Lowassa aitabiria CCM Ushindi, Uchaguzi Mkuu 2015

Lowassa aitabiria CCM Ushindi, Uchaguzi Mkuu 2015

Hee, we vp, Kama hujui!!!!!!!!!ya Nini sasa Kumuita Lowasa Mstaafu!!!!!!
Huu ni Uzumbukuku Mtakatifu aisee

Namuita hivyo kwa sababu sijui sasa wewe unayejua niambie basi. Hakuna ligi hapa hiki ni kisima cha elimu toa elimu
 
Hivi mlitarajia asemeje. Mtu ana ndoto hizo kupitia huko, so asemeje? Halafu source: Jambo Leo.

Ndivyo TB JOSHUA alimuagiza? Amemrithisha utabiri. Kazi kweli....naona huyu mzee ana kihoro cha kutoshwa Kamati kuu na kwenye ulezi wa uvccm. Hakuna lingine!
 
Chadema kuingia ikulu ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano! Haitawezekana mara mia elfu kukiachia chakula cha watoto wako kwa mbwa mwenye njaa wewe mzazi utaönekana mjinga na hamnazo kichwani mwako!

Sijui 2015 mtakimbilia wapi? Na tutawatafuta tu kokote mtakapokimbilia. Kama mnaamini ccm ni tofauti sana na vyama vingine vya Afrika ambavyo vilishnang'olewa, TUTAONA!
 
Waziri Mkuu wa Zamani na Mbunge wa Monduli aliye jiuzulu kwa Kashfa ya Ufisadi,Mh Edward Ngoyai Lowassa,ametoa angalizo hilo kwa Chama cha mapindinduzi ,kwamba endapo CCM haitatekeleza kwa usahihi Maagizo na Maelekezo ya Mkutano Mkuu wa Ccm,basi itakuwa ni rahisi kwa Chama hicho kushindwa Uchaguzi ujao . aliendelea kusema kuwa Mkutano mkuu wa CCM ulitoa maelekezo mengi kwa chama hicho ili kupambana na upinzani mkali uliopo sasa hivi. Akaendelea kusema kuwa Hakika CCM isipofuata hayo maagizo Itashindwa uchaguzi ujao.
 
Huyu jamaa Lowassa anajua sana ,hali ilivyo nchni kisiasa,Hebu CCM msikilizeni mzee Wetu huyu.
 
CCM ni sikio la kufa!, halisikii dawa!, na kama ni tunda, basi ni la kuvunda halina ubani!, kama muda wa CCM kuondoka ukifika, CCM itaondoka tuu!, bahati nzuri iliyonayo CCM, ni kuendelea kuutegemea mtaji mkubwa wa ignorance ya Watanzania, hivyo 2015, tutaipa tena, na tena na tena mpaka litimie line neno kuwa CCM itatawala miaka 100 au milele kabisa!, kwa sababu Watanzania ni miongoni mwa watu majuha wa kupindukia ambao tunakwenda kinyume kabisa cha ule msemo wa "you can fool some people, sometime!, but you can't fool all the people all the time!, "We have all been fooled all times", na 2015 tutaichagua tena!. Mtakao bisha, bisheni tuu for the sake of kubisha, ila ukweli mchungu ndio huu!.
Pasco.
 
Huyu mtu mnampa sifa hasizostahili, kuna jipya gani hapo aliloongea tulikuwa hatulijui? Halafu Simpendi mimi Huyu FISADI, Na publicity INANIUDHI MNO....
 
Angeanza kujivua gamba mwenyewe kwa maslah ya chama chake mana nae ni mmoja wa matatizo ya chama. Otherwsie akae kimya hana jipya la kutuambia.
 
CCM ni sikio la kufa!, halisikii dawa!, na kama ni tunda, basi ni la kuvunda halina ubani!, kama muda wa CCM kuondoka ukifika, CCM itaondoka tuu!, bahati nzuri iliyonayo CCM, ni kuendelea kuutegemea mtaji mkubwa wa ignorance ya Watanzania, hivyo 2015, tutaipa tena, na tena na tena mpaka litimie line neno kuwa CCM itatawala miaka 100 au milele kabisa!, kwa sababu Watanzania ni miongoni mwa watu majuha wa kupindukia ambao tunakwenda kinyume kabisa cha ule msemo wa "you can fool some people, sometime!, but you can't fool all the people all the time!, "We have all been fooled all times", na 2015 tutaichagua tena!. Mtakao bisha, bisheni tuu for the sake of kubisha, ila ukweli mchungu ndio huu!.
Pasco.

Nakubaliana nawewe kuhusu ujuha mana hilo linakua reflected kwa mkuu wa kaya na familia yake, hata hvyo kuna tofauti ya kutoichagua na kuitoa madarakan. Hilo la kwanza kwa machungu tunayopata tunaeza thubutu but hilo la pili ujuha utatuzuia ukisaidiana na ile single ya amani amani. Kwamba tunaeza tusiichague CCM but ikachakachua matokeo na jinsi Amani ilivyomuhimu sana kwa watanzania wenye dhiki basi CCM itaendelea.
 
CCM ni sikio la kufa!, halisikii dawa!, na kama ni tunda, basi ni la kuvunda halina ubani!, kama muda wa CCM kuondoka ukifika, CCM itaondoka tuu!, bahati nzuri iliyonayo CCM, ni kuendelea kuutegemea mtaji mkubwa wa ignorance ya Watanzania, hivyo 2015, tutaipa tena, na tena na tena mpaka litimie line neno kuwa CCM itatawala miaka 100 au milele kabisa!, kwa sababu Watanzania ni miongoni mwa watu majuha wa kupindukia ambao tunakwenda kinyume kabisa cha ule msemo wa "you can fool some people, sometime!, but you can't fool all the people all the time!, "We have all been fooled all times", na 2015 tutaichagua tena!. Mtakao bisha, bisheni tuu for the sake of kubisha, ila ukweli mchungu ndio huu!.
Pasco.

Mkuu 2010 ni nani aliyeichagua CCM? Kwani kila unaemgusa anakana yeye kuichagua CCM. Mambo siyo rahisi kama unavyofikiria, uchaguzi wa 2015 ni exceptional usiulinganishe na chaguzi zilizopita, kwa kifupi patachimbika.
 
kwa kweli mkuu lazima Pachimbike
 
Uchaguzi wa 2015 lowassa aujua mziki wake, utakuwa na mchuano mkubwa sana
 
Mkuu 2010 ni nani aliyeichagua CCM? Kwani kila unaemgusa anakana yeye kuichagua CCM. Mambo siyo rahisi kama unavyofikiria, uchaguzi wa 2015 ni exceptional usiulinganishe na chaguzi zilizopita, kwa kifupi patachimbika.
Sisi wengine, yetu macho na masikio, tukisubiri kusikia na kuona hiyo "patachimbika!".
Pasco.
 
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu na mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, amesema kuwa iwapo serikali zote mbili; ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar, zitatekeleza kwa usahihi maelekezo ya mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) juu ya suala la ajira, chama hicho kitashinda kiurahisi katika uchaguzi mkuu wa 2015.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana kuhusu uchaguzi wa Kenya, Lowassa alisema amefurahishwa na jinsi Wakenya walivyolichukulia tatizo la ajira kama moja ya ajenda muhimu katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Alisisitiza kuwa, kama CCM nayo italichukua tatizo la ajira kwa vijana kama moja ya ajenda yake, kitashinda kwenye uchaguzi mkuu ujao kwa urais kabisa.
"Nimefurahi wenzetu Kenya wameliona tatizo la ajira kama moja ya ajenda muhimu katika uchaguzi wao. Nimefurahi Waziri Mkuu Odinga alieleza jinsi serikali yao ilivyojaribu kulishughulikia suala hili," alisema Lowassa.
Alisema CCM imepiga hatua kubwa, kwanza kwa kukiri kwamba suala la ajira kwa vijana ni tatizo na kutoa maelekezo kwa serikali kulishughulikia.
"Moja ya maazimio ya mkutano mkuu wa CCM ni juu ya suala la ajira, na katika kikao cha Halmashauri Kuu hivi karibuni, tulilijadili kwa kina tatizo hili, na kwa kweli kama serikali zetu hizi zitatekeleza maelekezo yake, sina shaka yoyote CCM tutashinda kiurahisi 2015," alisema.
Lowassa ambaye amekuwa msemaji mkuu wa suala la ajira kwa vijana akiliita kuwa "ni bomu linalosubiri kulipuka", aliongeza kuwa uamuzi wa vikao hivyo ukitekelezwa vizuri utaifanya CCM iingie kwenye uchaguzi mkuu ikiwa na majibu sahihi yaliyokwishajibiwa juu ya tatizo la ajira kwa vijana.
"CCM imeanza kulishughulikia ili tusiulizwe na vijana 2015, tuangalie uchaguzi wa Kenya, hii ni moja ya ajenda muhimu katika kujinadi," alisema.
Alisema kilimo ni moja ya eneo ambalo linaweza kwa kiasi kikubwa kutatua tatizo hilo pamoja na kwamba bado anaamini kuwa elimu ni muhimu kabla kilimo kwanza.
Aidha, alisema viwanda vikubwa vya nguo ni eneo jingine ambalo linaweza kwa kiasi kikubwa kusaidia upatikanaji wa ajira kwa vijana.
"Hii inawezekana kabisa, viwanda vya nguo ndiyo vyenye kutoa ajira kubwa, tusingoje mpaka vijana waje kutuuliza 2015," alionya Lowassa ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa watu wanaotaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Kauli hiyo ya Lowassa imekuja siku moja tu baada ya Shirika la Utafiti la Synovate kutoa matokeo ya utafiti wake yanaoonesha kuwa chama tawala CCM kimeongezeka umaarufu ambapo asilimia 52 ya wananchi waliohojiwa wamesema wangependa kujiunga nacho.
Ama kwa upande wake, Lowassa kwa mujibu wa utafiti huo umaarufu wake kuelekea 2015 umepanda kwa asilimia sita na kufikia asilimia 7 akiwa miongoni mwa vigogo watano wa juu wanaopewa nafasi ya kushinda urais iwapo uchaguzi ungefanyika leo.
Lowassa kwa mujibu wa utafiti huo anatanguliwa na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli mwenye asilimia nane, Zitto Kabwe wa CHADEMA na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wenye asilimia tisa kila mmoja na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa mwenye asilimia 17.

h.sep3.gif
source: Tanzania daima

[TD="bgcolor: #ffffff"]
Lowassa atoa masharti CCM

na Mwandishi wetu

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"]
amka2.gif
[/TD]
 
Lowasa ni waziri mkuu aliyeondolewa kwa rushwa. Walio jiuzuru ni kama Sumaya, Warioba, Malecela n.k. Waandishi wa habari mnaniudhi eti aliye jiuzuru
 
Back
Top Bottom