Lowassa akataza wanachama kuhama CCM

Lowassa akataza wanachama kuhama CCM

mkuu mleta mada umenichanganya, habar unayotuletea ni ya lowasa au maandamano ya ccm? Mbona taarfa zenyewe hazilandani...? Kuhusiana na taarfa ya lowasa kuna mtu alisema hivi "ni ngumu kuyazuia mafuriko"
 
''Lowassa pia alisema CCM ni chama kinachotetea maslahi na rasilimali za nchi ili zisiporwe na wageni''.Nimecheka mpaka karibu nipasuke,hivi bado kuna watanzania wanadanganyika kwa kauli za kifedhuli kama izi,kila mtu anaona kinachoendelea jinsi wageni wanavyoivuna nchi kama shamba la bibi alafu bila aibu unatoa kauli kama hiyo hadharani? Kingine anazuia zisipore na wageni,na je zikiporwa na wenyeji hazuii?
 
CCM inateteaje maslahi ya 'wanyonge'? uongo dhahiri!

Ufisadi wa RICHMOND,MEREMETA,UNUNUZI WA RADAR, UNUNUZI WA NDEGE YA RAIS, MIKATABA YA MADINI BOMU etc hivi vyote ndio ccm inatetea maslahi ya wanyonge? You must be outside your LOCKER!!
 
KAZI KWELI KWELI....Mh LOWASSA ANATAKIWA AZUNGUKE NCHI ZIMA KAMA ATAWEZA CONVICE RAIA JUU YA AMSHA AMSHA YA CDM.KWA MONDULI PEKEE ANAPOTEZA MUDA.BORA AENDE AKALALE TU....


Kimsingi LOWAXA, ni kama kujamba ushizi kwenye blakenti huku umejifunika gubugubi na kuuliza kuuliza wengine kama unatoa halufu mbaya.Hoja ya kuhama wana CCM si wimbi, bali ni ukweli kuwa watu wamechoka ghiriba, za kuwadaganya maisha bora huku wakiendelea kuteseka , na wachache kama akina maige mtoto mdogo sana kisiasa anakuwa tajiri kwa kutumia madaraka ya umma.Hoja ni lowaxa sasa yeye mwenyewe awe msafi na chama kiwe kisafi kiseme na kutenda haki na si kukumbati uozo.Serikali inalijua dhruma mbalimbali ambazo wananchi wanatendewa, na CCMwamekaa kimya na kuendekeza ulaghai wa kizamani.Haya sasa ndo madhara yake propanganda na ukweli ni vitu tofauti.na uhakika hawezi kufanya namna ham kuksiafisha chama chake bali ni kutapatapa.
 
Mkuu wangu kuna watu walimzushia anahama chama ndio imebidi aje amwage sumu rasmi, maana walisahau kuwa yuko fit kwa mapambano
Ukiona mwanaume anajinadi kuwa yeye si shoga hata mahali ambapo jambo hilo halijazungumzwa, basi huyo ni wa kuwa na wasiwasi naye.
 
Hapo kwenye Red. Lowassa amejisahau. Amesahau kuwa Arumeru Mashariki mgombea wa ccm alisimamishwa kimizengwe.
Amesahau kuwa CCM ndiyo iliyosimamia Ardhi ya watanzania kuporwa na wageni.

Jamani Lowassa vipi? Mbona anaiua CCM kwa makusudi? Au hakujiandaa kuzungumza na wananchi?

Naona huyu bwana RICHMOND amecopy na kupest moja ya statements za mwalimu Nyerere, ya miaka ya 1957 wakati akiwashaushi watu kudai uhuru kutoka kwa mkoloni mweupe. Amesahau kwamba kuna gap kubwa sana kati ya kizazi cha miaka hiyo na miaka hii ya leo. Sasa hivi watu hawadanganyiki wanajua kutofautisha mbichi na mbivu bila chenga yeyeto. Namuonea sana huruma bwana RICHMOND because he is real behind the time, and also is very very premitive and same unconcious!!!
 
Ukiwa maskini akatokea mtu akakupa sh. 500 (jero) utaona amekusaidia sana. Haya ndio maendeleo yanayoletwa na viongozi wetu. kama wote watakuwa wajanja utawala wao uko mashakani.
 
Yaani ccm inatekeleza kwa vitendo sera za baba wa Taifa?Vijana Wa mjini wanasema mateja hawanaga aibu hujiibia wenyewe alosto inapowakalia kooni.Nnaufananisha msemo huu wa maisha ya mateja na chama cha ccm,sababu ni moja tu:chama kimekosa mwelekeo na kimekiuka ile misingi Yake ya awali(enzi za baba Wa taifa mwal Jullius Kambarage Nyerere).Chama kimekuwa cha wafanya biashara/mafisadi.wanachama wake wakubwa wanakihama makada wake wakumbwa wanakisema wazi wazi bila woga.Kwa maneno haya ya Lowasa yalio kinyume na uhalisia ni sawa kabisa kukilinganisha chama hichi cha ccm na tabia ya mateja.
 
Wakuu bado natafakari haya, EL kama ni kweli anaweza kuwaambia watanzania maneno haya....kweli?..mbona anajisema yeye mwenyewe?...Lo!
 
Lowassa anaona namba ya watu watakaopewa kofia, t-shirt, khanga, vitambaa na mambo mengine wanapungua, inabidi awaombe wabaki asije akaadhirika mtu mzima. Hii ni hatari sana. CCM hawataisahau CDM. People's power kweli.
 
Aliye msafi katikati yenu na abebe jiwe ampige Lowassa.
 
Mtu yeyote atayetambua ubaya wa chama cha majambazi na ubaya wanaotufanyia lazima ahamie chadema ili apate tumaini jipya.
 
Back
Top Bottom