Jakaya Kikwete.
  *
  Rostam Aziz, mwanachama mashuhuri na muhimu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndiye aliyeshitaki, aliyeajiri mawakili, ndiye alidai na ndiye anayepokea na atakayepokea malipo yoyote ya fedha kwa niaba ya makampuni ya Dowans Holding SA, Dowans Tanzania Limited (DTL) na Richmond Development Company (LLC).
  *
  Lakini kuna hili pia. Lowassa anafahamu jinsi katibu wa Tanesco, Subira Wandiba,* alivyojitolea kwa taifa lake. Alieleza kwa ufasaha ubatili wa hatua ya Richmond ya kuhamisha mkataba.
  *
  Wandiba alikuwa akiandikia mwenyekiti wa bodi ya TANESCO, Balozi Fulgence Kazaura, tarehe 28 Novemba 2006, kwamba “…kufuatana na mkataba wa 23 Juni 2006, Richmond hairuhusiwi kuhamisha mkataba wao kwenda kampuni nyingine yeyote.” Hii ilikuwa kabla ya mkataba kumilikishwa kwa Dowans.
  *
  Lakini nani alimsikiliza Wandiba? Nani alisikiliza ushauri wake, kwamba Richmond – kampuni iliyopewa mkataba kwa upendeleo, ikiwa haina fedha, haina utaalam wala historia ya kufua umeme – haikupaswa kuhamisha mkataba wake kama ilivyofanya tarehe 23 Desemba 2006. Ilikuwa kinyume cha sheria za nchi.
  *
  Akiwa nchini Canada, Nazir Karamagi aliyekuwa waziri wa nishati na madini, aliamuru Richmond kuruhusiwa kuhamisha mkataba wao. Leo hii, Wandiba ameondolewa kwenye nafasi yake hiyo. Je, uzalendo ambao Lowassa anasema uko wapi, ikiwa wale ambao wameonyesha uzalendo ndio wanasakamwa na hata kuondolewa kazini?
  *
  Nani anaweza kuwa mzalendo, wakati wale ambao wamesababisha haya, wanaendelea kupeta? Wanalipwa na serikali. Wanahudumiwa na serikali. Wanatumia magari ya serikali; wanakaa nyumba za serikali na wanatibiwa nje ya nchi kwa gharama za walipa kodi wa hapa?
  *
  Nani ataweza kuwa na moyo wa kujitolea, wakati Lowassa mwenyewe anaendelea kulipwa mafao ya waziri mkuu mstaafu, wakati ukweli ni kuwa hakustaafu?
  *
  Nani anaweza kujitolea nguvu kazi yake wakati anaona rasilimali za taifa zinatumika kugharamia watu walioshindwa kazi; waliongiza nchi kwenye mikataba yenye utata na wanaoendelea kulipwa, wao na wasaidizi wao, kwa fedha za walalahoi?
  *
  Nani ataweza kutumia nguvu kazi yake kufanya kazi ya maendeleo, wakati nguvu walizotumia kufanya kazi zao binafsi na kulipa kodi kubwa isiyo na kipimo, inatumiwa na wale waliosaidia kufikisha taifa hapa lilipo?
  *
  Nani atakubali kumwaga jasho lake kufanya kazi za kujitolea, wakati wanaona kiongozi wao – Waziri Mkuu Mizengo Pinda – anayelipiwa kila kitu na serikali akisaini posho ya Sh.250,000 kwenye semina ya Bunge?
  *
  Ilitegemewa badala ya Lowassa kuwaalani na kuwadhihaki wanaoshinikiza wananchi kupinga udhalimu huu; wanaotaka serikali kuwajibika kwa wananchi wake; wanaotaka kupunguzwa kwa ugumu wa maisha; angesimama pamoja nao – hata kama yeye si miongoni mwa wanaojua bei ya sukari, mafuta, chuvi, umeme na kibiriti – kuhimiza serikali kutekeleza wajibu wake.
  *
  Angalau angefanya hivyo, angeweza kusamehewa kwa dhambi hii aliyosababishia taifa hili. Lakini kwa hatua yake ya kusema wananchi – wenye njaa, wanaopunjwa bei ya mazao yao, wanaolazimishwa kutoa rushwa kwa kila huduma wanayostahili – wamepoteza uzalendo; basi amefanya dhihaka ambayo inahitaji toba.
  *
  Wananchi waandamanaji ambao Lowassa anawalaani wanataka kuona taifa lao linatokomeza ufisadi; linakuwa taifa huru kwa watu huru. Wanaoandamana wanataka kuona heshima, utu wao na mali za taifa vikirejeshwa.
  *
  Wanaoandamana wanataka kuona misingi ya haki inatolewa kwa raia wote, bila kujali kipato cha mtu, umaarufu wa mtu au nasaba yake. Wananchi wanaoandamana wanataka kuona utawala wa matabaka nchini unatokomezwa. Hakuna tena mabwana na watwana.
  *
  Wanataka kuona tofauti kubwa ya kipato kati ya masikini na matajiri inaondoka. Huduna zinapatikana katika hospitali za umma. Karo kwenye shule za msingi, sekondari na vyuo, zinalipwa na serikali, tena bila ubaguzi.
  *
  Wananchi wanataka kuona wote walioiba au walioshiriki wizi, ukwapuzi na ufisadi wa aina yoyote ile lakini bado wamejificha nyuma ya siasa au wanalindwa na watawala, wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.
  *
  Wanataka kuona walioshiriki kuuza nchi kwa njia ya kunadi raslimali za taifa kwa bei ya karanga, wakichukuliwa hatua na jeuri yao inakoma mbele ya nguvu ya umma.
  *
  Wanaotetea nguvu ya umma wanataka kuona walioingiza taifa hili katika mikataba ya kinyonyaji wanaswekwa mahakamani na wanazuiwa hata kugombea uongozi wa ngazi yoyote.
  *
  Kuchukuliwa kwa hatua hizi ndiko pekee kunakoweza kurejesha uzalendo; chini ya watawala wapya ambao mikono yao haihusiki hata kidogo na ukamuaji jasho na damu ya wananchi.
  *
  Moyo wa utaifa – uzalendo – utarejea chini ya watawala wapya ambao wanathamini nguvu kazi ya umma; wale ambao hawahusiki hata kidogo na wala hawajawahi
  kushiriki ufisadi na ukamuaji jasho na damu ya wananchi.
  *
  *
  mwisho*
  *
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda makala hii
  Mwandishi kweli amechambua
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ukimsikiliza nape ,ukirudi kwa lowasa,ukipitia kwa membe ukija kwa 6 akaangalia anayofanya nyalandu ukarudi serikalini juu ukawasikiliza unapata jibu hili,
  ccm imefika mwisho sawa na mbwamwitu mnyama wanagawana juu kwa juu na atakayebaki na damu mdomoni nae ni chakla.:lol:
   
 4. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hakuna cha kusema zaidi.
  Wanaomsafisha Lowassa, wajipange upya.
   
 5. C

  Chesty JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 2,348
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Kubenea amejipanga sana kwenye hii makala. Anamshangaa Lowasa kuzungumzia uzalendo ambao haupo kwenye moyo wake. Mtu wa namna hii ambaye anajua kabisa kuwa watanzania wanajua kuwa ni msaliti wa uzalendo wa nchi yake halafu leo anakuwa na guts za kuongelea uzalendo.

  Nyerere pia alipima uzalendo wake akaona hatufai kabisa, eti leo amekuwa mwalimu wa uzalendo kama sio laana ni nini hii.
   
 6. M

  MALAGASHIMBA Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Makala nzuri sana kaka,endelea hivi hivi,usitumike tena
   
 7. naninibaraka

  naninibaraka JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  sijaoni jambo baya kwa lowassa kuwa karibu na waumini na kuchangia maendeleo,kubenea kawa bias kwa sababu kuan viongozi wengine kama sitta,membe na wengine ambao wanatumia makanisa ili kutafuta umaarufu,kwa nini lowasa peke yake?
   
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  'Everyone has a price; the important thing is to find out what it is' Pablo Escobar
   
 9. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wale waliokuwa wanasema kubenea kanunuliwa na lowasa, sasa watasema kanunuliwa na nani?
   
 10. Dume la Mende

  Dume la Mende JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 419
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hana lolote huyu ana tamaa ya madaraka na kukimbilia Ikulu.Tumwogope kama ukoma
   
 11. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Hata ungemsafisha kwa dodoki la chuma huyo hasafishiki kama KIMBA!
   
 12. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  Good moves makanisa kwani nyie ndo mnajua ni jinsi gani anavyoweza kuturudishia fedha zetu ni through kumkamua mpaka arudishe zote then akimaliza alizokwapua serilkalini miskiti na nyie anzeni kumkamua zake binafsi ili tuone huo uzalendo wake anao uhubiri sasa... RICHMOND 40% juu juu zaidi....we turudishie fedha zetu maana magamba menzako yanakuogopa kukufikisha mahakamani then UTUBU DHAMBI ZAKO kwani wanao kufa kwa kukosa uduma za msingi kisa wewe/nyie ni wengi
   
 13. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Iidumu Azimio la Arusha!
   
 14. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Big up Kubenea, umesema sana,bora nisikutane na Lowassa hivi karibuni maana naweza mrushia kiatu!
   
Loading...