hekimatele
JF-Expert Member
- May 31, 2011
- 9,889
- 2,799
13. (1) Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa:-
(a) Kujiuzulu mwenyewe;
(b) Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(c) Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(d) Kutotimiza masharti ya uanachama.
(e) Kujiunga na Chama kingine chochote cha
siasa.
(2) Mwanachama ambaye uanachama wake
unakwisha kwa sababu yoyote ile
hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada
aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.
(3) Mwanachama aliyeachishwa au kufukuzwa
Uanachama akitaka kuingia tena katika
CCM, itabidi aombe upya, na atapeleka
maombi yake hayo ama katika Halmashauri
Kuu ya Wilaya ama kikao kilichomwachisha
au kumfukuza Uanachama.
(4) Mwanachama aliyejiuzulu akitaka kuingia
tena katika CCM ataomba upya kwa kufuata
utaratibu wa kuomba Uanachama kwa
mujibu wa Katiba ya CCM.
14. Mwanachama yeyote atakuwa na haki
zifuatazo:-
(1) Haki ya kushiriki katika shughuli zote za
CCM kwa kufuata utaratibu uliowekwa.
(2) Haki ya kuhudhuria na kutoa maoni yake
katika mikutano ya CCM pale ambapo
anahusika kwa mujibu wa Katiba.
(3) Haki ya kuomba kuchaguliwa kuwa Kiongozi
wa CCM na ya kuchagua viongozi wake wa
Katiba ya Chama Cha Mapinduzi 11
Kuondoka katika
Chama
Haki
sawa mkuu