Jamaa kaja na style kali ya kumfagilia Lowassa, hii nimeitoa hapa:
Lowassa; "Mungu Yupo Na Mimi Nitayashinda Majaribu" « Strictly Gospel
Lowasa Edward Ngoyayi akiwa Rais wa Tanzania mambo 10 yafuatayo yatatokea:
1. Mfumko wa Bei utashuka kutoka 17% ya sasa hadi 5% ndani ya miaka 5 ya mwanzo
2. Thamani ya Shiilingi ya Tanzania itaimarika zaidi dhidi ya sarafu za nje hasa Dollar ya marekani na Yuro ya Ulaya.
3. Shule za Sekondari zote za Kata alizoziasisi zitapata mabweni, Maabara, Vitabu, Walimu, Mdawati na Vifaa vyote muhimu ndani ya Miaka 2 ya mwanzo.
4. Uchumi utakua kwa kasi kama ya ndege inayotaka kupaa angani kama enzi za Mkapa. Kumbukeni wakati ule wa Mkapa uchumi ulitaka kupaa ila baada ya Mhe. Kikwete kuingia Ikulu, ile ndege iliyotaka kupaa kama alivyosema Mkapa iliamua kuahirisha safari.
5. Lowasa akiwa Rais wa Tanganyika na Zanzibar muungani wetu utaimarika zaidi. Natamani tuwe na Serikali Tatu. Kama serikali 3 haziwezekani basi Bora tuwe na Serikali MOJA yenye nguvu kiuchumi. Tuwe na Rais aliye na nguvu pande zote visiwani na Bara.
6. Lowasa akiwa Rais wa nchi hii, Reli ya Kati toka DAR – KIGOMA/MZA itatengenezwa kwa kasi ya hali ya juu. Ndani ya miaka 3 ya mwanzo Reli itakuwa iko saaaafi sana.
7. Lowasa akiwa Rais wa Nchii hii, uwajibikaji katika ofisi za umma, serikali na Binafsi utaongezeka kwa kasi. Sasa hivi Bara na visiwani uwajibikaji wa kazi umepungua sana. Watu wengi wanafanya dili za fedha tu bila kuchapa kazi. Lowasa si unamjua anavyowaka hapo hapo na kuwawajibisha wazembe bila kusubiri maamuzi ya vikao na taratibu na kanuni za kazi. Ukivurunda hapo ulipo anakuwasha vibao na kibarua kinaota miguu.
8. Lowasa akiwa Rais, waislam na wakristo wataheshimiana na wataweza kufuata maadili ya dini zao. Rais akiwa Lowasa Makamu wake atakuwa Mwislam na Waziri Mkuu atakuwa Mwanamke mama Anna Tibaijuka (Professor).
9. Lowasa akiwa Rais, ufisadi utaendelea lakini kazi mahala pa kazi zitaonekana na maendeleo yataonekana kwa haraka na uwajibikaji utaonekana kwa haraka. Kwa sasa ufisadi upo, uwajibikaji hakuna, kuwajibika au kuwajibishwa hakuna. Lowasa akiwa Rais watu siyo kwamba hawatafanya ufisadi wa mali za umma ila naamini nidhamu itakuwepo. Hata kama yeye anasemwa kuwa ni fisadi, lakini kazi zake kama waziri Mkuu tuliziona. Tatizo ni kwamba wengine ni mafisadi tuuuu ambao kazi yao ni kufukuzia dili za pesa kila kukicha, kazi za maendeleo hawafanyi. Kumbuka Mkapa alivyokuwa mchapa kazi. Kuchapa kazi hakumwondoi kuwa fisadi. Lakini watu hawatamsahau kamwe kwani aliweza kuushusha mfumko wa bei kutoka asilimia 40% mwaka 1995 hadi 5% mwaka 2005. Lowasa akiwa Waziri Mkuu Maamuzi magumu ya kuwajibisha wazembe aliyatekeleza na ndiyo maana na yeye aliamua kujiuzuru ilipotokea kashifa ya Richmond.
10. Lowasa akiwa President wa URT wanafunzi wa elimu ya juu wote watapewa mikopo bila ubaguzi wala bila hata mmoja kubaki kwa visingizio vya bajeti ya serikali kuwa ndogo.
Unakumbuka alivyoshawishi mabenki mwaka 2007 yafute vikwazo vya utoaji mikopo kwa wajasiliamali waliokuwa wanaomba mikopo ile ya mabilioni ya JK? Mabenki yalikuwa yamegoma yakitaka DHAMANA ZA MIKOPO hiyo iwe viwanja vya nyumba, Lowasa akakataa kwani kulikuwa na dhamana ya serikali.
Lowasa akiwa Rais, atashawishi Mifuko ya Pensheni, LAPF, PSPF, NSSF, PPF, GEPF, ZSSF iweke utaratibu wa kukopesha wanafunzi wa elimu ya juu kama alivyoishawishi yote kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma -UDOM. Kile chuo kimejengwa kwa fedha za kutoka Mifuko hiyo ya pensheni nchini na siyo wafadhili. Aidha, atashawishi mabenki yote ya biashara kutoa mikopo ya riba nafuu kwa wanafunzi wote wanaokidhi vigezo vya kusoma elimu ya juu.
Hayo ni baadhi tu ya yale yanayotarajiwa ikiwa Lowasa atagombea kuwa Rais na akashinda wapinzani wake wa kisiasa. Lowasa hata kama anatafsiriwa kuwa mchafu ni kwa sababu tu aliamua kujiuzuru. Hii haina maana kwamba wale ambao hawakujiuzulu walikuwa WATAKATIFU. Hivi kuna mtu wezaye kuwa Mtakatifu huku akiwa mwanasiasa?
LOWASA EDWARD NGOYAYI, SONGA MBELE, MUNGU IBARIKI TANZANIA. HATA KAMA HUTAKUWA RAIS WA NCHI HII, WENGI TUTAKUKUMBUKA KWA MICHANGO YAKO YA MAENDELEO KWA NCHI HII NA WATU WAKE HASA MAKANISA/MISIKITI HATA KAMA UNGEKUWA FISADI WA VIPI?
LOWASA EDWARD NGOYAYI WEWE NI POOA SANA. UNYENYEKEVU WAKO SIYO TU KWAMBA UTAKUKWEZA BALI PIA UTAKUOKOA MILELE.
WATU WA KIGOMA TUNAKUKUMBUKA SANA ULIVYOSAFIRI KWA GARI TOKA BIHARAMULO-KIBONDO-KASULU, NGURUKA- UVINZA TABORA ILI KUANZA MCHAKATO WA KUTENGENEZA BARABARA YA LAMI TOKA KIGOMA HADI DODOMA. SONGA MBELE.