Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Wana JF:
Kushindwa kwa siasa kunatokana na sababu za nje na za ndani. Mpaka sasa watanzania wengi wanafikri kuwa Ujamaa ulishindwa kwa sababu za nje. Wanafikri kulikuwa na maadui ambao hawakutaka sisi kuendelea.
Kwa zaidi ya miaka miwili sasa nimefanya kazi ya utafiti na matokeo niliyopata ni kuwa Ujamaa umeshindwa na ulipotezea Tanzania muda wa kupiga hatua kwa sababu ni siasa mbaya. Na hakuna sababu hata moja ya nje yaliofanya ujamaa kushindwa na haya ni maelezo yangu.
Ujamaa ulishika hatamu kati ya mwaka 1967 mpaka 1981. Katika kipindi kulikuwa na matatizo kama vile ukame, vita vya uganda, kuvunjika kwa jumuia ya Afrika mashariki na kupanda kwa bei ya mafuta. Hizi sababu zilitosha kuhujumu siasa za Ujamaa.
Lakini pamoja na hayo katika kipindi hicho hicho, Tanzania ilikuwa ni nchi inayoongoza katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara kwa kupokea misaada. Tulipewa zaidi ya dollar billion 3.
Hivyo misaada tuliyopewa ilikuwa ni mikubwa ya kuweza ku-counter balance, negative impacts ya ukame, kupanda kwa bei ya mafuta, vita vya Uganda na kuvunjika kwa jumuia EA.
Vilevile katika kipindi hicho kulitokea expansion ya viwanda. Wafanyakazi wa viwanda waliongezeka kwa asilimia 8 kwa mwaka lakini uzalishaji wao ulipungua kwa 3.5 kwa mwaka.
Kipindi hiki kilikuwa na uhaba wa biadhaa za viwandani. Na waungwana wengi hapa wanasema kuwa ulitokana na wahujumu uchumi. Lakini sources zangu zinaonyesha kuwa viwanda vilikuwa vinafanya kazi kwa kiwango vya asilimia 45 tu. Je hiyo 55 kwanini hatukuweza kuifikia.
Vilevile Tanzania ikaanza kuwa muagizaji wa chakula kutoka nje. Kwenye nchi kama yetu yenye siasa inayojidai kuwa bora kwanini tuagize chakula?