Lowassa aitabiria CCM Ushindi, Uchaguzi Mkuu 2015

Lowassa aitabiria CCM Ushindi, Uchaguzi Mkuu 2015

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
1,832
Reaction score
566
Waziri Mkuu wa Zamani na Mbunge wa Monduli aliye jiuzulu kwa Kashfa ya Ufisadi,Mh Edward Ngoyai Lowassa,ameendeleza ndoto zake za Mchana,kwamba endapo CCM itatekeleza kwa usahihi Maagizo na Maelekezo ya Mkutano Mkuu wa Ccm,basi itakuwa ni rahisi kwa Chama hicho kushinda Uchaguzi ujao bila shida.!

Source: Gazeti la Jambo Leo!
 
Waziri Mkuu wa Zamani na Mbunge wa Monduli aliye jiuzulu kwa Kashfa ya Ufisadi,Mh Edward Ngoyai Lowassa,ameendeleza ndoto zake za Mchana,kwamba endapo CCM itatekeleza kwa usahihi Maagizo na Maelekezo ya Mkutano Mkuu wa Ccm,basi itakuwa ni rahisi kwa Chama hicho kushinda Uchaguzi ujao bila shida.!

Source: Gazeti la Jambo Leo!

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli......
 
Maelezo yenyewe ya mkutano mkuu ndio yalikuwa ni kuitukana chadema Kama wanavyofanya sasa badala ya kutekeleza ahadi zao za 2010
 
Japokuwa amejivika viatu vya shehe Yahaya, lakini anakiri kwamba CCM itashindwa, unless watekeleze hayo masharti yake?
 
Hakuna njia nyingine ya kuipatia ushindi magamba zaidi ya kutekeleza ahadi zake. Hayo mengine kama maneno ya fisadi Lowasa ni maneno ya mfa maji. Mkutano mkuu haukuwa na lolote zaidi ya kutafuta na kujadili namna ya kuididimiza CDM. Matusi wanayo itupia CDM katika mikutano wanayo fanya ndio maelekezo ya mkutano mkuu wa magamba. Aache kuudangana umma.

NARUDIA TENA; HAKUNA NJIA YOYOTE INAYOWEZA KUIPATIA USHINDI CCM A.K.A MAGAMBA ZAIDI YA KUTEKELEZA AHADI ZAKE ZA TOKEA 2005..
 
mimi naona kaitabiria ushindi chadema kwani ccm haiwezi kutekeleza lolote inaloahidi!
 
Kimbunga. Sasa hapo unamdanganya nani mgeni nchini,Ndg.Lowassa alistaafu lini zaidi ya kujiuzulu kwa kashfa ya ufisadi wa Richmond? Mkutano mkuu haukupanga kuwaondoa wala rushwa na watoaji?
 
Last edited by a moderator:
Huyu nae keshakuwa mzee wa matamko, sasa hivi atageuka vuvuzela kama mengine!
 
Naona Lowasa hataki kupotea kwenye ulingo wa Siasa.....
 
Huyu ni ndoto inamsumbua tu!
Atajaanguka na presha huyu na asiamini yatakayotokea kwa macho yake!
 
Chadema kuingia ikulu ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano! Haitawezekana mara mia elfu kukiachia chakula cha watoto wako kwa mbwa mwenye njaa wewe mzazi utaönekana mjinga na hamnazo kichwani mwako!
 
Pia asisahau kuikumbusha CCM kutimiza azimio la kumvua magamba ndani ya siku90 vinginevyo haitashinda.
 
Chadema kuingia ikulu ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano! Haitawezekana mara mia elfu kukiachia chakula cha watoto wako kwa mbwa mwenye njaa wewe mzazi utaönekana mjinga na hamnazo kichwani mwako!

kama ngamia aliweza kuingia mjini Yelusalemu kwa kupita kwenye tundu la sindano baada ya lango kuu kufungwa pamoja na kwamba ilikuwa ni kwa shida sana kwa sababu alikuwa analazimika kuinama.Hata CHADEMA wataingia ikulu hivyo hivyo.
 
Kuna habari nyingi kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa Lowasa kaitabiria CCM ushindi 2015, ukiangalia Lowasa kaweka condition kuwa ili ushindi upatikane ni Lazima itengeneze ajira ili kupata mvuto mbele ya jamii. Ukweli wa mambo ni kwamba CCM hawana uwezo huo kwa sasa na zaidi ni kuzidi kuwanyima Vijana fursa za kufanya kazi na kulitumikia Taifa lao ( Issue ya Gesi ya Mtwara ni Mfano Bora).

Kama Gesi ingeandaliwa mazingira mazuri ya kubakishwa Mtwara implication yake ni kwamba Vijana wengi wa Kusini wangepata ajira hata kama zingekuwa ni ajira za muda mfupi tu na hivyo kufanya wimbi la Vijana kukimbilia mijini kupungua kwa kiasi kikubwa na opengine kurtumia mianya hiyo kujitanua kwa CCM kuwa wametengeneza ajira. Suala la Viongozi wao kusimama kwenye majukwaa na kusema kuwa ajira zimeongezeka kwa kuwa hata wingi wa Bar umeongezeka ni ujinga na dharau kubwa sana kwa wananchi.

Kwa ufpi sana ni kwamba, kwa kuwa CCM hawataweza kutengeneza ajira hizo hadi kufikia 2015 ni sahihi kabisa kuhitimisha kuwa Lowasa kaitangazia Kiama CCM na sio ushindi kama wengi wetu tunavyoshawishiwa. Karibuni Pro-CCM
 
Ohoooo Mods sasa mbona mmeiunganisha tena? Hii thread ni ya upembuzi sio kwamba nimeandika walichokiandika hao....mmh haya tuendelee na show
 
Back
Top Bottom