Lowassa ammwagia sifa Mkapa

Labda uwe na akili finyu ndiyo utaona vichekesho. Hivyo vichekesho utakavyoviona viweke hapa ili tuvijadili.

jamaa anatamani angekua amejiunga jf mwaka huu. hahaha ngoja tuendelee kufokonyoa nyuzi zake za zamani tuone vichekesho
 
Hakuna popote pale nilipohamisha goli weka uthibitisho wa kuonyesha kwamba siku za nyuma niliandika hivi na hivi karibuni niliandika tofauti na kile nilichoandika siku za nyuma. Kama ushahidi kama huo upo uweke hapa tuujadili badala ya kukurupuka.

Soma nilipoku quote kwamba fisadi ana mfagilia fisadi mwezake.
Ama ulipoandika hivi ulikuwa na maana gani?

"tunaambiwa aliiongoza nchi kwa umakini, uadilifu na ushupavu mkubwa!!!! Fisadi anamsifia fisadi mwenzie ili apigiwe debe 2015!!!!"
 
Huo ulikuwa msimamo wangu wakati ule na hadi leo hii sioni wapi nilihamisha goli labda kama Kiswahili kinakupiga chenga. Wote hao ni mafisadi.

Lowasa ni fisadi? Na bado ukampigia kura ya ndiyo. Nimekuelewa mkuu kiswahili sasa nimekipata vyema.
 
Jamani mnafukua makaburi sasa. Jamaa alikuwa anampiga mawe vibaya sana. Sasa ndio we kwanza kupiga brashi.
 
Mkuu huyu fisadi kapotoka sana na wala si kidogo. Kwanini anaukimbia ukweli wa utendaji wa fisadi Mkapa wakati Watanzania wengi tunaufahamu!? Unafiki kitu kibaya sana.

Leo kawa kamanda
 
Hapo tunakubaliana kabisa Lowassa ni fisadi, Mkapa ni fisadi, Sumaye ni fisadi, Magufuli ni fisadi na Kikwete pia ni fisadi. Ingekuwa amri yangu Lowassa na Sumaye wasingepokelewa CHADEMA, lakini huo ubavu sina.
Ila chaajabu huyo lowasa na sumaye ndio uliowanadi kuwa wakombozi wa kweli kwa watz
 
Hakuna kitu kama hicho mie si bendera fuata upepo wa kuyumbishwa yumbishwa katika misimamo yangu yoyote ile. Utalala na kushinda humu 24/7 365 days KAMWE hutaweza kuthibitisha ulichoandika.

Back
Top Bottom