Love juakali alivyomlipa Wema mwanamke mwenzake aliyedai hampendi kwasababu ana sura na umbo baya

jamaikatz

Member
Jul 11, 2023
51
132
LOVE JUAKALI ALIVYOMLIPA WEMA MWANAMKE MWENZAKE ALIYEDAI HAMPENDI KWASABABU ANA SURA NA UMBO BAYA.

Unaweza kushangaa! unaweza usiamini lakini watu wema bado wapo! kama matukio yanavyojieleza pichani. Siku kadhaa zilizopita content creator mmoja wa hapa Dar es salaam aliongozana na Love Juakali hadi kwenye duka moja linalojihusisha na uuzaji wa nguo za wanawake zikiwemo nguo za ndani n.k

Kama ilivyokawaida ya content creators wakataka kutengeneza content na mojawapo ya content waliyoichagua ni kumhoji mmoja wa wateja waliyemkuta dukani hapo kama anamjua Love Juakali na anampenda kiasi gani lakini wakati huo Love alitakiwa kujificha sehemu ili anayeulizwa asimuone. Basi, huyo dada baada ya kuulizwa kama anamfahamu Love Juakali alisema anamfahamu na alipoulizwa anampenda kiasi gani alisema

"Love Juakali namfahamu lakini simpendi hata kidogo kwasababu ana sura mbaya, hana shepu ameumbwa-umbwa tu, havutii kwenye TV hata nikikutana nae siwezi kusita kumwambia kama simpendi, kwasababu huo ndio ukweli ni sura mbaya na umbo lake ni baya"- alisema

Akiwa anaendelea kuelezea hisia zake jinsi anavyomchukia, ghafla Love Juakali alimuibukia nyuma yake akiwa na tabasamu mwanana utadhani hajasikia chochote baada ya kumuona Love mwanadada huyo alishtuka misili ya mtu anayetaka kung'olewa roho, akashusha pumnzi kisha akaulizwa tena, unampenda Love Juakali?

Akasema "Nampenda sana, huyu ni shoga yangu, ni rafiki yangu, ni mwanamke mwenzangu siwezi kumchukia, ni Mwigizaji mzuri anapendeza kwenye TV hakika anajua kuigiza na ninampenda sana".

Baada ya maneno hayo Love Juakali aliendelea kutabasamu tu akaigiza kama hajasikia chochote, akamnunulia vitu vya elfu 92 akampa na pesa ya nauli kisha akamwambia "Nimesikia maneno yako dada, lakini hata kama wewe haunipendi mimi nakupenda sana tena sana".

Kwa aibu mwanadada huyo akajizungusha-zungusha kama feni mbovu akitafuta upenyo wa kuutorosha uso wake uliokuwa umejaa aibu na baada ya kupata upenyo huyoooo akatokomea kusikojulikana .
 
1711629788347.jpg
 
Wote ni usanii tu hapo, mwanamke aambiwe hayo maneno ya kumbagaza na bado amnunulie vitu!! Huo ni uongo labda bwana kontenti krieta ndiye alifanya hivyo ili kupamba kipindi chake
 
Thamani ya mtu haipo kwenye mtu wa nje (mwili) bali ipo kwenye mtu wa ndani (roho na nafsi) 🤔
 
Thamani ya mtu haipo kwenye mtu wa nje (mwili) bali ipo kwenye mtu wa ndani (roho na nafsi) 🤔
Hapana. Thamani ya mtu ipo kwenye muonekano wake, ndiyo maana mamiss wote wana muonekano mzuri. Na mamiss wanalipwa hela nyingi kwa huo muonekano.

Sura na shepu mbovu ya love juakali inabidi ujibanze kwenye vitabu vya dini kwanza ili kuvifunika.
 
Hapana. Thamani ya mtu ipo kwenye muonekano wake, ndiyo maana mamiss wote wana muonekano mzuri. Na mamiss wanalipwa hela nyingi kwa huo muonekano.

Sura na shepu mbovu ya love juakali inabidi ujibanze kwenye vitabu vya dini kwanza ili kuufunika.
Wewe mtazamo wako ni wa kibinadamu. Mungu haangalii kama mwanadamu anavyoangalia. 🤔
 
Wewe mtazamo wako ni wa kibinadamu. Mungu haangalii kama mwanadamu anavyoangalia. 🤔
Sasa huo uwezo wa kimungu sisi wanadamu hatuna. Uwezo tulionao ni huu wa kutumia macho. Hayo ya Mungu tumwachie mwenyewe.
 
Hapana. Thamani ya mtu ipo kwenye muonekano wake, ndiyo maana mamiss wote wana muonekano mzuri. Na mamiss wanalipwa hela nyingi kwa huo muonekano.

Sura na shepu mbovu ya love juakali inabidi ujibanze kwenye vitabu vya dini kwanza ili kuufunika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom