Lowassa akiwa Rais, Mwakyembe na wenziwe wataishi wapi?

Lowassa akiwa Rais, Mwakyembe na wenziwe wataishi wapi?

kauli nzito

New Member
Joined
Jan 22, 2014
Posts
2
Reaction score
2
Ni vigumu kama si muhali kujua kwa uhakika nani atakuwa Mrithi wa Rais Kikwete au pia tuseme Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ugumu huo unatokana na ukweli kuwa Siasa za ndani ya vyama na siasa za ushindani ndizo zitakazoamua.

Kwa upande wa Siasa za ndani ya Vyama, CCM ina nidhamu yake ya kupokezana madaraka kila baada ya kipindi cha muongo mmoja. Vumbi hutimka kwelikweli pale Rais kutoka chama hicho anapomaliza muda wake kwani wanachama wote huwa huru kuchukua fomu ya kugombea Urais.

Ukitembea ndani ya fikra za wana-CCM, unaweza kukuta kila mtu hana jawabu la kitendawili cha nani atakuwa mgombea wa chama hicho. Siasa za ndani maana yake ni mchujo wa majina ya watakaoomba kugombea nafasi ya Urais.

Kamati Kuu ya CCM ndiyo yenye dhamana ya kuchuja wagombea. Ni vigumu kutabiri nani atachujwa, na nani atapita. Ukiitazama nguvu ya Kamati Kuu ya CCM unaweza kusema labda Mwenyekiti wa CCM-Taifa anaweza kuwa na uhakika wa kiasi fulani nani atakuwa mgombea wa kumrithi yeye mwenyewe katika nafasi ya Urais.

Kwamba labda yeye pekee tayari anaye Rais ajae kichwani mwake. Lakini bado mazingira yanaweza kulipiga kumbo wazo lake kwani hata Mkapa huenda alikuwa na ‘Rais' wa kumrithi kichwani mwake lakini mwisho wa siku JK ambaye hakuwa kichwani mwake akawa Rais.

Si ukweli wa kuficha kuwa Dkt. Salim alikuwa na nafasi kubwa vichwani mwa wazito wa chama hicho. Kumbe basi, hata katika siasa za ndani bado nako kuna kitendawili.

Kwa upande wa siasa za ushindani, zenyewe ziko za aina mbili; mosi ushindani wa kupata kura za kutosha za Wajumbe wa Mkutano Mkuu, na pili, ushindani wa kupata kura za wananchi.

Kwa imani ya CCM, ushindani wa kupata kura za Wajumbe wa Mkutano Mkuu ni mgumu mno kuliko ule wa kupata kura za wananchi. Kwa mtazamo wao, kupata ushindi wa kura za wajumbe ndio tayari kuna maana ya kupata Urais.

Kwamba siasa za ushindani wa nje ya chama dhidi ya vyama vya upinzani kwao si tatizo sana. Makala hii itajikita zaidi katika siasa hizo za ndani za CCM na ushindani wake.

Binafsi sina uhakika na demokrasia ya Kamati Kuu ya CCM ndiyo maana naita "siasa za ndani". Kama ni mtu mmoja au watu wachache wanaoamua nani awe mgombea wa chama, hilo ni gumu kujadilika.

Lakini ‘weupe' wa demokrasia ya chama huanza kuonekana pale mambo yanapotoka ndani ili Wajumbe wa Mkutano Mkuu ‘wamaliza kazi'. Mwaka 1995, kidogo demokrasia ilikuwa na ‘wingu' la Butiama, Mwalimu wa Pugu aliishikia fimbo demokrasia kuhakikisha kuwa ‘mtu wake' anapita.

Ushindani wa 2005 bila ‘Wingu la Butiama'

Lakini mwaka 2005, demokrasia ilitakata kwani ‘wingu la Butiama' halikuwepo tena. Wadadisi wa siasa za CCM wanasema laiti ‘wingu' lile la Butiama lingeendelea kuwepo mwaka 2005, basi Dkt. Salim angepata Urais. JK angeendelea kusubiri, na angeenguliwa mapema ili kuokoa nafasi ya Salim mikononi mwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu.

Kwa kutoweka wingu, bila kutarajia, Jakaya Kikwete akamshinda mtu aliyepewa nafasi kubwa ya ushindi, Dkt. Salim Ahmed Salim. Laiti Kikwete ‘angekula panga' la Kamati Kuu, Salim angekuwa Rais wa Nne wa Tanzania.

Lakini wengine walisema laiti ‘embe bivu' lisingekatwa panga la Kamati Kuu, basi ushindani wa JK na Malechela ungekuwa mkubwa zaidi kuliko ule wa JK na Salim ambapo kura za ushindi kwa JK zilikuwa nyingi mno.

Mazingira ya safari hii hayajaonesha nani na nani wanaweza kutikisa siasa za CCM lakini watabiri wa mambo ya siasa tayari wanasema kuwa kama panga la Kamati Kuu ‘litamkosa' mzee wa Monduli, halafu uamuzi wa mwisho waachiwe wajumbe wa Mkutano Mkuu, basi Edward Ngoyai Lowassa ana nafasi kubwa ya kupeperusha Bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa 2005.

Edward Lowassa

Kuna aina mbili za vikwazo kwa Mhe. Edward Lowassa; mosi, wapo wanaoogopa kuwa Lowassa ana maamuzi makali na anaweza kulipa visasi jambo ambalo litakuwa na maana kuwa wajumbe wa iliyokuwa Kamati ya Richmond iliyomporomosha Waziri Mkuu watafute pa kuishi endapo mwanaCCM huyo atakuwa Rais.

Siasa hizo za visasi ni hatari kwa nchi na wananchi. Hivyo busara ya Kamati Kuu inaweza kuliepushia Taifa janga la siasa za visasi. Pili, wapo wanaoamini kuwa Lowassa ana kashfa mbaya ambazo zimewakera wananchi wengi, na akisimama kugombea urais, CCM itakuwa imejimaliza yenyewe!

Hivyo, busara ya Kamati Kuu inaweza kukinusuru chama kwa kukata jina la Lowassa. Lakini wengine wanasema Urais ni mamlaka yanayozunguukwa na washauri wengi.

Rais hawezi kukurupuka bila ushauri. Hivyo, hata akiwa Rais, bado Lowassa hawezi kuamua atakavyo. Wengine wanasema urais ‘unashepu' saikolojia ya mtu. Wengi wanatoa mfano wa Rais Kikwete kwamba ni mtu aliyebadilika mno kwa siasa za Urais tofauti kabisa na alivyokuwa Waziri.

Baadhi ya waliotaka kumkataa asiwe Rais waliitazama zaidi haiba yake alipokuwa Waziri. Wapo waliomuona kama ni mtu mwenye kujinata ambaye hata marafiki wa karibu walipotaka msaada wake Wizarani waliishia getini.

Wapo walioona kuwa ujana ulimzidi sana hivyo Ikulu isije kugeuka ukumbi wa disko! Wapo waliomuona mtu huyu kuwa alikuwa mbali mno na dini, hivyo asingejali maslahi ya imani zao. Lakini baada ya kuwa Rais, yote hayo yamefutika.
Kinachoshuhudiwa ni uwezo mkubwa wa kuendesha nchi ambao, kwa mtazamo wangu unaozingatia rekodi za Marais wote waliopita, umepiku ule wa watangulizi wake. Inahitajika makala maalum ya kueleza nini ambacho Marais wajao wanaweza kujifunza kwa Rais Kikwete.

Mhe. Lowassa kama mtu wa karibu wa JK huenda amejifunza mengi kama si yote. Utumishi wake kama Rais unaweza kusalimika na hisia za visasi na kutawaliwa na maungwana ya kuwashangaza watu. Huenda Mheshimiwa huyo ana kazi ya ziada ya kujisafisha na kuliondolea Taifa wasiwasi juu ya siasa za visasi.

Kwa Lowassa, Urais utakuwa na umuhimu mkubwa wa kusafisha haiba yake. Huenda anasaka urais, pamoja na mambo mengine, kuonesha usafi na uadilifu wake kinyume na picha ya Richmond iliyomshushia heshima chambilecho mwenyewe siku alipojiuzulu. Dalili nyingi zinaonesha kuwa Lowassa amekamia kupata Urais.

Kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya CCM hivi karibuni kilitawaliwa na tetesi kuwa moja ya ajenda zake ingelikuwa ni kuwaadhibu wale walioonywa lakini ‘wasionyeke' juu ya pilikapilika zao za kutafuta Urais 2015.

Lakini hadi mwisho wa kikao hakukuwa na taarifa za kuadhibiwa MwanaCCM yeyote yule. Kinyume chake, kana kwamba kikao hicho kimehalalisha jambo hilo, Mtu mzito Serikalini, Mhe. Waziri Mkuu naye ameripotiwa kutangaza azma yake ya kugombea Urais.

Mambo yalianza kuwa wazi kabisa miezi kadhaa nyuma kabla ya Chama cha Mapinduzi-CCM kuzuia kampeni za wanachama wake kujinadi kugombea Urais 2015 na kujiandalia mazingira ya kukubalika na kuchagulika ndani ya Chama na nje yake.

‘Nyepesi-nyepesi' zilidai na zinaendelea kudai kuwa Lowassa amejipanga sawasawa kwa ajili ya Urais wa 2015. Kwamba ametenga bajeti ya kutosha kwa ajili hiyo.

Kama ilivyokwishaelezwa, kazi kubwa ambayo atakuwa nayo mheshimiwa huyu ni ya kujisafisha na kashfa iliyomsukuma kujiuzulu wadhifa wake mkubwa. Itabidi aweke mambo hadharani ni namna hakuhusika na kashfa ile.

Hii labda itarejesha imani kwa Wajumbe wa Chama chake ili kuvuka ndani ya chama, na kwa wananchi kwa ujumla ili kupata kura za ushindi dhidi ya wagombea wa vyama vingine.

Wapinzani wanadhani kuwa akisimama Lowassa kwa tiketi ya chama chake, basi kazi ya kukiangusha chama hicho itakuwa nyepesi kwa kutumia " ile kashfa."

Benard Membe

Lakini fununu nyingine ni kwamba, Mheshimiwa Benard Camillius Membe naye kajipanga vizuri. Na tayari ameshaaga kwao. Hatua ya kuaga ni ishara ya uhakika kuwa mambo yatakuwa mazuri.

Yasemekana Waziri huyu ana sifa mbili za kumfagilia. Mosi, ‘ushemeji', na pili Uwaziri wa Mambo ya Nje. Katika sifa ya kwanza yasemekana ‘dada' kapania ‘kaka' awe Rais. Na ‘mpwa' wake wa kambo anasapoti kwa nguvu.

Na katika sifa ya pili, rekodi inaonesha kuwa wasifu wa Marais wawili wa Mwisho umejumuisha Uwaziri wa Mambo ya Nje. Mhe. Benjamin William Mkapa alitumikia wizara hiyo kwa muda mrefu, na Rais Jakaya Kikwete halikadhalika.

Kama sifa hiyo ina kisimati cha Urais, basi Membe kaupata. Lakini wadadisi wa siasa za Urais wanakosa imani ya moja kwa moja kwa mheshimiwa huyu kwani hana rekodi kubwa nje ya Uwaziri wa Mambo ya Nje.

Wengi wao hawataki siasa za majaribio. Mheshimiwa huyu ana kibarua kizito cha kuonesha jinsi anavyoijua nchi yake, na anavyoyajua matatizo ya Watanzania.

Lowassa Vs Membe

Kwa fununu zilizopo, hawa ndio walioanza kushindana japo muda bado sana wa kutoa fursa kwa wengine. Wakati Lowassa amekuwa zaidi "mzee wa mshiko", Membe amekuwa kama Simba mwendapole.

Kila mmoja anajaribu kiaina kujijengea mustakabali wa ushindi. Ni vigumu kuainisha shughuli za watafuta-Urais kama ni kampeni za 2015 lakini kile kinachofanyika hata kama hakina nia na lengo hilo ndio tayari kinamjenga mtu.

Membe ana kazi kubwa ya kuishinda nguvu ya Lowassa ambayo imejitokeza kila kipindi cha kutafuta mgombea Urais wa chama chao. Labda ‘silaha' muhimu ya kumzima Lowassa ni Ripoti ya Mwakiyembe iliyomdondosha madarakani.

Hata hivyo, CCM ina watu wengi wenye sifa za kugombea Urais labda wakati haujawafichua. Huenda wakati ukifika watafichuka, lakini kanuni ya mwendo husema aliyeanza kaanza.

Hao wenye dhamira wasiendelee kuusubiri muda bali wauwahi! Kwa mjibu wa kichwa kikubwa cha Habari kuu ya gazeti hili toleo lililopita, kuna mzito anayetajwa kufaa kuwa Rais wa 2005.

Huyu ni mtu ambaye chama chake kimepata uhai muda mfupi tu baada ya kushika nafasi ya utendaji. Abdurahman Kinana haonekani kuwa na nia ya kugombea Urais lakini uchapakazi wake unatosha kabisa kuusukuma Umma kumshawishi Mtanzania na Mzalendo huyu kuchukua fomu ili Taifa lirudishe nidhamu ya uwajibikaji.

Wanaosema Tanzania itakuwa "Somalia B" Kinana akiwa Rais si wazalendo, na ni watu wanaoshindwa kutofautisha' uanajeshi' na uwajibikaji. Kinana haendeshi chama kijeshi bali anatumia nidhamu ya uwajibikaji kukijenga chama chake na kurejesha imani ya Watanzania juu ya chama hicho.

Kwa maana hiyo, akiwa Rais, nchi haitaendeshwa kijeshi bali itatawaliwa na nidhamu ya uwajibikaji ambayo tayari huko nyuma ilishaundiwa mafagio ya vyuma bila mafanikio.

Dkt. Salim Ahmed Salim ni kada ambaye bado umri unamruhusu kugombea. Bado "kijana" ukimlinganisha na Mzee wa ZANU-PF. Ama Dkt. Salim au Dkt Shein, mmojawapo anaweza kuwa na turufu ya "zamu ya Wazanzibari" Urais wa Muungano. Yasemekana moja ya kero za Muungano japo haitajwi sana ni kupitiliza kwa zamu ya Bara katika Urais wa Muungano.

Baada ya Mkapa wa Bara ilikuwa aje Mzanzibari. Lakini akaja tena M-bara. Kwa hiyo, Bara sasa yatosha! Wakae kando kumpisha Mzanzibari. Anayepewa nafasi kubwa zaidi ni Dkt. Shein.

Lakini damu mpya kama si changa ya makada nayo pia ipo. Baada ya vijana kufanya vizuri katika majaribio ya madaraka ya uwaziri, sasa wanajiamini kuwa wanaweza kuchukua fomu ya Urais mwaka 2015.

Hapana shaka vijana hawa wana ushawishi zaidi katika makundi ya makada wanaounda mkutano mkuu wa kuamua kwa kura zao nani awe mgombea Urais. Lakini si vijana wote wanaotajwa kuwa na dhamira ya wazi ya kugombea Urais. Ni kijana wa Bumbuli tu ndiye anayesemekana kupasha? Vijana wanaona mbona Kabila kaweza tena katika nchi yenye vita!

Natamani CCM waseme, 2015, Urais ni zamu ya Vijana kama walivyomwambia mzee Sitta, "2010 Uspika zamu ya Wanawake!" Lakini "Urais 2015 zamu ya Wanawake hapana! Hapana! Hapana!" Na ndio maana sikumtaja mwanamke yoyote yule katika makala hii!

Wengine wanasema Edward Hosea itabidi ajipange kwelikweli na kupiga kambi Dodoma kwani Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama watakwenda kufanya biashara
 
Umenikuna maana mie nilipenda Salimu awe Rais ila kura hazikutosha kutokana na sunami. Ila umaarufu huwa una shida zake kwa utawala wa kisheria maana watz hatujasitarabika kivile.

Rafiki wa rais anaweza kungáng'ánia kujenga kwenye chanzo cha maji akijua na kusema hakuna wa kumzuia.

Mie huwa nawaogopa wenye Team kubwa nafikiri hata watanzania wengi ndio maana madogo yalikuwa na nafasi kubwa ya kutoa rais.
 
Abadilike wakati wa kutafuta urais,mnafiki tu, Lowasa ,Membe out kwa maslai ya chama na taifa kwa ujumla.
 
Mwaka huu asiye na makundi ndani ya CCM na amewatumikia watanzania kila sehemu ya nchi hii ndo atapitiswa kuwa rais.

Habari ya do hiyo,na kama una makundi pole sana.
 
babu wa genge la wezi atavuna alichopanda,ailyoyafanya na anayotaka ukufanya kwa awa ndo kiama chake

1,Mwakyembe -nyonyoa ngozi
2 Mwandosya -nyonyoa ngozi
2,Makongoro -kili
3,Mangula -sumu
4,Kikwete - kumvua wenyekiti wa ccm

mpe pole
 
Hongera kwa ufafanuzi lakini umesahau kwamba pamoja na yote linapokuja suala la mstakabali wa kuchukuwa mamlaka ya nchi kuliko ccm wakose mmlaka hayo ni bora wakubaliane hata kwa kupeana ulaji.
 
Hii ni taarifaya lini? Naona kama imepitwa na muda. Yaani unaongelea Salimu na Shein leo? Au umesahau!!!
 
Kwel huyu jamaa huenda hayupo nchin! kisasi hakuna aliyemkosea el ye ndo wa kulipwa ksas! kawakosea weng!
 
Last edited by a moderator:
Mamvi makazi yake ya kudumu yatakuwa ICU kuanzia 12.07.2015
 
kweli ndani ya makengeza ni shida!! tutaona mwisho wa wanafiki tu!! maaana mmeanza kwa visasi.
 
Inawezekana kabla ya hiyo date 12,ww ukawa kwenye friji au umeishasahaulika kabisa
 
umesema ukweli lakn wamechelewa sana kumzuia edward ameshafika ndan na analeta taharuki iv nikuulize mwanachama 879000+ waliomdhamini na wenyeviti wa mikoa zaidi ya 15 its means hana haja tena ya kampeni nipe wadhamini wa membe(sijui) UKIJUMLISHA WADHAMIN WA WATIA NIA WOTE UFIKI 224800 AMBAYO NI ROBO YA LOWASSA sasa utamzuiaje tena labda chuki binafsi tu na lowassa hilo
My take:KIKWETE ALISHINDWA KUMUANDAA MRITHI WAKE NA LOWASSA AMETOKEA HAPO NA AMESHAWAZIDI NAAMINI KIKWETE MWENYEWE HAAMINI KINACHOTOKEA
 
Ni vigumu kama si muhali kujua kwa uhakika nani atakuwa Mrithi wa Rais Kikwete au pia tuseme Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ugumu huo unatokana na ukweli kuwa Siasa za ndani ya vyama na siasa za ushindani ndizo zitakazoamua.

Kwa upande wa Siasa za ndani ya Vyama, CCM ina nidhamu yake ya kupokezana madaraka kila baada ya kipindi cha muongo mmoja. Vumbi hutimka kwelikweli pale Rais kutoka chama hicho anapomaliza muda wake kwani wanachama wote huwa huru kuchukua fomu ya kugombea Urais.

Ukitembea ndani ya fikra za wana-CCM, unaweza kukuta kila mtu hana jawabu la kitendawili cha nani atakuwa mgombea wa chama hicho. Siasa za ndani maana yake ni mchujo wa majina ya watakaoomba kugombea nafasi ya Urais.

Kamati Kuu ya CCM ndiyo yenye dhamana ya kuchuja wagombea. Ni vigumu kutabiri nani atachujwa, na nani atapita. Ukiitazama nguvu ya Kamati Kuu ya CCM unaweza kusema labda Mwenyekiti wa CCM-Taifa anaweza kuwa na uhakika wa kiasi fulani nani atakuwa mgombea wa kumrithi yeye mwenyewe katika nafasi ya Urais.

Kwamba labda yeye pekee tayari anaye Rais ajae kichwani mwake. Lakini bado mazingira yanaweza kulipiga kumbo wazo lake kwani hata Mkapa huenda alikuwa na ‘Rais’ wa kumrithi kichwani mwake lakini mwisho wa siku JK ambaye hakuwa kichwani mwake akawa Rais.

Si ukweli wa kuficha kuwa Dkt. Salim alikuwa na nafasi kubwa vichwani mwa wazito wa chama hicho. Kumbe basi, hata katika siasa za ndani bado nako kuna kitendawili.

Kwa upande wa siasa za ushindani, zenyewe ziko za aina mbili; mosi ushindani wa kupata kura za kutosha za Wajumbe wa Mkutano Mkuu, na pili, ushindani wa kupata kura za wananchi.

Kwa imani ya CCM, ushindani wa kupata kura za Wajumbe wa Mkutano Mkuu ni mgumu mno kuliko ule wa kupata kura za wananchi. Kwa mtazamo wao, kupata ushindi wa kura za wajumbe ndio tayari kuna maana ya kupata Urais.

Kwamba siasa za ushindani wa nje ya chama dhidi ya vyama vya upinzani kwao si tatizo sana. Makala hii itajikita zaidi katika siasa hizo za ndani za CCM na ushindani wake.

Binafsi sina uhakika na demokrasia ya Kamati Kuu ya CCM ndiyo maana naita “siasa za ndani”. Kama ni mtu mmoja au watu wachache wanaoamua nani awe mgombea wa chama, hilo ni gumu kujadilika.

Lakini ‘weupe’ wa demokrasia ya chama huanza kuonekana pale mambo yanapotoka ndani ili Wajumbe wa Mkutano Mkuu ‘wamaliza kazi’. Mwaka 1995, kidogo demokrasia ilikuwa na ‘wingu’ la Butiama, Mwalimu wa Pugu aliishikia fimbo demokrasia kuhakikisha kuwa ‘mtu wake’ anapita.

Ushindani wa 2005 bila ‘Wingu la Butiama’

Lakini mwaka 2005, demokrasia ilitakata kwani ‘wingu la Butiama’ halikuwepo tena. Wadadisi wa siasa za CCM wanasema laiti ‘wingu’ lile la Butiama lingeendelea kuwepo mwaka 2005, basi Dkt. Salim angepata Urais. JK angeendelea kusubiri, na angeenguliwa mapema ili kuokoa nafasi ya Salim mikononi mwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu.

Kwa kutoweka wingu, bila kutarajia, Jakaya Kikwete akamshinda mtu aliyepewa nafasi kubwa ya ushindi, Dkt. Salim Ahmed Salim. Laiti Kikwete ‘angekula panga’ la Kamati Kuu, Salim angekuwa Rais wa Nne wa Tanzania.

Lakini wengine walisema laiti ‘embe bivu’ lisingekatwa panga la Kamati Kuu, basi ushindani wa JK na Malechela ungekuwa mkubwa zaidi kuliko ule wa JK na Salim ambapo kura za ushindi kwa JK zilikuwa nyingi mno.

Mazingira ya safari hii hayajaonesha nani na nani wanaweza kutikisa siasa za CCM lakini watabiri wa mambo ya siasa tayari wanasema kuwa kama panga la Kamati Kuu ‘litamkosa’ mzee wa Monduli, halafu uamuzi wa mwisho waachiwe wajumbe wa Mkutano Mkuu, basi Edward Ngoyai Lowassa ana nafasi kubwa ya kupeperusha Bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa 2005.

Edward Lowassa

Kuna aina mbili za vikwazo kwa Mhe. Edward Lowassa; mosi, wapo wanaoogopa kuwa Lowassa ana maamuzi makali na anaweza kulipa visasi jambo ambalo litakuwa na maana kuwa wajumbe wa iliyokuwa Kamati ya Richmond iliyomporomosha Waziri Mkuu watafute pa kuishi endapo mwanaCCM huyo atakuwa Rais.

Siasa hizo za visasi ni hatari kwa nchi na wananchi. Hivyo busara ya Kamati Kuu inaweza kuliepushia Taifa janga la siasa za visasi. Pili, wapo wanaoamini kuwa Lowassa ana kashfa mbaya ambazo zimewakera wananchi wengi, na akisimama kugombea urais, CCM itakuwa imejimaliza yenyewe!

Hivyo, busara ya Kamati Kuu inaweza kukinusuru chama kwa kukata jina la Lowassa. Lakini wengine wanasema Urais ni mamlaka yanayozunguukwa na washauri wengi.

Rais hawezi kukurupuka bila ushauri. Hivyo, hata akiwa Rais, bado Lowassa hawezi kuamua atakavyo. Wengine wanasema urais ‘unashepu’ saikolojia ya mtu. Wengi wanatoa mfano wa Rais Kikwete kwamba ni mtu aliyebadilika mno kwa siasa za Urais tofauti kabisa na alivyokuwa Waziri.

Baadhi ya waliotaka kumkataa asiwe Rais waliitazama zaidi haiba yake alipokuwa Waziri. Wapo waliomuona kama ni mtu mwenye kujinata ambaye hata marafiki wa karibu walipotaka msaada wake Wizarani waliishia getini.

Wapo walioona kuwa ujana ulimzidi sana hivyo Ikulu isije kugeuka ukumbi wa disko! Wapo waliomuona mtu huyu kuwa alikuwa mbali mno na dini, hivyo asingejali maslahi ya imani zao. Lakini baada ya kuwa Rais, yote hayo yamefutika.
Kinachoshuhudiwa ni uwezo mkubwa wa kuendesha nchi ambao, kwa mtazamo wangu unaozingatia rekodi za Marais wote waliopita, umepiku ule wa watangulizi wake. Inahitajika makala maalum ya kueleza nini ambacho Marais wajao wanaweza kujifunza kwa Rais Kikwete.

Mhe. Lowassa kama mtu wa karibu wa JK huenda amejifunza mengi kama si yote. Utumishi wake kama Rais unaweza kusalimika na hisia za visasi na kutawaliwa na maungwana ya kuwashangaza watu. Huenda Mheshimiwa huyo ana kazi ya ziada ya kujisafisha na kuliondolea Taifa wasiwasi juu ya siasa za visasi.

Kwa Lowassa, Urais utakuwa na umuhimu mkubwa wa kusafisha haiba yake. Huenda anasaka urais, pamoja na mambo mengine, kuonesha usafi na uadilifu wake kinyume na picha ya Richmond iliyomshushia heshima chambilecho mwenyewe siku alipojiuzulu. Dalili nyingi zinaonesha kuwa Lowassa amekamia kupata Urais.

Kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya CCM hivi karibuni kilitawaliwa na tetesi kuwa moja ya ajenda zake ingelikuwa ni kuwaadhibu wale walioonywa lakini ‘wasionyeke’ juu ya pilikapilika zao za kutafuta Urais 2015.

Lakini hadi mwisho wa kikao hakukuwa na taarifa za kuadhibiwa MwanaCCM yeyote yule. Kinyume chake, kana kwamba kikao hicho kimehalalisha jambo hilo, Mtu mzito Serikalini, Mhe. Waziri Mkuu naye ameripotiwa kutangaza azma yake ya kugombea Urais.

Mambo yalianza kuwa wazi kabisa miezi kadhaa nyuma kabla ya Chama cha Mapinduzi-CCM kuzuia kampeni za wanachama wake kujinadi kugombea Urais 2015 na kujiandalia mazingira ya kukubalika na kuchagulika ndani ya Chama na nje yake.

‘Nyepesi-nyepesi’ zilidai na zinaendelea kudai kuwa Lowassa amejipanga sawasawa kwa ajili ya Urais wa 2015. Kwamba ametenga bajeti ya kutosha kwa ajili hiyo.

Kama ilivyokwishaelezwa, kazi kubwa ambayo atakuwa nayo mheshimiwa huyu ni ya kujisafisha na kashfa iliyomsukuma kujiuzulu wadhifa wake mkubwa. Itabidi aweke mambo hadharani ni namna hakuhusika na kashfa ile.

Hii labda itarejesha imani kwa Wajumbe wa Chama chake ili kuvuka ndani ya chama, na kwa wananchi kwa ujumla ili kupata kura za ushindi dhidi ya wagombea wa vyama vingine.

Wapinzani wanadhani kuwa akisimama Lowassa kwa tiketi ya chama chake, basi kazi ya kukiangusha chama hicho itakuwa nyepesi kwa kutumia “ ile kashfa.”

Benard Membe

Lakini fununu nyingine ni kwamba, Mheshimiwa Benard Camillius Membe naye kajipanga vizuri. Na tayari ameshaaga kwao. Hatua ya kuaga ni ishara ya uhakika kuwa mambo yatakuwa mazuri.

Yasemekana Waziri huyu ana sifa mbili za kumfagilia. Mosi, ‘ushemeji’, na pili Uwaziri wa Mambo ya Nje. Katika sifa ya kwanza yasemekana ‘dada’ kapania ‘kaka’ awe Rais. Na ‘mpwa’ wake wa kambo anasapoti kwa nguvu.

Na katika sifa ya pili, rekodi inaonesha kuwa wasifu wa Marais wawili wa Mwisho umejumuisha Uwaziri wa Mambo ya Nje. Mhe. Benjamin William Mkapa alitumikia wizara hiyo kwa muda mrefu, na Rais Jakaya Kikwete halikadhalika.

Kama sifa hiyo ina kisimati cha Urais, basi Membe kaupata. Lakini wadadisi wa siasa za Urais wanakosa imani ya moja kwa moja kwa mheshimiwa huyu kwani hana rekodi kubwa nje ya Uwaziri wa Mambo ya Nje.

Wengi wao hawataki siasa za majaribio. Mheshimiwa huyu ana kibarua kizito cha kuonesha jinsi anavyoijua nchi yake, na anavyoyajua matatizo ya Watanzania.

Lowassa Vs Membe

Kwa fununu zilizopo, hawa ndio walioanza kushindana japo muda bado sana wa kutoa fursa kwa wengine. Wakati Lowassa amekuwa zaidi “mzee wa mshiko”, Membe amekuwa kama Simba mwendapole.

Kila mmoja anajaribu kiaina kujijengea mustakabali wa ushindi. Ni vigumu kuainisha shughuli za watafuta-Urais kama ni kampeni za 2015 lakini kile kinachofanyika hata kama hakina nia na lengo hilo ndio tayari kinamjenga mtu.

Membe ana kazi kubwa ya kuishinda nguvu ya Lowassa ambayo imejitokeza kila kipindi cha kutafuta mgombea Urais wa chama chao. Labda ‘silaha’ muhimu ya kumzima Lowassa ni Ripoti ya Mwakiyembe iliyomdondosha madarakani.

Hata hivyo, CCM ina watu wengi wenye sifa za kugombea Urais labda wakati haujawafichua. Huenda wakati ukifika watafichuka, lakini kanuni ya mwendo husema aliyeanza kaanza.

Hao wenye dhamira wasiendelee kuusubiri muda bali wauwahi! Kwa mjibu wa kichwa kikubwa cha Habari kuu ya gazeti hili toleo lililopita, kuna mzito anayetajwa kufaa kuwa Rais wa 2005.

Huyu ni mtu ambaye chama chake kimepata uhai muda mfupi tu baada ya kushika nafasi ya utendaji. Abdurahman Kinana haonekani kuwa na nia ya kugombea Urais lakini uchapakazi wake unatosha kabisa kuusukuma Umma kumshawishi Mtanzania na Mzalendo huyu kuchukua fomu ili Taifa lirudishe nidhamu ya uwajibikaji.

Wanaosema Tanzania itakuwa “Somalia B” Kinana akiwa Rais si wazalendo, na ni watu wanaoshindwa kutofautisha’ uanajeshi’ na uwajibikaji. Kinana haendeshi chama kijeshi bali anatumia nidhamu ya uwajibikaji kukijenga chama chake na kurejesha imani ya Watanzania juu ya chama hicho.

Kwa maana hiyo, akiwa Rais, nchi haitaendeshwa kijeshi bali itatawaliwa na nidhamu ya uwajibikaji ambayo tayari huko nyuma ilishaundiwa mafagio ya vyuma bila mafanikio.

Dkt. Salim Ahmed Salim ni kada ambaye bado umri unamruhusu kugombea. Bado “kijana” ukimlinganisha na Mzee wa ZANU-PF. Ama Dkt. Salim au Dkt Shein, mmojawapo anaweza kuwa na turufu ya “zamu ya Wazanzibari” Urais wa Muungano. Yasemekana moja ya kero za Muungano japo haitajwi sana ni kupitiliza kwa zamu ya Bara katika Urais wa Muungano.

Baada ya Mkapa wa Bara ilikuwa aje Mzanzibari. Lakini akaja tena M-bara. Kwa hiyo, Bara sasa yatosha! Wakae kando kumpisha Mzanzibari. Anayepewa nafasi kubwa zaidi ni Dkt. Shein.

Lakini damu mpya kama si changa ya makada nayo pia ipo. Baada ya vijana kufanya vizuri katika majaribio ya madaraka ya uwaziri, sasa wanajiamini kuwa wanaweza kuchukua fomu ya Urais mwaka 2015.

Hapana shaka vijana hawa wana ushawishi zaidi katika makundi ya makada wanaounda mkutano mkuu wa kuamua kwa kura zao nani awe mgombea Urais. Lakini si vijana wote wanaotajwa kuwa na dhamira ya wazi ya kugombea Urais. Ni kijana wa Bumbuli tu ndiye anayesemekana kupasha? Vijana wanaona mbona Kabila kaweza tena katika nchi yenye vita!

Natamani CCM waseme, 2015, Urais ni zamu ya Vijana kama walivyomwambia mzee Sitta, “2010 Uspika zamu ya Wanawake!” Lakini “Urais 2015 zamu ya Wanawake hapana! Hapana! Hapana!” Na ndio maana sikumtaja mwanamke yoyote yule katika makala hii!

Wengine wanasema Edward Hosea itabidi ajipange kwelikweli na kupiga kambi Dodoma kwani Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama watakwenda kufanya biashara

Umesema ukweli lakini wamechelewa sana kumzuia Edward ameshafika ndani na analeta taharuki.

Hivi nikuulize mwanachama 879000+ waliomdhamini na wenyeviti wa mikoa zaidi ya 15 it means hana haja tena ya kampeni nipe wadhamini wa Membe(sijui) UKIJUMLISHA WADHAMIN WA WATIA NIA WOTE UFIKI 224800 AMBAYO NI ROBO YA LOWASSA sasa utamzuiaje tena labda chuki binafsi tu na Lowassa anafahamu hilo.

My take: KIKWETE ALISHINDWA KUMUANDAA MRITHI WAKE NA LOWASSA AMETOKEA HAPO NA AMESHAWAZIDI NAAMINI KIKWETE MWENYEWE
HAAMINI KINACHOTOKEA.
 
Safari ya matumaini ilianza mara tu baada ya uchaguzi mkuu wa 2005 kumalizika - kujairibu kuizuia kwa sasa ni sawa na kuzuia mafuriko kwa mikono!!

CCM kazi pevu!!
 
Ule usemi wa aliyepata wadhamini wengi (ENL) ndiye anaweza kutoka unaweza kutimia? Kigezo hiki kinaonekana kuwafurahisha wengi, vigezo vingine kwa CCM hivi sasa hakuna anayevijali labda Mangula peke yake ndiye ana ajenda ya siri.
 
Mwaka huu asiye na makundi ndani ya CCM na amewatumikia watanzania kila sehemu ya nchi hii ndo atapitiswa kuwa rais.

Habari ya do hiyo,na kama una makundi pole sana.

Hapo ndo anakuja Magufuli...
 
KWA TAARIFA YAKO hao wadhamini 879000+ni feki angalia card zao zimenunuliwa lini na wamelipia wapi mfano iringa data base inasema kuna wanachama 26,000 yeye alipata 58,000 sasa anataka kutudanganya watu wazima na akili zetu.
na tena chama inabidi kiangalie huyu jamaa ana malengo yake kwa kua anajua hana sifa "kwa mujibu wa msekwa juzi CLOUDS RADIO"anahangaika kutengeneza wanachama wake kusudi akiondoka aanze kupokea hizo card na ninawahakikishia hii post mtaikumbuka
 
Back
Top Bottom