Wana Jf, jana usiku nikiwa ni melala, kiusingizi kikanichukua kama tulivyo zoea kusema. Nikiwa ktk usingizi mara nikajikuta nikiwa katika mahojiano na lowassa, na mahojiano yetu yalikuwa hivi.
Twijuke. Mheshimiwa pele na majukumu
Lowassa: Ashsante kijana
Twijuke: Mzee wangu naona fahari kukaa meza moja nawe lakina pia nafasi hii adim inayoliliwa na wengi, mzee wangu sina mengi sana bali machache ambayo ningependa kujua juu yako.
Lowassa: Kama yepi hayo kijana ungependa kujua
Twijuke : Mzee wangu kwanza binafsi ningependa kujua kuhusu Richimond, kwani yamenenwa mengi kuhusu zabuni iliyo tolewa kwa kampun ile ya kufua umeme inasadikiwa ulitoa upendeleo na wengine wanaenda mbali na kusema kuwa wewe ndo uliye ileta hapa nchini ile kampuni je! nikweli
Lowassa: Sikiliza kijana kilchotokea kati yangu na mwenzangu kwenye jambo lile la Richimond, ni sawa na babako na mamako wapo kwenye gari moja na mwedeshaji wa gari lile ni babako, na wakiwa safarini babako anamgonga mtu anakufa, sasa babako na mamako wanakubaliana kuwa kwamba hii ni kesi na hivyo tukihojiwa tuseme mama ndo aliye gonga ili babako aweze kushugulikia mabo na hatimaye kumaliza kesi kuliko babako kuwa ndani na mamako ahangaike. Umenielewa?
Twiujuke: Hapa mzee wangu nimekuelewa ila umenifumbua macho japo jibu ni tata linahitaji king'amuzi. Mzee wangu ebu nambie, baada ya misukosuko yote hiyo badaye watu wamezusha kuwa eti wewe na Jk hampatani na sasa kila mtu na mabo yake, je ni kweli?
Lowassa: Sikiliza kijana, achana na mambo ya magazeti, Jk ni bwana mdogo na ni rafiki yangu kitambo, mahusiano yangu naye si ya njiani, mimi ndo nimemfikisha hapo alipo na nakuibia siri, kitendo cha watu kuona hatuelewani hilo ndo hitaji letu.
Twijuke: Aasante sana mzee wangu kuning'amua, ebu nambie mzee wangu kuna suala hili la wewe kuutaka urais mwaka 2015
je unalizungumziaje!
Lowassa: hilo la mimi kuutaka urais halihitaji miwani.
Twijuke: Mara nikastuliwa na Alarm kumbe mida ya kwenda kuusaka mkate ikwa imewadia, ndugu yangu nilikuwa na shehena ya maswali lakini ndo hivyo tena.