Lowassa ana dhambi nyingine zaidi ya Richmond?

Amejitangazia ushindi dhidi ya wabaya wake lakini mbaya wake mkuu ni mwananchi hao katu hawezi kujitangazia ushindi. Wananchi ndiyo watakaozima purukushani zake na siyo harambee za makanisa wala misikitini.

Watu wa karibu na E. Lowasa wamwambie adui yake si JK wala Nape Nnauye bali adui yake ni wananchi wanaochukia ufisadi alioufanyia nchi na kugeuka mungu mtu ndani ya CCM asiyefukuzika.
 
lowasa ni zaidi ya umjuavyo....hakuna wa kufanana naye hapa tz, labda kwa mbali sana.....RA (kwa kifupi ni zaidi ya Intelligent)
 
Safari ya Nigeria imejibu... Tutayakumbuka maneno ya Mwalimu alipomkariri mwanafalsafa wa kiyunani.... "watu wanaofaa kuwa marais huigopa na kuiheshimu nafasi hii".."Ukiona mtu anausaka uraisi kwa udi na uvumba..ujue iko maneno zaidi ya hapo". Twende makanisani na misikitini kushuhudia jinsi Mwuumba alivyotusitiri..Lakini si kutangaza ushindi wa kisiasa. Amrudie Mungu kwa kutaja madhambi yake yote tuyasikie pia kama mwendo ni huo.....
 
Lowasa kakomaa kisiasa anajua nini cha kusema na kwa wakati gani.....haya si maneno yake hata kama ningeamka saa nane usiku ningemkania.Haya ni najungu fitna na umbea,unadhani utarudisha maamuzi kwa majungu haya the train has gone no reverse.
 
Tatizo la watu kama nyinyi huwa mmezoea kupata tathmini katika scale ya one to one (1:1) hebu tathmini hotuba ya EL singida leo ktika scale ya one to hundred (1:100) utaelewa vizuri mleta mada anauelewa mpana

Huwezi wapotosha watanzania wa karne hii
 
Lowasa kakomaa kisiasa anajua nini cha kusema na kwa wakati gani.....haya si maneno yake hata kama ningeamka saa nane usiku ningemkania.Haya ni najungu fitna na umbea,unadhani utarudisha maamuzi kwa majungu haya the train has gone no reverse.
Mtu yoyote mwenye akili timamu na sio "bendera fuata upepo" ataona kuna watu wamewekwa hapa kwa ajili ya 2015.Na kazi yao ni kutengeneza habari za kummaliza Lowassa kisiasa.
 
Jamaa amedai Mungu kamficha dhidi ya maadui wake wote... Amechangia 10mil out of 138mil zilizopatikana...

Nahisi huyu jamaa anachanganyikiwa na kutapatapa, baya zaidi udhaifu ulionyeshwa na NEC na CC kushindwa kumchukulia hatua kwake yeye ni ushindi mkubwa sana.....na ndio maana ameanza kutoa kauli za kejeli kwa wanachama na wananchi kwa ujumla....
Kwa ujumla walichokifanya akina Nape dhidi ya Lowasa ni makosa ya kimkakati ambayo sasa yanaigharimu NEC kufanya maamuzi dhidi yake.

Kingine CCM itambue kuwa huyu Bwana amejishikiza sana na kanisa hususan Lutheran na ana sapoti kubwa ya waumini wa kanisa kutokana na michango yake kwenye harambee..

Binafsi sina tatizo na Lowassa as long as siamini kuwa Lowasa anaweza kuwa mchafu na Swaiba wake akabaki msafi, manake dili nyingi walicheza pamoja.. Isitoshe huyu Bwana alikuwa Mchapakazi kulinganisha na waliobakia madarakani..!
 
hii statement ya mheshimiwa kwamba ushindi tayari umepatikana is rather strange; huenda alihisi kwamba vita kubwa ingekuwa kwenye NEC ndio maana akaamua kushambulia badala ya kusubiri kuwekwa kitimoto; but now that NEC wamemgwaya na kurudisha mchakato kwenye CC [ambako possibility ya kumn'goa ni so remote] labda ndio maana anaona kwamba kashinda
 
let him be! He has crushed his enemies, let him enjoy the moment! But will it last?
 
labda kama atatumia njia mbadala lkn kama n nguvu ya uma ikulu atakuwa akipita kwa nje tu wakati anaenda kununua samaki feri
 
lowasa mwacheni jamaani awe raisi wetu tuondokane na viongoz maneno tunataka watendaji

Hatumuachi ng'o mpaka atutajie richmond ilikua ni ya nani na nani?na kwanini toka zama hizo mpaka yeye kushika madaraka tukaendelea kuamini suluhisho la matatizo yetu ya umeme ni kukodi majenereta toka nje ya nchi???
 
Nikiwa kama mtanzania ninaetafakari juu ya hali ya siasa tz, ninasimama ktk ukweli kusema zaidi ya Richmond hakuna ruhwa yenye mashiko ya kumuhukumu roho ya paka Lowasa!

Mwenye ushahidi wa ufisadi mwingine wa Lowasa auweke hapa! Kama si zaidi ya propaganda za wapinzani wake kisiasa!
Wewe una ushahidi gani kuhusu kiongozi yeyote wa serikali sasa hivi?
 
Maswali mengine yanaulizwa na watu ambao uwezo wao wa kukumbuka matukio umefifishwa na mapenzi kwa huyu mtu wao. Kama unataka makosa mengine ya Lowassa basi mtafute mwalimu Nyerere.

Mwalim alikuwa hapendi watu aggressive wanaojitafutia maisha, mwalim mwenyewe aliwahi kutuambia mkapa ni Mr Clean!
 
Mwalim alikuwa hapendi watu aggressive wanaojitafutia maisha, mwalim mwenyewe aliwahi kutuambia mkapa ni Mr Clean!

usiwe mjinga kama lowassa!kwa hiyo na wewe unataka kutuambia lowassa ni mr clean hivyo tuzunguke mitaani kumsafisha sio?
 
Mwenye evidence za ufisadi wa EL aumwage hadharani sio maneno tu

Nani alikwambia rushwa huwa ina evidence, lakini zaidi ya richmond muulize El wakati anagombea 1995 baba wa taifa alimuuliza nini na kwa nini alikosa majibu. Na hiyo ilikuwa kabla ya Richmond wakati baba wa taifa anasema ananuka rushwa lakini kama vile sikio la kufa halisikii dawa nilidhani baada ya kuwa waziri mkuu angejirekebisha ila bado akaendelea na richmond. Hilo ndilo tatizo lake
 
Una ushahidi kuwa baba wa Taifa alimuuliza maswali au ni makala ya Kasori? Mwaka ule kulikuwa na wagombea wengi na walienguliwa wengi tuuuu na hao waliulizwa maswali gani au walienguliwa kwa sababu gani? Warioba, Bomani, Malecela, n.k. Mbona Kasori amemuongelea Lowassa tu? Kasori hakuwa mjumbe wa CC alikuwa mshika mkoba wa Mwalimu kwa hiyo hana mandate ya kuisemea CC ama NEC. Ni tetesi tu
 
Back
Top Bottom