Lowassa akataza wanachama kuhama CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa akataza wanachama kuhama CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tume ya Katiba, May 11, 2012.

 1. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Wadau, tupate taarifa toka kwa mweshimiwa sana ndugu EL

  MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa amekuwa akifanya mikutano ya ndani na ya hadhara jimboni humo katika kinachoonekana ni kuzima wimbi lililoibuka hivi karibuni la wanachama wa CCM kuhamia Chadema.

  Tangu kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa Mkoa wa Arusha, James ole Millya, limekuwapo wimbi la wana CCM kuhamia Chadema katika mikoa kadhaa nchini.

  Mbali na Millya, wanachama wa CCM wakiwamo viongozi wenye nafasi za udiwani, walitangaza kuhamia Chadema ambayo moja ya ngome zake ni Arusha iliko na wabunge wawili; Arumeru Mashariki na Karatu.

  Chadema pia ilikuwa ikiongoza Jimbo la Arusha Mjini kabla ya matokeo yake kutenguliwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kutokana na kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu wa CCM.

  Lowassa alifanya mikutano ya ndani jana eneo la Mto wa Mbu na wa hadhara, ambako aliwaambia wananchi, kwamba pamoja na kuwa suala la kujiunga na chama chochote cha siasa ni haki ya yeyote, lakini haoni umuhimu wa wanaCCM kuhama sasa.

  Mbunge huyo ambaye alikuwa Waziri Mkuu katika miaka ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Nne hadi alipojiuzulu Februari 2008, alisema CCM ni chama kinachotetea maslahi ya wanyonge na wananchi wa hali ya chini, hivyo akawataka kutathmini katika kipindi chote tangu Uhuru kama CCM imeshindwa kulitimiza hilo.

  Aidha, alisema chama hicho kimekuwa kikitekeleza kwa vitendo mchango wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambao ni umoja na mshikamano, vinavyoifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani.

  Mwanasiasa huyo ambaye katika jamii ya Wamasai anaheshimika kwa kuwa kiongozi wao mkuu wa kimila, alisema CCM ni chama ambacho kimekuwa kikitetea maslahi na rasilimali za nchi kutoporwa na wageni.

  Aliwaeleza kuwa CCM ni chama kinachotoa nafasi kwa wanachama wake kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa bila mizengwe ya ubaguzi wa rangi, ukabila au udini.

  Aidha, alisisitiza kuwa chama hicho kina utaratibu wa kujisahihisha makosa kwa kufuata vikao halali, hivyo kwa msingi huo, aliwataka wanachama wanaofikiria kuhama, kutathmini ili wasije kujuta mbele ya safari.

  Naye Jasmine Shamwepu anaripoti kutoka Dodoma kuwa CCM imefanya maandamano ya kupinga kauli ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), wakisema ni za kibaguzi na zinaweza kuleta machafuko.

  Maandamano hayo yalifanyika mjini humo, huku wana CCM wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali ukiwamo wa "Chadema wanataka kutengana bora watengane wao na familia zao kuliko kuigawa nchi ambayo ina amani."

  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake (UWT), Amina Makilagi alisema CCM wanaamini nchi imezoea umoja na mshikamano na kama Chadema hawataki amani, basi wasilete machafuko ambayo yanaweza kuleta mgawanyiko usiokuwa na maana yoyote.

  Makilagi alifafanua kuwa kauli iliyotolewa na Nassari kwamba Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wasifike Ukanda wa Kaskazini, ni dhamira yake wala si kwa bahati mbaya.

  Hata hivyo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kauli hiyo iliyojaa utoto ni ya Nassari binafsi na si ya chama hicho.

  "Mwaka 2005 na 2010 katika kampeni zao za uchaguzi, walitangaza kuwa lazima damu imwagike na sasa dhamira yao imeanza kwa kutoa kauli za uchochezi ambazo zinaweza kuleta machafuko," alisema Makilagi.

  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Martini Shigela alimtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa kuchukua hatua kwa kutolea maelezo kuhusu kauli hiyo ya Nassari ambayo inaweza kuleta machafuko na kugawa Watanzania.

  "Msajili anatakiwa achukue hatua na asilinyamazie suala hili, kwani ni kubwa na ni kitendo cha kujitenga na kutaka wao wawe Jamhuri ya Kaskazini, kwa jambo hilo tayari Chadema wameshaitenga Zanzibar," alisema Shigela.


  sosi: HabariLeo | Lowassa akataza wanachama kuhama CCM
   
 2. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  CCM ni sawa na watu wanaozuia risasi kwa mikono
   
 3. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 788
  Trophy Points: 280
  Hivi jamani CCM mbona mnapenda makuu, hamna kingine cha kuongea? kauli ya Nasari imeishazungumziwa sana na ilishatenguliwa na Mh. Freeman Mbowe ile siku ya Mkutano na isitoshe Mh. Nasari ameishatoa maelezo Polisi. Hivi hakuna kitu kingine cha kuongea mimi kwa ushauri wangu mngemshinikiza Mh. Rais awawajibishe wale mawaziri walioisababishia hasara serikali yetu ili angalau chama chenu kipate heshima kidogo lakini sio kushughurika na kauli ya Mh. Nasari ambayo Mtanzania yeyote ameisha itafakari na kuona haina madhara yeyote.
   
 4. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yeye anahamia CDM lini!!!.
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  It is a gimmick show.
   
 6. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu kuna watu walimzushia anahama chama ndio imebidi aje amwage sumu rasmi, maana walisahau kuwa yuko fit kwa mapambano
   
 7. d

  dizzle1 Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  KAZI KWELI KWELI....Mh LOWASSA ANATAKIWA AZUNGUKE NCHI ZIMA KAMA ATAWEZA CONVICE RAIA JUU YA AMSHA AMSHA YA CDM.KWA MONDULI PEKEE ANAPOTEZA MUDA.BORA AENDE AKALALE TU....
   
 8. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa amekuwa akifanya mikutano ya ndani na ya hadhara jimboni humo katika kinachoonekana ni kuzima wimbi lililoibuka hivi karibuni la wanachama wa CCM kuhamia Chadema....!
   
 9. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  issue ya nassari sasa inaingiaje humu??
   
 10. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  :biggrin1::biggrin1::biggrin1::biggrin1: nimeipenda hii
   
 11. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160


  Hakiamama atahamia siku si nyingi!

  Mbona juzi alizuiwa kutoa tamko lake?
  Ngoja iko siku si nyingi atatoa tamko lake na hapo wanaccm mtajua kilichonyoa kanga ndege manyoa ya shingo.

  Eti watu wasiihame chichiem????
  Ina nini jipya.
   
 12. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Lowassa mwenye hayupo CCM sasa hii huruma yatoka wapi au yeye na JK wameamua kuzika tofauti zao? Au sanaa na unafiki? Penye udhia penyeza rupia.
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ccm wanafanya maandamano kwaajili ya nassary? Mbona ni kitu kidogo saaaaana!!! Sasa Kama CDM wangefanya maandamano kwa kauli za lusinde na ole sendeka si ingekuwa vichekesho? Kweli ccm wamekalia mipasho.
   
 14. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Yeye apambane na Magamba wenzake...
  Sisi tunaendelea kuvuna mtaji wa kura za mwaka 2015.
   
 15. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Lowassa, acha uzumbukuku, ccm kumebaki nini mpaka ukataze watu wasihame? Waache watu wahame toka pango la wanyang'anyi, ili wapate ukombozi wa kifikira, kimtizamo, kimaslahi na kiuchumi. Watu wanatafuta ukombozi toka mkoloni mweusi ccm, wanakimbilia CDM waache bhana!
   
 16. Kumbakumba

  Kumbakumba JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napata tabu sana..bado katika nchi hii kuna mwanasiasa anasimama na kuwalaghai wananchi na tunajivunia amani,utulivu mshikamano na blah blah kama hizo?huu ni ukichaa au ni nn?watz wanahitaji zaidi ya hivi..came ooooon!
   
 17. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Waziri mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowasa anafanya mikutano ya ndani ya chama chake kuwashawishi wananchi jimboni humo wasikihame chama hicho.
  Source: Mwananchi
  Naona M4C inawatia kiwewe magamba
   
 18. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Si aliwaambia yeye watangulie?
   
 19. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Amegundua waliotangulia wameondoka mazima na kumwacha kwenye mataa. Kimbunga cha m4c na operation vgvg vinawawewesesha vibaya magamba. Homa imepanda hadi kwa Gamba kuu!
   
 20. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]MBUNGE wa Monduli, Edward Lowassa, amekuwa na mikutano ya ndani katika jimbo lake katika kile kinachoonekana kuwa ni jitihada za kutuliza wimbi la wana CCM kuhamia Chadema.

  Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wanaCCM katika mikoa mbalimbali kuhamia Chadema. Mkoa wa Arusha ndiyo unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanachama wa CCM wanaojiunga na Chadema.
  Jana Lowassa ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu kabla ya kujiuzulu, alifanya mkutano wa ndani katika eneo la Mto wa Mbu na baadaye kufuatiwa na mkutano wa hadhara.

  Katika mkutano huo wa hadhara, mbunge huyo aliwaambia wananachi kuwa pamoja na kuwa suala la kujiunga na chama chochote cha siasa ni haki ya mtu, lakini haoni umuhimu wa wana CCM kwa sasa kuhama chama hicho kinachotawala.

  Alisema CCM ni chama chenye kutetea maslahi ya wanyonge na kwamba kuna haja kwa wananchi kutathimini ili kuona kama kweli CCM imeshindwa kutimiza malengo yake.


  Alisema CCM imekuwa ikitekeleza kwa vitendo mchango wa Baba wa Taifa Mwalimu Jiulius Nyerere ambao nni umoja na mshikamano, vinavyoifanya Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani.
  Lowassa pia alisema CCM ni chama kinachotetea maslahi na rasilimali za nchi ili zisiporwe na wageni.

  Amewakumbusha kuwa CCM ni chama kinachotoa nafasi kwa wanachama wake kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa bila ya mizengwe au ubaguzi wa rangi, ukabila au dini.
  Source: Mwananchi
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...