Lowassa acha kuhadaa Watanzania, sema ukweli wako juu ya kuchukia umasikini

Ulipata pia kutafakari utajiri wa Tanzania ukalinganisha na umasikini wa wananchi wake? Ama utafiti wako umeufanya Monduli tu?

Unajibu kama siyo msomi bana! Lowassa amekuwa mbuge na waziri kwenye wizara tofauti zaidi ya miaka 20 na hakuweza hata kupunguza umasikini jimboni kwake, Monduli. Je ataweza vipi? kuondoa umasikini nchi nzima. Kweli ushabiki unapunguza uwezo wa kufikiri.
 
ukisema hivyo mbona mwl nyerere hakufanya hayo mkoani mara?kwahiyo nyerere hakuwa mchapakazi?Kiongozi mzuri ni yule asiyekuwa na upendeleo acheni kuudanganya umma.Usimamizi wa shule za kata uliufanya wewe?na kile chuo kikuu cha dodoma pia ulikisimamia wew?hebu kuwa thinker na usifanye ushabiki humu jf
 
Acheni mambo ya kufikirika! I know Lowassa in person. This man is not rich, he is a man of welfare, he is a hard working man, his children are also hard working. Amekuwa PM akiwa na what we call a hut/nyumba ya kawaida tu. Hakuna Tajiri anangojea nyumba ya kifahari ijengwe na serikali, amabyo ndiyo aliyonayo hivi sasa. Ana ranch pale Handeni, hizo ndiyo juhudi za kazi, sasa mnataka asijibidishe? Mbona hiyo ofisi yake ya Mikocheni iko kama godown -ndiyo utajiri huo?. Tofautisha utajiri na welfare.
This man amejaliwa diplomacy-ukiwa na fedha utasaidiane naye kwenye harambee za maendeleo ya jamii penda usipende-sasa shida iko wapi?
This man akiwa waziri wa ardhi nilimkuta na volckswagen sasa ulitaka abaki nayo asinunue VX hadi leo?
Na hiyo Monduli mbona more than 70% ina maji safi na salama! Ni wapi ulikuta mpaka leo wilaya ikawa na 100% ya wananchi kuridhika kwa huduma hiyo?
Basi bwana!
 
Tatizo la wengine humu wanataka kumbilia matusi badala ya kueleza hali ya mgombea binafsi.Mi nafikiri wale wanayoyajua vema majimbo ya hawa wagombea waendelee kutujuza kwa kina.Na humu JF si mahala pa ovyo kama huko kwenye FORUM nyingine.
 
Mchukia umaskini ameshindwa kuwawezesha watu wa eneo dogo la monduli kuwa na hali nzuri na kuwa na ufugaj bora kuliko wafugaj wa maeneo mengine. Maasai wa monduli ilikuwa wawe role model - mfano kwa Maasai wengine. Lakini sivyo.

Sasa kwa Tanzania atakuwa na lipi jipya? Hamna lolote.

Zaid zaid atawatuma hao wafugaj wavamie maeneo mengine ya nchi wakaendeleze ufugaj wa ovyo na mwisho kufanya Tanzania nzima ya kufugia ng'ombe kiholela holela tu.
 
Unajibu kama siyo msomi bana! Lowassa amekuwa mbuge na waziri kwenye wizara tofauti zaidi ya miaka 20 na hakuweza hata kupunguza umasikini jimboni kwake, Monduli. Je ataweza vipi? kuondoa umasikini nchi nzima. Kweli ushabiki unapunguza uwezo wa kufikiri.

Kikwete kawa rais wa nchi kwa miaka almost kumi, amefanikiwa vipi kuwatoa watanzania kwenye hali waliyokuwa nayo miaka kumi iliyopita kuwasogeza pengine?
 
Wafugaji kwani ni maskini? Wale wanamiliki utajiri wa mifugo ukitaka kuamini badili mifugo kuwa fedha uone.
 
Mbwa anapendwa na mzungu, japo mzungu hali mbwa na wala mbwa sio mlinzi wa mzungu.

Hiyo administration ilifelishwa na akina nani, kama na yeye sio mmoja wao! nadhani kuna kitu kinapungua sana hapa. monduli ni jimbo ambalo mkataa umasikini amelitumikia muda mrefu sana. sasa kama alishindwa muda wote huo kuwaondolea umasikini na badala yake akawa anawaibia mpaka hela za miradi, ataweza huku?. Lowassa ni mwizi tu na wala sio wa kumwonea haya hata kidogo.

kwa kikwete chalinze hakuna maji ya uhakika sembuse monduli kwa Lowasa .. amafanya meengi ila kwa kuwa hamumpendi hamuwezi ona wamasai wanamkubali na watamnyeshea kura kama mvua ya mawe. wewe mbunge wako ameondoa matatizo uote ya wananchi?
 
Ww unaona viongozi ni bora kuliko watanzania wa hali ya chini kama wewe, mbona unakuwa mkali sana au babako alikosa nyumba nn, Elimu ndogo ya Mbowe ndo imewafikisha hapo eti alijiona mjanja kubadilisha gia angani na nyie mburula makofi pwa pwa pwa!! ss Dr.slaa kaondoka Prof.Lipumba kaondoka- kisa tu eti Lowasa anapesa zake, kudadeki sasa mtabadilishia gia chooni.

mbonna kama we ndo mbulula unayeshabikia mafisadi waliobaki ccm bora lowasa ameamua kutoka. tumeshaamua mabadiliko huko mnachosha akili tuu hakuna kurudi nyuma
 
Unajibu kama siyo msomi bana! Lowassa amekuwa mbuge na waziri kwenye wizara tofauti zaidi ya miaka 20 na hakuweza hata kupunguza umasikini jimboni kwake, Monduli. Je ataweza vipi? kuondoa umasikini nchi nzima. Kweli ushabiki unapunguza uwezo wa kufikiri.

kwetu bora sehemu ya choo iliyohamishiwa chumbani kuliko kulikobaki choo kixima
 
Kwa kweli Bumbuli na Arusha leo wamenifurahisha! Watanzania tuungane tuhakikishe ikulu inakwenda kwenye mikono sahihi ya Magufuli!
#HapaKaziTu kwa maendeleo!
 
Wafugaji kwani ni maskini? Wale wanamiliki utajiri wa mifugo ukitaka kuamini badili mifugo kuwa fedha uone.

aliyewaambia wamasai masikini nashangaa tena wanajitibu hospital za gharama na wanamudu waone na lubega zao walivyo lakini ni matajiri sana
 
Mchukia umaskini ameshindwa kuwawezesha watu wa eneo dogo la monduli kuwa na hali nzuri na kuwa na ufugaj bora kuliko wafugaj wa maeneo mengine. Maasai wa monduli ilikuwa wawe role model - mfano kwa Maasai wengine. Lakini sivyo.

Sasa kwa Tanzania atakuwa na lipi jipya? Hamna lolote.

Zaid zaid atawatuma hao wafugaj wavamie maeneo mengine ya nchi wakaendeleze ufugaj wa ovyo na mwisho kufanya Tanzania nzima ya kufugia ng'ombe kiholela holela tu.

tusidanganyane hapa huku kuna wasomi habari ya kudanganyana muache hao walioongoza miaka 8 bila lowasa kuwa na madaraka weshindwaje kumaliza hiyo migogoro?
 
Najiuliza tu kama amekuwa mbunge wa monduli kwa miaka 30 watu baado wanashirikiana maji na mifugo. Ameshindwa kuwahamasisha wachimbe vyoo, anapata wapi ujasiri kusimama hadharani eti anachukia umasikini!!!

umasikini mbaya kweli lazima auchukie, tena hasa umasikini wa akili. unafikili ni swala la kawaida kwa watu waliojenga chama kwa miaka 23 tokea 92 kikiwa na usajili wa muda 3/9/1993 kupata usajili wa kudumu akaweza kuwateka kwa siku moja na kuwanunua wote ni kazi ndogo? akisema anauchukua umasikini anamsuta Mbowe na genge lake kuwa ameweza kuwateka kwa utajiri wake ndani ya siku moja. kweli anauchukia umasikini.
 
Vijana wa Tanzania wengi ni wajinga sn. Ona kama mtoa post huyu, hakumbuki hata kuwa yy ni mtanzania na anajukumu la kuwa mzalendo. Tunaacha kujadili maswala ya umeme ambyo nchi ipo gizani tangu July 28, mpaka leo tunaanza kujadili mada ambazo tumetumwa na waliotoa hela zao wakanunua tablet wakawapa. Shame
 
Nimezunguka karibu jimbo zima la Monduli. HAKUNA MAJI, UMEME, VYOO,Kuna Umasikini wa kutosha! Nimepita Eslalei, Mswakini, Mbuyuni, Nanja, Mti mmoja, Losimingori hali ni mbaya.

Najiuliza huyu lowassa anayegawa mapesa nchi nzima anashindwaje kuendeleza jimbo lake?

Jaribu kuzunguka Chato pia
 
Jaribu kuzunguka Chato pia

Mkuu hukujua hilo? Hana shida na Monduli na umaskini wake ambo anauchukia anashida na kujipreted il kuhadaa wasiojua Monduli. Janami Monduli kuna shida! Afadhali sehemu nyingine watu wananyanganyana maji na ngombe waliowazoea, Monduli wanaviziana maji na tembo, hatari kwa usalama, mtu asiporudi nyumbani tafuta ushahidi wa nguo maana hiliwi na tembo.
 
mi naamini watanzania tuamke tuwapime wanasiasa wetu,kwa ujumla wengi wao ni wadanganyifu kwani lengo lao ni kujitafutia riziki yao na watoto wao,haiwezekani mtu aambie watu eti kama atachaguliwa ataondoa umaskini kwa watanzania ili hali kawa mbunge jimboni kwake kwa zaid ya miaka 20 lakin kashindwa kuwaondolea wananchi wake umaskini au kero mbalimbali.

Ama kweli umenena muungwana,katika watanzania wachache waliojaaliwa kuona mbali na wewe ni mmojaw wao,ila watanzania tumerogwa kwa kuwa hatufanyi upembuzi yakinifu kufuatia mwenendo wa siasa za nchini na wanasiasa wetu zaidi tumekalia ushabiki wa vyama na mtu anayegombea, kuliko kujiridhisha kama mgombea kweli anatufaa? je kweli anaweza kutuletea mabadiliko tunayoyataka?Kweli anaweza kusimamia utekelezaji wa sera nyingi nzuri za vyama vyetu? tunaishia kutupiana maneno makali wao wanasiasa wanatucheka na kutuona mazuzu.

kwa Mwaka huu tumeliwa si UKAWA wala CCM watakaotuletea mabadiliko, CCM washapenyeza ndani ya upinzani wanajifanya wanataka kuleta mabadiliko walikuwa wapi miaka yote waliyokaa katika uongozi? wapinzani wamedanganywa kidogo tu wametuuza watanzania.Mwaka huu ukichagua magufuli ni CCM ukichagua Lowassa ni CCM tujipange baada ya miaka kumi ili tujaribu kufanya hayo mabadiliko tutakayo kwa mwaka huu tumechemsha.:crying::crying::crying:
 
Back
Top Bottom