Louis Chevrolet mbunifu wa magari na utajiri wa makaburini

dengue f

Member
Jun 4, 2017
17
75
Nilipata kusoma sehemu kwamba; Makaburi ni sehemu yenye utajiri zaidi, Kule kuna Viwanda ambavyo havikujengwa, Biashara ambazo hazikuanzishwa, Mashamba ambayo hayakulimwa, Safari ambazo hazikufanyika, Vitabu ambavyo havikuandikwa na Mafanikio mengi tu yaliyojaa. Kwanini? Kwa sababu waliolala hawakuvifanya, Wamelala na mawazo, malengo na fikra zao!
Louis Chevrolet ni mmoja kati ya watu waliolala huku wakiwa wametimiza ubunifu wao, Ingawa walikufa wakiwa fukara wa Mali.

Ukitazama jezi za timu ya Manchester United utaona jezi zao zimeandikwa Chevrolet, Hiyo ni kampuni maarufu ya magari inayoidhamini timu hiyo.

Mwanzilishi wa kampuni hilo ni Louis Chevrolet, ingawa alikuwa tajiri mkubwa sana na mbunifu wa magari wa aina yake kupata kutokea duniani lakini alikufa masikini mno akiwa na umri wa miaka 63(Kwa wakati huo ilionekana kafariki akiwa kijana).

Chevrolet alizaliwa usiku wa Christmas mwaka 1878 katika jimbo la La Chaux-de-Fonds, Switzerland. Baba yake alikuwa ni fundi saa. Akiwa na miaka 8 tu familia yake ilihamia ufaransa. Akiwa kijana mdogo kabisa alibuni mashine ndogo ya kukamulia zabibu na kutengeneza mvinyo.
Wakati huo huo alitengeneza baiskeli aliyoipa jina Frontenac— alitengeneza nyingi Zaidi na kupata kipato Zaidi. Mwaka 1902 alihamia Marekani na kupata kazi kama dereva wa mashindano ya magari katika kampuni ya Fiat.

Alitambulika Zaidi alipomshinda bingwa wa wakati huo Barney Oldfield ambaye alikuwa ni maarufu Zaidi.
Wakati wa Mapumziko ya mashindano ya magari alitumia muda wake kubuni na kuchora michoro ya magari. Mwaka 1906 alikutana na dereva mwingine wa magari ya mashindano, Walter Christie mara wa kawa marafiki. Hapo ndipo Chevrolet alisaidia kuunda gari aina ya V-8 kwa ajili ya mashindano.

Uwezo wa Chevrolet kama dereva, fundi wa magari na mbunifu wa aina yake ulivutia watu wengi. Kampuni kubwa kwa wakati huo la General Motors liliingia katika shida kubwa la kukosa wataalamu. Mkurugenzi wa General Motors alimwomba Chevrolet amsaidie kubuni magari yatayoweza kuendana na ushindani wa soko! Kwa usaidizi Durant alianzisha kampuni yako Chevrolet Motor Co. ilianza kuzalisha magari maarufu kabisa ya ‘Chevrolet’

Durant alikuwa na mawazo ya kupambana na Henry Ford kwa kutengeneza magari ya bei rahisi, Chevrolet alitaka kampuni itengeneze magari ya kifahari na yenye bei mbaya! Utofauti huo wa mawazo ulipelekea Chevrolet aachane na kampuni aliyoianzisha kwa kuuza hisa zake zote! Alikuwa na ukwasi wa maana, Milionea wa 1913. Durant aliendelea na biashara, alifungua matawi mengi nchini marekani na Canada. Aliweza kumiliki karibu hisa zote za Chevrolet!

Upande wa pili Louis Chevrolet alianzisha kampuni ya Frontenac Motor Corp akishirikiana na swahiba wake aliyeitwa Albert Champion. Haikudumu sana, Ushindani wa soko la magari ulikuwa mkubwa na hatimaye Louis Chevrolet alifilisika!

Mwaka 1933 alienda kuomba kazi Chevrolet Motor Co.(Kampuni aliyoianzisha mwenyewe) na akaajiriwa kama fundi wa kawaida tu wa magari. Jina la ‘brand’ yake ambayo ni maarufu mpaka leo yaani Chevrolet ikaendelea kutumika. Wakurugenzi aliokuwa nao katika vikao sasa ndio wakawa wanampangia kazi za ukarabati wa magari hasa mabovu!
Louis Chevrolet alipata tatizo la damu kuvujia katika ubongo, alifariki dunia akiwa kwa dada yake na kuzikwa 1941 akiwa na miaka 63 huko Indianapolis.

Jarida la The Gentlemen of General Motors mwaka 2000 lilimtaja Chevrolet kama mbunifu wa magari, fundi wa magari na dereva wa aina yake kupata kutokea katika uso wa dunia. Brand yake Chevrolet imekuwa ‘hirizi’ ya biashara chini ya kampuni maarufu la General Motors! Mwaka 2014 waliingia mkataba wa matangazo na timu ya Manchester United kwa kiasi cha milioni 600 dola za kimarekani.
Chevrolet ni kati ya magari ya bei mbaya kabisa kwa sasa, Lakini mbunifu wake alikufa akiwa fukara mno!

Itumie vizuri kila nafasi unayoipata, Historia yako iandikwe kwa wino wa Dhahabu!

Huyu ndiye Louis Chevrolet!
Francis Daudi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tyrex

JF-Expert Member
Oct 15, 2012
1,503
2,000
Ni kama umeanzisha msingi mzuri wa gorofa kubwa ukauza kwa bei ya hasara uliemuuzia akaiendeleza halaf baadae ukarudi kupanga ki apartment kwenye gorofa lilelile

Sent using Jamii Forums mobile app
 

The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
5,469
2,000
Nimejifunza kipaji na juhudi ya kazi visipounganishwa na akili za kibiashara ni upuuzi na utatajirisha wengine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom