Wana jamvi,leo nimeona nilete swali hili kwenu,hivi mbunge wa Monduli na Waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Edward Lowassa hawezi kutafuta urais bila kumchafua Rais aliyeko madarakani na familia yake??
Wana jamvi,kwa muda mrefu sasa imekua huyu bwana na wafuasi wake wamekua wakimchafua mh. Rais na kumtukana yeye na familia yake kama njia yao ya kunadi uzuri wa mtu wao. Wamesikika wapambe wa karibu wa bwana Edo wakisema JK ni dhaifu,serikali imemshinda,mwanae Ridhiwani kuzushiwa kumiliki kila ghorofa mjini,kila sheli ya mafuta,kila hoteli mpya,kukamatwa na dawa za kulevya,kauli za kuwa Edo akipata nchi akina Riz moko wahame nchi n.k. Kauli hizi wakati mwingine huambatana na matusi ya nguoni kutoka kwa wafuasi wa Edo kwa wanafamilia wa JK.Hapo ndipo tunauliza,Mzee Lowassa hawezi kutafuta urais bila kumdhihaki Rais aliyeko madarakani???
Ikumbukwe kuwa Tanzania imekua na utamaduni wa viongozi wetu kuheshimiana.Mzee Mwinyi hakupata urais kwa kumuhujumu Mwalimu, mzee Mkapa hakupata urais kwa kumtukana Mwinyi, wala Jakaya hakutafuta urais kwa kumtukana mzee Mkapa. Utamaduni huu ndio umeendelea kujenga misingi mizuri ya nchi yetu.Tunajiuliza,hii style ya huyu bwana Edo imetoka wapi?
Kweli ni lazima kumtukana Rais ili wewe upate urais??Kumbukeni wana jamvi kuwa urais ni taasisi kubwa.Inahitaji hekima na busara.Mtu mwenye kuonesha visasi kabla hata hajapata huo urais akipata itakuwaje??
Rais Kikwete aliwapa nafasi watu ambao wengine walimpinga kufa na kupona na kumpiga vita asiwe Rais. Akina Nape Nnauye, Salim Ahmed Salim, Joseph Sinde Warioba, Butiku na hata Mzee Mangula. Huo ndio uongozi wakuu. Sasa hii style mpya inatutisha sana.
Urais unatafutwa kwa kumtukana Rais na familia yake????
Yangu macho.