Watu waliojitambulisha kuwa wana uhusiano na Lowassa, wamevamia nyumba ya mtu Tegeta na kutaka kuibomoa. Baada ya kufuatiliwa, mwanamke mmoja amesema kuwa ni ndugu wa Lowassa, wametumwa na Lowassa kubomoa hiyo nyumba
Hii ndiyo picha halisi tulipofikia. utawala wa sheria unawekwa kando kilicho baki niutawala wa wenye nguvu. unaweza kuona mtu anafanya jambo baya kabisa la uvunjifu wa sheria, kwa kisingizio cha "unajua mi ni nani? au unajua mie mtoto wa nani? n,k". na akishataja yeye ni mkubwa fulani au ana uhusiano na mkubwa fulani, sheria hufyata mkia. hiyo ndiyo sababu na hao wanaosemekana kuwa ni wahuni wa mjini kwa mjibu wa ndg.Bashe, waliona watumie hilo jina la Ndg Lowassa ili waogopwe, na hatimaye wafanikishe hila zao. Watanzania amkeni kukataa tabia hii. sheria na utaratibu wa kistaarabu utumike msikubali kkuteswa na majina kama walivyo fanya watu wa tegeta. nawashukuru sana.