Hakuna popote pale nilipohamisha goli weka uthibitisho wa kuonyesha kwamba siku za nyuma niliandika hivi na hivi karibuni niliandika tofauti na kile nilichoandika siku za nyuma. Kama ushahidi kama huo upo uweke hapa tuujadili badala ya kukurupuka.
Soma nilipoku quote kwamba fisadi ana mfagilia fisadi mwezake.
Ama ulipoandika hivi ulikuwa na maana gani?
"tunaambiwa aliiongoza nchi kwa umakini, uadilifu na ushupavu mkubwa!!!! Fisadi anamsifia fisadi mwenzie ili apigiwe debe 2015!!!!"
Huo ulikuwa msimamo wangu wakati ule na hadi leo hii sioni wapi nilihamisha goli labda kama Kiswahili kinakupiga chenga. Wote hao ni mafisadi.
Leo kawa kamandaMkuu huyu fisadi kapotoka sana na wala si kidogo. Kwanini anaukimbia ukweli wa utendaji wa fisadi Mkapa wakati Watanzania wengi tunaufahamu!? Unafiki kitu kibaya sana.
Ila chaajabu huyo lowasa na sumaye ndio uliowanadi kuwa wakombozi wa kweli kwa watzHapo tunakubaliana kabisa Lowassa ni fisadi, Mkapa ni fisadi, Sumaye ni fisadi, Magufuli ni fisadi na Kikwete pia ni fisadi. Ingekuwa amri yangu Lowassa na Sumaye wasingepokelewa CHADEMA, lakini huo ubavu sina.
SubiriWapi nilipowanadi wewe!? Weka ushahidi wa kuthibitisha ulichoandika. Acha kukurupuka!
Hili swali "Lowasa ni fisadi?" hawezi kulijibu sasa. Ni ngumu kumeza.Lowasa ni fisadi? Na bado ukampigia kura ya ndiyo. Nimekuelewa mkuu kiswahili sasa nimekipata vyema.